INAWEZA KUWA NI KUTELEZA, lakini Ndio maana niliwahi kusema kwamba JF ni kiboko na hili la kutojuana (isipokua wachache) ni jambo jema sana, linatusaidia, kwamba tunaweza kuwa na watu kutoka popote, BoT, Buzwagi, Bulyanhulu, Polisi, Usalama, jeshini, waandishi, wakulima, wanakijiji, wanasiasa, matapeli, wachungaji, mashehe, warembo, na sisi akina ........... TUENDELEE KUENZI HALI HIYO BILA KUVURUGANA KWA MASLAHI YA TAIFA NA VIZAZI VYETU.. SOTE TUNA AKILI TIMAMU. JF KEEP IT UP.
Ama kuhusu uwezo wa elimu wa baadhi ya watoto hao, nina maoni tofauti kwamba; Kwanza kabisa ukiondoa wachache, wengi wa watoto hao kweli wana elimu nzuri na sababu kwa wengi zinafahamika ni za kimazingira (rejea mfano wa Kayumba) lakini pia ni wangapi wenye uwezo kama huo pia lakini wako mitaani wanazurura kama hawataajiriwa katika sekta binafsi baadhi ambazo hazina hata UHAKIKA WA MAISHA YAO YA BAADAE? Kwa ufupi taasisi nyeti za umma kama BoT na TRA zingekua zinapokea watoto wa masikini ambao wangesaidiwa kwa makusudi ili waweze kuinua familia zao ambazo ni duni na zinamtegemea msomi mmoja ambaye hawezi kuinuka kwa kuwa na kundi kubwa la watu wanaomtegemea. NI MAONI YANGU, ambayo naamini wengi watapingana nayo na wapo watakaoelewa. Mimi kihistoria, NIMEVAA VIATU SEKONDARI TENA PEA MOJA KWA MIAKA MITATU ikipasuka INASHONWA NA KUWEKWA VIRAKA, Chai ya asubuhi ilikua anasa (Day school), nilikua NADOWEA kwa jamaa, wakati mwingine nasubiri chakula cha mchana shuleni (wakati ule bure) na ukishakula ndio wakati mwingine hadi kesho tena, huku mwendo wa kutoka nyumbani hadi shule ni masaa matatu.... HAYA JAMANI INAUMA SAAAAANA