Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Mswahili,

Heshima mkuu, una maana gani kwamba prosecutor ni kabila la kaskazini na ameachia kaskazini wenziwe na kumfunga mhaya? au?
 
wandugu,

hii hoja ya ukabila ina mapana na marefu yake,na yote yameongelewa vizuri humu na yameonekana kueleweka.ila it seems like kuna watu wako addicted kupotosha ukweli,labda kwa sababu wazijuazo.

unajua,sisi tofauti na wakenya[na wafananao nao] ni watu wamoja sana...tume soma,fanyakazi,oleana,shirikiana kwenye raha na tabu,kaa vijiweni,tongoza,tongozwa,kunywa pombe,kunywa ghahawa,swali,sali,na kadhalika pamoja na still tunaendelea kufanya hivyo na tutaendelea hivyo[mwenyaazi mungu apishilie mbali dhambi hii]

hivi ni nani asiyejua kwamba elimu ni ufunguo wa maisha? ni nani asiyejua kwamba kazi ni kipimo[utu?]cha maendeleo...ni nani asiyejua kwamba upandacho ndicho uvunacho[kama ngedere hajakuwahi...wakaazi wa pwani mpo?]...na hii ndio inayotufanya waswahili tuendelee au tukwame!

tutaongea kuhusu ukabila hapa mpaka kuchwe...halafu tungamue kuwa hatukulala au pata usingizi, kwa maana hiyo. tukabakia kushindwa fanya kazi nyingine[za maendeleo].

nani alisema duniani...achilia mbali tanzania,hamna ukabila?tatizo ni ukabila unatumika vipi...je, unaleta maendeleo au unayarudisha nyuma?je, unaua watu au unazalisha watu?[wasukuma na wangoni mpo...mnakumbuka vita vya mababu zetu?]namna ya kushindana nao katika hili ni kuaminiana na kushirikiana[kuna watu huogopa kuoa wakina dada wa kihaya..ukiuliza kwanini..hupati sababu za msingi]

halafu,tusisahau kwamba baadhi ya watu wanaousema ukabila[uko hapa au pale]ndio wenye upendeleo wa kikabila!. hebu jiulize...fundi bomba wako ni kabila gani?kinyozi wako je?mwanasheria wako?mkeo[na kwa maana hiyo mwanao]?jirani yako?mlinzi wako?rafiki yako kipenzi?mshirika wa biashara?anayekukopesha fedha ukichacha?na kadhalika. ukijibu haya..utastaajabu!

ukweli ni kwamba wapo watakaoendelea zaidi ya wenzao[si tanzania tu bali duniani kote]...ukiweza soma culture and prosperity kilichoandikwa na john kay ,utayaona baadhi ya yaliyoandikwa humu kwenye forum kama sababu na zaidi. kikuu ni kujifunza "wao wameweza vipi na sisi tushindwe?"

ukiwa nyuma ni busara kufikiria namna ya kufika mbele na si kumsema aliye mbele,kwani "maneno matupu hayavunji mfupa"

asalaam aleykhum.
 
Mzee nafikiri the ishu hasa ni TRA, ambako kama utaisoma kwa makini hii mada utaelewa kuwa ndiyo inayodaiwa kuhusika na kuwa na kabila moja la kaskazini,

sasa unasema eti watu hawataki kuoa kina dada wa kihaya? Una maana gani? na WHY?
 
Mzee nafikiri the ishu hasa ni TRA, ambako kama utaisoma kwa makini hii mada utaelewa kuwa ndiyo inayodaiwa kuhusika na kuwa na kabila moja la kaskazini,

sasa unasema eti watu hawataki kuoa kina dada wa kihaya? Una maana gani? na WHY?

sentensi yangu inasema hivi "kuna watu huogopa kuoa kina dada wa kihaya...ukiuliza kwanini...hakuna sababu za msingi"

maana yangu huu ni ukabila,kwa kuwa wanakuwa na sababu ambazo zimejikita kwenye kuona kabila hili liko hivi wakati yote yako hivyo!

nadhani umenielewa.
 
Mzee nafikiri the ishu hasa ni TRA, ambako kama utaisoma kwa makini hii mada utaelewa kuwa ndiyo inayodaiwa kuhusika na kuwa na kabila moja la kaskazini,


issue ya tra inafahamika sana mzee es,na nimeisoma hapa pia....maoni yangu ni ya jumla juu ya ukabila yanalenga kugusa kila kona ya maisha ya mtanzania[mzanzibari na mtanganyika]
 
Mzee Dar,

Heshima mbele, ninajaribu kukuelewa, but, nafikiri point yako inalalia kwenye idea kwamba huenda kabila linalolalamikiwa lina maendeleo ya binafsi kuliko mengine, sidhani kama that is the ishu hapa,

nafikiri the ishu ni kiongozi wa kabila moja kupata nafasi ya uongozi kwenye shirika la umma na kuwaajiri watu wa kabila lake kwa wingi kuliko makabila mengine, sasa sidhani kwa mantiki hiii hoja ya maendleo ya binafsi kwenye kabila moja inasimama, hapa ni farvortism ndio the ishu, pia hii ndio hasa ishu inayoleta utata huko Rwanda,

sidhani kuwa Tanzania nzima kuna kabila moja tu lenye maendeleo ya binafsi kuliko mengine yote kiasi cha kuhalalisha kujazwa kwao katika TRA, binafsi isna data za TRA, isipokuwa ni kwa kufuatilia huu mjadala tu ndiyo nimejifunza hayo!
 


kumbuka kuwa humu wamesemwa wahaya na watu wa mbeya[yapo makabila mengi huko]wakifananishwa na wachagga....hivyo si kabila moja "lenye maendeleo binafsi" ninaloongelea.

naongelea ujumla mzee wangu!nadhani umenielewa!
 
Mwanakijiji.
vipi interview? au umeingia mitini? tunataka kusafiri hii ni pasaka tunasubiri INTERVIEW NA TRA(JUNGU LA UKABILA).
 
It has turned to be the interview of Mwakijiji and TRA was HOAX!
 
Interview ilivyopangwa imepanguka.. kwanini sasa ni vigumu kuwapata watu wote kwa pamoja kama nilivyokusudia. Hata hivyo bado tunajaribu kuona angalau kufanya mahojiano na mmoja wa viongozi wa TRA kuhusu suala hili na pale itakapowezekana kuwapata wote tutafanya hivyo.
 
Mswahili

Nadhai MKJJ alikuwa anajaribu kutaka kukunyamazisha kwa kukutishia interview so alidhania utatishika- alisahau kuwa mtumzima hatishiwi nyau
 
Makubwa haya! Mwanakijiji nae kawa kama wasomi wa Udsm? nilijua ni Mzumbe product(kichwa).
 
Mazingaombwe mengine ama ............................anyway nafikiri kuna haja ya kuingilia ofisi nyingine zilizoorodheshwa hapo juu ili kujua hawa mafisadi wanaoendeleza ukabila bila aibu wasutwe waache mtindo huo mara moja, kwani panga limeishanyanyuliwa.
 
Dua.

TRA Bado hatujamaliza tulikuwa tunasubiri interview ili tulete hoja zetu naona kuna kanyaboya imechezwa.

ukisikiliza BBC Swahili kipindi cha Dira ya dunia leo hii kuna mtaji wa dola elfu mbili toka BBC waliojitokeza karibu wote ni watu wa kilimanjaro wanagombania hizo pesa sioni kama kuna wasomi toka huko. jee wangekuwa na Professor Warioba sijui kama kungelalika.
 
duh.. waswahili bwana.. sasa mnataka niwadanganye itanisaidia nini..? kama hawataki tena kupatikana nifanyeje niwafunge pingu? Ningekuwa jijini.. believe me... ningewafanyia ile investigative reporting ambayo haijawahi kufanyika TZ bado...! sorry to disappoint you.. but siinamishi kichwa kwa aibu.. move on I do.! ikipatikana nafasi.. sitailazia damu.
 
kukataa kwao kupatikana haionishi kuwa kuna uhalali wa madai ya mswahili na wenziwe?

si bure iko namna hapa
 
Ok MKJJ usijali no problem, wacha tuendelee na office nyengine hii naona ishamalizika - MKJJ kesha kubali kuwa TRA ukabila upo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…