nimekuwa Nikitembelea Jf Kwa Muda Na Nimekuwa Nikijifunza Mambo Mengi Kupitia Tasnia Hii.
Ingawa Sijawahi Kutoa Maoni Yoyote Wala Kujiandikisha Lakini Leo Nimeona Nitoe Maoni Yangu Japo Kwa Uchache.
Hoja Ya Samvulachole Ingawa Imeonekana Kupingwa Na Watu Wengi, Kitu Ambacho Hata Mwanzilishi Wa Hoja Alikuwa Amekihofia.
Kwa Uzoefu Wangu Katika Ajira Za Serikalini, Idara Zake Na Mashirika Ya Umma Kwakweli Ukabila Umezidi.
Pamoja Na Nukuu Nzuri Za Mzee Mwanakijiji, Anasahau Kuwa Hayo Ni Mambo Ambayo Jkn Aliyazungumza Miaka Zaidi Ya 30 Iliyopita. Sasahivi Ukweli Ni Kuwa Makabila Mengi Yanatambua Umuhimu Wa Elimu. Hizo Shule Zinazofanya Vizuri Huko Moshi Na Mbeya,chukua Mfano Shule Ya St.francis Ya Mbeya Na Agape Ya Moshi, Haimaanishi Kuwa Wanaosoma Kwenye Hizo Shule Ni Wachaga Na Wanyaki Peke Yao.huko Wapo Makabila Mchanganyiko.
Miaka Ya 90 Kurudi Nyuma Shule Kama Moshi Technical, Old Moshi, Ilboru, Kibaha, Tabora Boys&girls,nganza,kilakala,mzumbe,ifunda Na Nyingine Nyingi Zilikuwa Zinapokea Wanafunzi Wenye Viwango Vizuri Kutoka Kona Zote Za Tanzania Kwahiyo Hawakuwa Wachaga,wahaya Na Wanyaki Pekee Wanaosoma.
Mzee Mwanakijiji Anazungumzia Enzi Za Giza, Wakati Nchi Ndipo Inapata Uhuru.
Nimalizie Kwa Kusema Hiyo Historia Anayoitukuza Mzee Mwanakijiji Inatumiwa Na Watu Wengi Sana Serikalini Kupeana Kazi Kwa Misingi Ya Ukabila Na Ndiyo Sababu Hata Wachangiaji Wengi Hapa Wameonekana Kuungana Na Mzee Mwnkjj Huenda Na Wao Wamewahi Au Wanaendelea Kufaidika Na Upendeleo Huo.
Wakati Fulani Nikiwa Katika Chuo Fulani Kikubwa Na Maarufu Hapa Dsm Niliwahi
Kufanya Tathmini Nikagundua Kuwa Watanzania Wa Kila Kabila Wanachangamkia Elimu Sio Mchezo.kila Kabila Sasahivi Lina Wasomi Waliobobea.
Tukikubali Huo Udhaifu Ndipo Tutaweza Kufaidi Matunda Ya Uhuru Wetu Kwa Usawa Na Haki Na Mapambano Dhidi Ya Mafisadi Wanaotumia Rasilimali Zetu Kwa Manufaa Binfsi Yatakuwa Na Tija.