Mwanakijiji kweli sasa nimeamini ukabila au kamaunavyouita kujuan kupo maana hadi world bank nako kuna kujuana!!!
http://news.bbc.co.uk/2/hi/americas/6558551.stm. Duh sasa hii ni hatari kweli ukabila, kujuana au undugunization sasa naamini upo pia Tanzania. Je sasa tutaumaliza je? kam sio kuupunguza?
Kwanza, hii inaonyesha kwamba kujuana kabla ya kupeana favours always, always kupo, whether ni kwa misingi ya kikabila, kimapenzi, kidini nk. Lakini itakuwa makosa, kwa mtazamo wangu, ku-equate uwepo wa wanawake wazuri sehemu fulani na favour, au kabila fulani na favour, unless una data za kuonyesha kwamba hao wamekuwepo hapo kwa njia za upendeleo! Halafu kama alivyoumbuliwa huyu bwana wa world bank, nasi tunatakiwa kuwa na ujasiri wa kufanya hivyo kwenye hoja zetu, kudhania tu haitusaidii.
Pili, mimi naamini kabisa kwamba in the long run favours hazimsaidii mtu yule anayepewa favours. Wala siyo kitu cha kutamani. Kupata kwa juhudi yako mwenyewe ndiko kunampeleka mtu. Na taifa linapokuwa na watu wa aina hiyo, basi nalo linakwenda mbele na kuyapita mengine haraka. Nitatoa mifano:
- Idi Amin aliwafukuza wahindi akagawa maduka kwa jamaa zake. Leo wapo wamebaki wangapi? Mbona serikali ilianza tena kuwaita iliyowafukuza warudi?
Watanzania tulitaifisha mali za watu kwa itikadi za wakati huo, tukazifanya kuwa zetu. Leo mali hizo zipo? Huko Zimbabwe mnaona kinachoendelea? Mashamba waliyochukua jamaa zake Mugabe yamegeuka kuwa vichaka.
Believe me, ukipewa favour unaweza kufikiri umepata kumbe umepatikana. Ni sawa na kuibia mtihani, unaiambia akili yako kwamba huwezi na kweli unaishia kutoweza.
Lakini muhimu zaidi ni kwamba vitu kama ukabila, rushwa, udini, vinachangia saaaana kudemoralise na ku-misplace juhudi za watu. Msingi wa maendeleo ya nchi yeyote ni watu waliolelewa kwenye misingi ya kupata kutokana na JUHUDI ZAO INDIVIDUALLY! Hivyo ili kujenga taifa, ni muhimu mno kukemea vitu hivyo. Kupata kuwe kunazingatia kanuni zilizowekwa kuzuia mambo ya favouritsm.
Kwa maana hiyo, kama kanuni za kuwapata watumishi zinafuatwa inavyostahili, mimi sitajali, na nasema kwa dhati kabisa, kama idara moja ya Serikali itakuwa na Wandengereko asilimia 50, lakini wanafanya kazi nzuri sana. It could be that Wandengereko wana natural skills na passion na hiyo kazi na ndiyo maana wapo kwa wingi pale na itakuwa makosa kuwaondoa just because unataka ku-balance.
Kuna utani Wapare ni bahili - wouldn't you trust them with your money?
Kuna utani Wakurya wanapenda uaskari - wengi watakuwa askari?
Ndugu zangu washomile - wouldn't be surprised to find some professors there!
This diversity can be of great use for us. We just have to put the right ones in place and then challenge them to deliver, which is the bottom line. Siyo ku-balance ...