Unajua tangia mwanzoni nilisema watu waache kutumia sababu binafsi kujengea "Nadharia za matatizo hata kama hayo matatizo hayapo"
Ni kawaida ya watanzania kutengeneza mazingira ya chuki, wivu, pale kwa watu au kundi la watu tusiowapenda au tulioshindwa kufikia kiwango chao.
Mifano ni mingi hapa JF na hata nje ya hapa.
Mfano tangia kule BCS na hata hapa JF watu wamekuwa wakisema Reginald Mengi anakwepa kodi na anadaiwa zaidi ya bilioni 5 kwa kodi ambayo hajalipa na kesi tayari imeshapelekwa Mahakama ya Biashara. Watu tulipouliza tuliambia kuna ushahid mwingi tu na tukaee mkao wa kula kwani kesi itaanza kunguruma, lakini cha kushangaza ni karibia miaka mitatu sasa hatujaona huo ushahidi siyo hapa tu hata mahakamani. Watu wanabakia kusema anatumia jina la Walemavu kuingiza mali zake binafsi, mara kaangiza benzi kwa kuzingizia ni la walemavu. Mtu mwenye akili timamu hawezi kusema kitu kama hicho, jamani tangia lini Mlemavu akaendesha Benzi sembuse baiskeli ya kusukuma.
Hata serikali hutumia nadharia pale inapoona mambo ya wapinzania ni bora kuliko yao. Chukulia mfano, serikali ya CCM inavyowaambia wananchi kuwa tuchagueni kwani wapinzani hawapendi au hawawezi kuleta maendeleo na hata hudhiriki kusema angalieni sehemu zinazoongozwa na madiwani na wabunge wa vyama vya upinzani yalivyo nyuma kimaendeleo, lakini wakibanwa hawana mfano.
Kuna wakati kuna mtu aliwahi pia kulalamika mbona madaktari na Manesi wengi waliosajiliwa ni kutoka Mikoa ya Kaskazini, nadhani aliyekuwa waziri wa Afya kipindi hicho aliwaambia katembelee huo mkoa utaona wana college ngapi za kusomea unesi kwani kila hospitali ina kituo cha kufundishia, na madaktari wengi tulio nao ni wale waliosomea kwenye vituo kama hivi na kuwa medical officer na baadaye kwenda kuongeza elimu hadi kupata hadhi ya Daktari kamili.
Binafsi siungi mkono upande wo wote ule kwa sasa ila ninataka watu wakilete kero basi wawe tayari kutetea kero zao mpaka mwisho na siyo maswala ya kuishia njiani.