Naam Mswahili, here you go!
Wakti naandika yaliyo juu huenda HUKUSOMA! Naomba ingia deep kwenye topic hii uchambue ofisi nyinginezo mkuu maana umeshatoa data za kutosha on TRA na wenye masikio na macho wamesikia na kusoma. Mbona hugusi Ikulu kuna nini? Kwingineko?
Itapendeza zaidi kuliko kuzodoana na kurushiana madongo badala ya kukata issues. Kweli; tunahitaji kujua ofisi nyinginezo zilizotajwa zinahusikaje na UKABILA ambao ni ugonjwa mbaya. Sioni sababu ya kufungua topics za kuandama Admin au Moderators.
Thanks
Invisible
usiyeonekana,
kwanza,pongezi kwa kuwa mtu mwenye hikma,busara na mvumilivu.....ningekuwa mimi...ningeshatoa onyo kitambo!na kama ukaidi ungendelea...ningetoa sababu,omba radhi...na kuifunga hii mada!.
pili,ningeifunga kwa sababu imeshaonekana kuwa kinachojadiliwa ni chuki,hisia,ushabiki,labda ukabila,labda udini...na mengineyo ambayo hayaleti mwanga wa kuichambua hoja,bali yanagombanisha watu humu....ni kama wamepewa virungu watiane ngeu.
tatu,kuna watu wamewasilisha baadhi ya data juu ya hii mada,lakini inaonekana aidha zimepuuzwa[kwa maana ya kuamsha uchunguzi wa nyingine au la]au hazikuwa na msaada kwa malengo yaliyokusudiwa juu ya hii mada[kwa maana yake halisi na si tuliyoaminishwa].
nne,yanaongewa maneno ambayo kama unatumia busara za kumwelewa mtu,utasema ameshikwa na hasira,anatania,ana utani na mtu,au agh!....lakini inatia shaka...kwani yanajirudia na yanazidi kuwa makali!.
tano,nikapata kujiuliza...kuna watu wako ulaya,sivyo?,...let say ujerumani...skin heads wanawajua?...hivi wanajisikiaje wakiwaona wako kundi mbele yao?. nikajiuliza...hivi...unapokaa kwenye kiti[bus au train]halafu ukainuka kushuka,mzungu akapapangusa kwanza kabla ya kukaa,unajisikiaje?. na maswali mengine mengi!.....
sita,kuna sehemu nshasema tu watu wa fitna siye waswahili!....na ndo maana hatutoendelea kamwe!....wageni watachukua vyetu mpaka kiyama,nasi tutaishi kwao au kufanya kazi kwao tena za hovyo...mpaka kiyama!.kisa ni fitna!
saba,nloyasema yanatosha!kila mtu anayo yake macho na wake uelewa! tumesoma humu vitu vingi,tutachambua wenyewe ndani ya akili zetu na kuikosoa mioyo yetu!.
usiyeonekana!...walaakhi hamna jipya litakaloibuka!...kwasababu halipo! muda utaonyesha hivyo...na majadiliano ndio yatathibitisha!