Ndugu wana JF kuna kaemail kalikua forwarded kwangu ,nilipokasoma nilipatwa na mshtuko lakini inshallah nguvu zangu zimenirudia leo na nachukua fursa hii kukawakilisha kwenu (in my own version) but i hope it will still be enjoyable to read........ enjoy!
Hii ni habari halisi na ya uhakika kutoka ndani ya BOT. Je unawajua walioajiriwa kusimamia uchumi wa nchi yetu na kutuletea mafanikio? Pokea taarifa ya wateule hawa.
Nakutajia kwanza wachache ili wewe na watanzania wenzetu watafakari kama kweli ndege yetu itaweza kupaa kama bwana Lowasa alivyosema, au tutabaki ombaomba kama Balali anavyodai!!!. Ama tunageuzwa kuwa wadanganyika!!!
Ndani ya Mtungi wa BOT walioqualify kuajiriwa kwa sifa na vigezo vinavyotambulika na BOT ni pamoja na hawa wafuatao:-
Pamella Lowassa, Filbert Frederick Sumaye, Zalia Kawawa, Harieth Lumbanga,Salama Ally Mwinyi, Rachael Muganda, Sylvia Omari Mahita, Justina James Mungai, Kenneth John Nchimbi, Blassia Blassius William Mkapa, Violeth Phillemon Luhanjo,Liku Irene Katte Kamba, Thomas Mongella,Jabir Abdallah Kigoda etc. Hii ndio success team, hapa nani atamuwajibisha Dalali alas Balali?
Je KAPUKU MWENDE(a.k.a KAYUMBA) ATAAJIRIWA KWELI HAPO?
Hawa ni wale wenye uhusiano wa moja kwa moja na wazito wa nchi, wapo wengine ambao ni ndugu wa karibu au kabila moja na waheshimiwa. Ni vigumu kuamini kuwa hii ni bahati mbaya(mere coincidence).
Wana JF, ni juu ya watanzania kuamua kuendelea na viongozi wabovu na wenye ubinafsi au kuwaambia ukweli hata kama utawauma na kwa vile wao ndio miungu basi watatoa adhabu za kukufukuza katika bustani ya Eden.
Rhuksa kupayuka utakavyoona inafaa, na kama kuna cha kuongeza na kiko ndani ya uwezo wangu, nitakuongezea.