Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Nakubali Lakini Isnt It True That Mwalimu Also Didin't Want Anyone One From The Mentioned Tribes To Hold The Highest Power Like Presidency?licha Ya Kwamba Alikuwa Na Nia Nzuri Ili Kuepuka Matabaka Kwasababu Yeye Alikuwa Ni Muumini Wa Ujamaa,je Kuna Ubaguzi Ambao Ni Justified?i Am Just Curious!
 

Mushi

Hii wewe umeipata wapi kuwa Mwalimu hukutaka wachaga washike nafasi za juu?
 
Jibu ni kuwasomesha Watoto wako leo. Wewe Treni ilikuacha zamani.
Well done Mkjj.
 
Kama ni kweli inatisha tuombe heri na Mola asimame kati yetu.
 


Hii ilisha postiwa hapa http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=6655
 

Jamani muwe mnasoma kwanza threads kabla ya kupost, hii post imerudiwa mara nyingi hapa mahali.
 
MROKI ni junior member so sio makosa yake ila kwa kumsaidia bora ifutwe
 
isifutwe iachwe tu..tusikatishe tamaa junior members....

mpoki hii nchi imeshaingia kwenye utawala wa kifalme if your dad is not or was not WHO IS WHO in tanzania circles bora tu utafutage kazi nyingine..watoto wetu watakuwa WORKING CLASS TU..ruling CLASS tayari ipo ..si unaona wameshawaazishia watoto hadi kwenye siasa...
 
Pamoja na kwamba ilishatoka hapa JF, jambo la kujivunia ni kwamba hata email zina circulate kwa watu wengi na hivyo inaonyesha idadi kubwa ya wasio na access na JF pia hupata habari kupitia njia nyingine.

This is just Feedback to JF
 
Pamoja na kwamba ilishatoka hapa JF, jambo la kujivunia ni kwamba hata email zina circulate kwa watu wengi na hivyo inaonyesha idadi kubwa ya wasio na access na JF pia hupata habari kupitia njia nyingine.

This is just Feedback to JF
Technical 'Know Who' hiyo. Inasikitisha sana.
 
jamani hawa tuwaweke kwenye maombi tu na vizazivyetu vije kuungana uko bila maoombi ya mwenyezi mungu mtaishia vumbi la chaki
mbarikiwe watoa mada
 
Naomba Tuifunge Mada Hii Leo Hii Jumapili Saa Moja Usiku,,imeashaandikwa Natumaini Wahusika Wamesoma Na
Habari Nyepesinyepesi Waungwana Wengine Wameamua
Kuanza Pale Open Wasijeaibika
Kwaherini
 
Mushi

Hii wewe umeipata wapi kuwa Mwalimu hukutaka wachaga washike nafasi za juu?

"PLEASE DONT PUT WORDS IN MY MOUTH"SIKUTAJA SPECIFICALLY WACHAGGA,WHAT I MEANT NI MWALIMU ALIOGOPA KWAMBA IF ANY OF THE MENTIONED BIG TRIBES HAPPEN TO ACQUIRE THE COUNTRY'S LEADERSHIP THEN KUNA POSSIBILTY YA KWA NA MATABAKA NA KUYASAHAU MAKABILA MADOGO,HIYO IKO WAZI KAMA HUJUI THEN I AM SORRY!NIA YAKE MAYBE ILIKUWA NI NZURI KWASABABU MWALIMU ALIPIGANIA UMOJA WA KITAIFA KULIKO KWA KILA HALI HILO LIKO WAZI.SO BILA KUJARIBU KUYUMBISHA MAANA HALISI YA POINTI YANGU KAMA UNAVYOTAKA KUJARIBU,BADO SWALI LINAJIRUDIA"IS IT JUSTIFIED?
 


Mwanakijiji umechemsha kwa kunukuu Nyerere. Hotuba za Nyerere ni lazima zichambuliwe kwa wakati. Miaka ya sitini nchi nyingi za kiafrika zilikuwa bado kwenye honey moon ya uhuru. Na uhuru huu ulipiganiwa kwa kuyaunganisha makabila yote.

Matatizo ya ukabila yalijifisha. Chukua mfano wa Kenya, Jomo Kenyatta na Odinga hawakuona tofauti ya ukabila wakati wa kupigania uhuru. Lakini miaka ilivyozidi kwenda tofauti zilionekana.

Miaka ilivyozidi kwenda Nyerere aliona matatizo ya ukabila na ndio sababu ya kuanzisha sera zenye gharama kuondoa ukabila. Tunapata uhuru, tulikuwa na majimbo tisa lakini wakati anaondoka madarakani tulikuwa na mikoa 20 Tanzania bara na ambayo mgawanyo wake umefuata ukabila kwa namna fulani. Tanganyika ina makabila zaidi ya 120 na wakati anaachia ngazi kulikuwa na wilaya 121. Hivyo kwa wastani kila kabila lilikuwa na wilaya yake.

Elimu ya sekondari ilimfanya mwanafunzi kutoka Mtwara kwenda Mwanza. Gharama hizo zilikuwa za nini kama ukabila ulikuwa haupo.

Na kwanini nafasi za kisiasa za ngazi za juu zinachukuliwa na watu kutoka makabila madogo madogo na sio makabila makubwa au yaliosoma?

Vijana wengi waliopata kazi TRA, BOT nk wamemaliza shule miaka ya1990. Na ikitokea kuwa idadi ya watu wa mikoa fulani ni wengi ni lazima kuna ulakini na hotuba zilizotolewa miaka 39 iliyopita zisitumike ku-halalisha uwiano huo.

Katika miaka ya 1990 Nyerere alisema Mkiona vinaelea, vimeundwa.
 

Mushi:

Kama mwalimu alipigania umoja wa kitaifa kwa kila hali ina maana kulikuwa na mgawanyiko fulani wa kikabila, kidini au kimajimbo. Huwezi kufanya jitihada za kupigania kitu ambacho hakipo. Huwezi kudai uhuru kama uhuru unao tayari. Umoja unatafutwa na wale wasio na umoja.

Katika ngazi za juu ilikuwa tabu kuwapata watu wa makabila makubwa. Mpare ana nafasi nzuri ya kuwa waziri kuliko mchagga pamoja na ukweli kuwa mchagga alianza kusoma mapema sana kuliko mpare.

Hakuna Justification yoyote zaidi ya fear.
 

Kuna ukweli usio na mawaa kuhusu mgawanyo wa wilaya kwa makabila, sijajua kama hayati Mwalimu Nyerere (RIP) alifanya kwa makusudi ama ilitoke bahati mbaya katika kuuzika ukabila ama kuuendeleza. Mfano,mkoani Tanga:
Muheza-Wabondei
Lushoto-Wasambaa
Korogwe-Wasambaa/Wabondei
Pangani-Wadigo
Handeni-Wazigua
Kilindi-Wazigua/wanguu
Mkinga-Wasegeju

Ukija mkoani Iringa hali ni hiyo hiyo:
Njombe-Wabena
Ludewa-Wapangwa
Mufindi-Wahehe
Kilolo-Wadzungwa
Iringa vijijini-Wahehe
Makete-Wakinga/Wawanji

Mkoani Mbeya hali kadhalika hali inashabihiana na mikoa mingine
Mbeya Mjini/Vijijini-Wasafwa/Wamalila
Rungwe/Kyela-Wanyakyusa
Ileje-Wandali
Mbozi-Wanyiha
Chunya-Wabungu
Mbarali-Wasangu

Na mkoani Pwani je?
Bagamoyo-Wazaramo
Rufiji-Wandengereko
Kisarawe-Wangindo?
Kibaha-Wazaramo?


Sasa ilikuwaje kukawa na mgawanyiko wa namna hii?
Na hii ni "Coincidence" pia?


Tunaomba ufafanuzi kwa mwenye ufahamu
 

..ufahamu mdogo nilionao ni kuwa hawa walikuwa na himaya zao na haikuwa rahisi kuchanganyika kutokana na tofauti ndogondogo walizokuwa nazo.mfano,lugha na baadhi ya mila na desturi!

..hivyo ilikuwa convinient kwao kukaa makundi na kujitwalia ardhi au maeneo ambayo leo hii ndio hayo!

..kumbuka kuwa hata baadhi yao walipigana kugombea ardhi na kuporana mifugo!sasa,kimsingi wasingeweza kukaa pamoja au kuchanganyika kutokana na hayo!

..ni historia!kama ambavyo wamasai walivyoamia northern tanganyika na kuwaswaga wa-iraqw[wa-mbulu]hivyo kukuta sehemu fulani wamejaa wao nyingine wa-iraqw!
 

Tunashukuru kwa ufafanuzi mkuu.
Tuendelee kuelimishana!
 
DUH!AMA KWELI MWANA WA MARYAM UNA PONITI!KUNA WATU WANA UPEO WA HALI YA JUU HUMU NDANI A FORUM KWAKWELI!
 
SI NDIO HAPO SASA FEAR ILIPO"JUSTIFY" DISCRIMINATION?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…