Mzee Mwanakijiji,
Mzee wangu unazungusha issue kwa kuuliza maswala ambayo majibu yake yapo wazi.
Najitahidi kweli kuona haya majibu wazi.
Je, haya makabila uliyoyataja ni majority ktk population ya Tanzania?.. hapana!
Very good! nimesubiri mmoja wenu alete hii point kwa sababu nimeshasema ukabila mnaozungumzia ni wa "idadi ya watu wa kabila moja mahali pa kazi" na wala si hisia ya kujiona bora, kustahili zaidi, na kukandamiza watu wa makabila mengine. Ukabila huu mnaouona nyinyi unatokana na kulinganisha na idadi ya watu wa makabila mengine? Je kuna wasomi wengi wa Kisukuma na Kinyamwezi (makabila makubwa zaidi Tanzania?) Hebu tuangalia idadi ya makabila makubwa zaidi Tanzania (unaweza kupata info hapa
www.ethnologue.com) Makisio ya 2000
- Wahehe est. 750,000
- Wandengereko est. 110,000
- Wazaramo est. 656,000
- Wadigo Est. 88,000 (Tanzania, 300,000 Kenya)
- Wairaqw Est. 462,000
- Waluguru Est. 692,000
- Wazanaki est. 62,000
- Wakwere est. 98000
- Wasukuma est. 3,200,000 (kabila kubwa zaidi)
- Nyamwezi est. 2,000,000 (kabila la pili kwa ukubwa likifunganga na Wachagga) ni ndugu za wasukuma
- Wagogo Est. 1,300,000 (Wanawazidi Wanyakyusa kidogo kwa wingi)
- Wamakonde est. 1,100,000
- Wapare est. 1,000,000
Haya makabila hayo matatu
- Haya est. 1,200,000 (1991)
- Chagga est 2,000,000
- Nyakyusa est. 1,000,000
A. Sasa kwa kufuata logic ya wingi peke yake Wasukuma na Wanyamwezi ndio wangekuwa wengi zaidi katika kila kona ya nchi na katika kila ofisi. Hali siyo hivyo kwanini, wakati tumeambiwa kuwa kuanzia miaka ya 70 watu wote wamepewa nafasi sawa ya kusoma? Kwanini wasukuma hawajapata nafasi nyingi za ajira kuliko watu wengi wa pwani wakati nafasi za kusoma zipo wazi kwa wote? Hivi hawa wote wamebaguliwa na kunyimwa nafasi za kazi licha ya kuwa na elimu sawa na watu wa makabila hayo matatu? Nitafurahi kuona ushahidi wa hilo.
B. Wahaya ni mara mbili ya Wazaramo na ni mara 12 ya Wakwere. Wachagga ni mara 10 zaidi ya Wadigo na Wandengereko combined! Wanyakyusa ni mara tano ya Wadigo na Wandengereko combined! Makabila hayo matatu combined ni zaidi ya makabila hayo nane ya kwanza! Sasa mtu aniambie iweje makabila madogo moja moja yawe na watu wengi maofisini kupita makabila haya matatu moja moja? Kama kabila lako lina watu 68,000 na wote wasomee uhasibu, na wote waajiriwe na serikali bado kuna watu zaidi ya milioni moja upande wa uchagga ambao nao wanataka nafasi hizo!!!! Hivyo hata kama nafasi zote za ajira za serikali zipewe watu wa makabila hayo nane, still makabila ya Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa wanao watu wengi zaidi kuwazidi waajiriwa hao wapya!!! Unless makabila madogo madogo wazaane kwa wingi na kufikia idadi ya makabila hayo matatu, na wakati huo huo watu wa makabila hayo matatu waache kuzaana wakiwasubiri hao ndugu zao... there will never be parity!!!! Huo ndio ukabila mnaouzungumzia!!
C. Kama kuna watu katika Tanzania ambao wanaweza kudai ukabila na kuonewa ni Wasukuma, Wanyamwezi, Wagogo, Wamakonde na Wapare ambao wote wana idadi zaidi ya milioni moja? Ni kwanini makabila hayo matano hayajaingia katika nafasi nyingi? Je hii yote ni njama za Wanyakyusa, Wahaya, na Wachagga?
Kisha nimekwambia tazama matokeo ya shule na vyuo vyetu toka 1970's utakuta watu wa makabila yote wamesoma je kuna ushahidi zaidi ya huo ama unataka nitafute matokeo ndipo utaweza kuamini hali wewe mwenyewe ni mfamo mmojawapo.
Ndio umeniambia, ila ushahidi hukutoa na mimi si mmojawapo!
Watu kama wewe na mimi na Dau Mikael na wengine wote ndio tunaowazungumzia.
Sifikiri mimi niko kundi hilo!
Hesabu ya Wachagga kupungua ama kuongezeka ni wazi zimepungua kwa sababu Tanzania tuna idadi ndogo sana ya shule na nafasi hazitolewi kwa sababu ya kuhudhulia shule!..
Najaribu kuuona huu "uwazi" wa wachagga kupungua. Je wamepungua kwenye population kitu kilichosababisha wao kupungua mashuleni na vyuoni.
Kisha mshikaji kuna studies zimefanywa nyingi tu zimeonyesha wazi kuwa wazee maskini wasiokuwa na elimu huwahimiza watoto wao shule kuliko wale wenye uwezo na mara nyingi watoto toka familia zenye uwezo wanapuuza shule ispokuwa kinachowashinda maskini ni uwezo wa kulipia shule hizo. hizi ni studies za in general.
Please cite one study for me, iliyofanywa Tanzania..! general studies can be applied anywhere hata msituni.
Kikubwa kuliko yote ni pale unapokimbia swala la TRA kwa visingizio vya kuzungusha issue. Tumesema kwa tafsiri yako ya mwanzo hakuna UKABILA lakini unapo question Ukabila kwa maswali unayotoa basi hakuna kitu UKABILA duniani tukifuata maswali hayohayo!... Wazungu wa South wanakila haki ya ku-claim kama unavyosema wewe.
Wala sijakimbia, huwezi kuchagua kitengo kimoja, mipaka miwili na ofisi tatu kujenga maoni ya jumla! Kwa watoto wa chekechea inaweza kuwafanya waduae, ila kwa watu wazima tunaoweza kusoma katikati ya mistari tunasema:
- Tupeni vitengo vyote vya TRA na viongozi wake
- Tupeni wakuu wa vituo vyote vya mipakani na ofisi zote za mikoa za TRA
- Tuonesheni kuwa wote walioajiriwa hawana elimu (sizungumzii walioteuliwa). Nionesheni Mhasibu TRA anayefanya kazi ambaye hajasomea uhasibu n.k
Hatubishi alimradi tunabisha tu, na haturukii treni hili la ukabila kwa vile watu fulani wanaimba nyimbo mzuri. Naomba mnishawishi kwa hoja zenye nguvu badala ya maneno ya mvuto! Narudia tena hakuna ukabila wa kibaguzi Tanzania kama jumuiya nzima, isipokuwa ule uliomo ndani ya wale wanaoutafuta. You can't conclude and then find the evidence to support your conclusions! Na pia mimi si mtoto mdogo ambaye sielewi kuwa kuna watu mmoja mmoja ambao wanasukumwa na ukabila na watu hawa hawako kwenye makabila hayo matatu tu, wapo na wa makabila mengine kama tulivyoshuhudia mumu humu!