Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

@Mwendapole

Its undeniable fact that we do have tribalism in Tanzania just like other African countries even though publicly we are in denial but deep down we know it is alive and many people are missing out due to this phenomenon that i call NATIONAL PSYCHOSIS which was and is still eating ating deep into the fabric of Tanzanian community.

DrWho please amuse me... show me the evidence of this "Undeniable fact" kwamba kuna ukabila Tanzania? Je ukikuta Wasukuma wengi kwenye kitengo fulani huko Mwanza tutaweza kudai ni ukabila? Nionesheni huo ushahidi wa ukabila ambao watu wanao!

Mwendapole if you look up the meaning of the word psychosis, it is explained as a severe mental derangement that results in the impairment or loss of contact with reality.In other words WE ARE IN DENIAL and if that definition is anything to go by, then we certainly have an arduous task to execute.

I'll argue the other way, may be the people who scream "tribalism" are the one who are in denial, they refuse to see anything else but tribalism, whenever they see a name of a Mnyakyusa, Mhaya, or Mchagga their antennas will pick tribalism vibes whenever they see a group of Wachagga, Wahaya, and Wanyakyusa!

iN THEORY that is the spirit we want in Tanzania- unity in diversity but in PRACTICAL this is impossible since the same people who advocate UNITY are the tribalists rulling class and we dare not talk about it

oh my! now we have "tribalists rulling class"... what a natural progression of ideas..! Keep going.. once you break a principle, that principle will find a way of breaking you! so keep breaking it!

.. We have often complained about the issue of square pegs in round holes. Tribalism can partly be blamed for this. For example there is always the tendency to feel that once the Managing Director is a NYAKYUSA (for example), he must give me the job even though it is obvious Mohammed Hassan from PEMBA is more qualified than I am. This phenomenon does not auger well for the development of our nation.

The sooner we admit we have a problem then we might as well talk about how we can solve it and not living in DENIAL


Could this Managing Director be a Mzigua and his hiring of another Mzigua considered to be ukabila? or this pseudo-tribalism can only be seen when Wanyakyusa, Wahaya and Wachagga practice it?
 
Mzee Mwankijiji,
Mzee wangu unazungusha issue kwa kuuliza maswala ambayo majibu yake yapo wazi.
Unauliza lini wazee hawa wasomi waliacha kusomesha watoto wao!... Mtazamo gani huu ndugu yangu?
I mean ni sawa na kusema kwamba hakuna waafrika weusi Marekani wanaoweza kushika nafasi za kazi kwa sababu wazungu hawajapungua kwenda mashuleni!...what ana excuse.... Swali ni je, kuna weusi ambao anaweza kushika madaraka?..Je, haya makabila uliyoyataja ni majority ktk population ya Tanzania?.. hapana!
Kisha nimekwambia tazama matokeo ya shule na vyuo vyetu toka 1970's utakuta watu wa makabila yote wamesoma je kuna ushahidi zaidi ya huo ama unataka nitafute matokeo ndipo utaweza kuamini hali wewe mwenyewe ni mfamo mmojawapo. Watu kama wewe na mimi na Dau Mikael na wengine wote ndio tunaowazungumzia.
Hesabu ya Wachagga kupungua ama kuongezeka ni wazi zimepungua kwa sababu Tanzania tuna idadi ndogo sana ya shule na nafasi hazitolewi kwa sababu ya kuhudhulia shule!..
Kisha mshikaji kuna studies zimefanywa nyingi tu zimeonyesha wazi kuwa wazee maskini wasiokuwa na elimu huwahimiza watoto wao shule kuliko wale wenye uwezo na mara nyingi watoto toka familia zenye uwezo wanapuuza shule ispokuwa kinachowashinda maskini ni uwezo wa kulipia shule hizo. hizi ni studies za in general.
Kikubwa kuliko yote ni pale unapokimbia swala la TRA kwa visingizio vya kuzungusha issue. Tumesema kwa tafsiri yako ya mwanzo hakuna UKABILA lakini unapo question Ukabila kwa maswali unayotoa basi hakuna kitu UKABILA duniani tukifuata maswali hayohayo!... Wazungu wa South wanakila haki ya ku-claim kama unavyosema wewe.
 
@ Dua:
hivyo hivyo barabara kila uchwao zinajengwa kwa Basil Mramba na Msuya area; huu sio ukabila bali ni historia. GIVE ME A BREAK!

a.hizo barabara za kwa kina msuya na mramba zimejengwa lini na zina urefu wa km ngapi?

b.barabara inayopita jimbo la msuya ni ya mkomazi-same-mwanga-moshi. jimbo la msuya ni kipande kidogo sana cha barabara hiyo.

c.barabara ya mkomazi-moshi imepita majimbo mengi mbona yanatajwa ya msuya na mramba tu? barabara ya kwenda tanga na nyingine lushoto milimani ilijengwa kabla ya barabara ya mkomazi-moshi-arusha, mbona hamuwalalamikii kina kagonji, na shelukindo?

d.barabara ya dar-moro-dodoma ilikarabatiwa kabla ya barabara ya mkomazi-same-mwanga-moshi. ukabila uko wapi? barabara za mwanza mjini,dodoma mjini,jijini dsm, zimekarabatiwa kabla ya barabara za moshi mjini. ukabila uko wapi?

d.mara nyingi wafadhili huchagua miradi yao, na kiwango gani watachangia.rejea mazungumzo ya Raisi Kikwete Davos. kwa msingi huo barabara mbalimbali zina wafadhili tofauti. nakuhakikishia kwamba barabara za maeneo mengine zilitengewa fedha as much as barabara za kaskazini.

e.barabara ya dodoma-manyoni-mwanza fedha zake zilipotea kwa uzembe wa Kiula[mtu wa manyoni] na Dr.Mlingwa[mtu wa mwanza]. gharama za ujenzi wa barabara ya dodoma-manyoni-mwanza ni kubwa kuliko barabara za kaskazini, pamoja na hayo ilitafutiwa wafadhili na ilitengewa fedha. hilo nalo utamlaumu msuya na mramba?

f. g.jimbo la chalinze limepata mradi mkubwa wa maji. kuna majimbo mengi tanzania yana uhaba wa maji kuliko jimbo la chalinze. je tuseme Kikwete naye ana ukabila?

g.mawaziri wa ujenzi samwel sitta,guntram itatiro,nalaila kiula,anna abdallah, wote hao wanapendelea kilimanjaro? hao ndiyo wahusika wakuu wa miradi ya ujenzi wa barabara. kwanini tuwalaumu msuya na mramba kwa majukumu ya mawaziri wengine?

kuna baadhi yetu wanachuki kali sana ya ukabila. Chuki hiyo inawafanya washindwe kuchambua mambo kwa misingi ya hoja, na tafakuri.
 
DrWho,
Umeshataja tatizo: ukabila. I am interested in the solution. Kwa maoni yako how do you think we can fight this demon called tribalism? Or is it too late?
 
Jafar asante kwa kutukumbusha, lakini kumbuka kwamba educational quarter system was very very unfair to some tribes. For example, how do you explain the sending of hundreds of chagga students to Iringa secondary schools and almost none from Iringa to moshi schools in the 1960s and 70s?
 
Jokakuu,
Nitakujibu hoja yako kirahisi sana...
Swala hapa ni TRA sio barabara kwa sababu hakuna barabara ya kabila fulani ama kutumika na kabila fulani. barabara ni infrastructure ya nchi nzima. Ujenzi wake ndio unaotenganisha viongozi wazuri na viongozi wabaya!
Sisi wote binadamu na kila mmoja wetu kaumbwa na akili isipokuwa kila mmoja wetu huzitumia akili hizo tofauti. Ukabila in general ni kitu kikubwa sana na huwezi kupima Ukabila kwa mifano ambayo kila mtu ana uamuzi wake ktk maslahi ya taifa.
Ukabila ni UBAGUZI, kutokuwa mbaguzi ama kuwakandamiza watu wako haiwezi kuwa na tafsiri sawa. Wapo viongozi wanao/takao watesa na kuwaua ndugu na jamaa zake, sijui kama utasema ni wakabila kwa sababu wame target ukoo ama kabila moja. Pia KUPENDELEA (favour) watu fulani bado haikamilishi tafsiri ya Ukabila ikiwa hutachulia kigezo cha kabila hilo kuwa bora na lenye kustahili kuliko makabila mengine.
JK kujenga barabara ya Chalinze ni moja ya kazi zake kama mbunge wa Chalinze, na mpango wa ujenzi wa barabara hiyo ulikuwepo muswada toka zamani akiwa bado mbunge, pia umuhimu wa barabara hiyo umejadiliwa bungeni na kupitishwa.
Mwisho, barabara hiyo haikujengwa na manufaa ya wakwere peke yake!

Mlowezi,
nakuomba unipe ukweli wa madai yako, Kwa sababu ni marafiki zangu wanyakyusa wamesoma Moshi..
 
Mkandara,
I was just responding to DUAallegations that there were tribal consideration when allocating funds to road projects. I hope DUA would read your response carefully.

@ Mkandara:
JK kujenga barabara ya Chalinze ni moja ya kazi zake kama mbunge wa Chalinze, na mpango wa ujenzi wa barabara hiyo ulikuwepo muswada toka zamani akiwa bado mbunge, pia umuhimu wa barabara hiyo umejadiliwa bungeni na kupitishwa.
Mwisho, barabara hiyo haikujengwa na manufaa ya wakwere peke yake!

Maelezo yako nayafahamu na nakubaliana nayo. Ninachojaribu kujiuliza ni kwanini Mramba na Msuya walalamikiwe kwa ujenzi wa barabara zinazopita majimboni kwao, wakati Kikwete,Kagonji,Shelukindo,Dialo....hawalalamikiwi? Swali hilo naomba umuulize DUA

Jinsi mjadala huu unavyosonga mbele, ndivyo ninavyozidi kuamini kwamba suala hapa siyo TRA, bali ni CHUKI dhidi ya WACHAGA, na makabila mengine yanayoonekana kuwa yamesonga mbele KIELIMU.

Mzee Mlowezi,
kuhusu quota system, naweza kusema atleast kulikuwa na juhudi za kutafutia ufumbuzi this glaring disparity. kwamba haikufanikiwa hilo ni suala lingine.

ninayo mifano ya vijana waliohama toka mikoa yenye pass mark kubwa na kwenda kurudia mtihani wa darasa la saba mikoa yenye pass mark ndogo na baadaye kuendelea na sekondari.

ninayo mifano ya vijana waliobadili majina ili kupata nafasi ya kuendelea na sekondari. ujanja huo ulifanywa na watu wa kilimanjaro na kagera ili kukwepa quota system.

quota system haikufanikiwa kwasabau ilizingatia zaidi pass-mark na siyo kubadilisha mazingira ya SHULE na ELIMU katika mikoa husika. serikali iliteremsha pass-mark lakini ikashindwa kupeleka waalimu ktk mikoa iliyokuwa nyuma kielimu. sote tunatambua kwamba ni vigumu kuwashawishi wataalamu wetu[waalimu,madaktari,bwana shamba] kwenda kufanya kazi ktk mikoa fulani.

nilibahatika kusoma boarding school, na katika shule yangu kila mwaka kulikuwa na intake ambayo ilikuwa na majority ya wanafunzi toka mkoa tofauti. nimeshuhudia intake zilizokuwa na majority ya wanafunzi toka Kigoma, Mwanza, Kilimanjaro-Arusha.
 
Jokakuu

Umedandia gari hujui linakokwenda. Naomba usome issue ambazo ni raised kutoka mwanzo, swala la barabara za kaskazini kupewa 17 billion na za Mtwara na Lindi kupewa 1 billion lilijadiliwa bungeni na wako waliosema kama wewe kwamba wafadhili ndio wanachagua wapi waweke pesa ambalo vilevile limejadiliwa pitia kurasa za mwanzo utapata majibu. usikurupuke kufikiri kila mtu hapa anawachukia wachaga au wambulu au wamang'ati. Siwezi kurudia majibu yapo kwenye hii thread huko mwanzo ndio nikasema sasa kama huu si ukabila ni nini?
 
Mzee Mwanakijiji,
Mzee wangu unazungusha issue kwa kuuliza maswala ambayo majibu yake yapo wazi.

Najitahidi kweli kuona haya majibu wazi.


Je, haya makabila uliyoyataja ni majority ktk population ya Tanzania?.. hapana!

Very good! nimesubiri mmoja wenu alete hii point kwa sababu nimeshasema ukabila mnaozungumzia ni wa "idadi ya watu wa kabila moja mahali pa kazi" na wala si hisia ya kujiona bora, kustahili zaidi, na kukandamiza watu wa makabila mengine. Ukabila huu mnaouona nyinyi unatokana na kulinganisha na idadi ya watu wa makabila mengine? Je kuna wasomi wengi wa Kisukuma na Kinyamwezi (makabila makubwa zaidi Tanzania?) Hebu tuangalia idadi ya makabila makubwa zaidi Tanzania (unaweza kupata info hapa www.ethnologue.com) Makisio ya 2000

- Wahehe est. 750,000
- Wandengereko est. 110,000
- Wazaramo est. 656,000
- Wadigo Est. 88,000 (Tanzania, 300,000 Kenya)
- Wairaqw Est. 462,000
- Waluguru Est. 692,000
- Wazanaki est. 62,000
- Wakwere est. 98000

- Wasukuma est. 3,200,000 (kabila kubwa zaidi)
- Nyamwezi est. 2,000,000 (kabila la pili kwa ukubwa likifunganga na Wachagga) ni ndugu za wasukuma
- Wagogo Est. 1,300,000 (Wanawazidi Wanyakyusa kidogo kwa wingi)
- Wamakonde est. 1,100,000
- Wapare est. 1,000,000


Haya makabila hayo matatu

- Haya est. 1,200,000 (1991)
- Chagga est 2,000,000
- Nyakyusa est. 1,000,000

A. Sasa kwa kufuata logic ya wingi peke yake Wasukuma na Wanyamwezi ndio wangekuwa wengi zaidi katika kila kona ya nchi na katika kila ofisi. Hali siyo hivyo kwanini, wakati tumeambiwa kuwa kuanzia miaka ya 70 watu wote wamepewa nafasi sawa ya kusoma? Kwanini wasukuma hawajapata nafasi nyingi za ajira kuliko watu wengi wa pwani wakati nafasi za kusoma zipo wazi kwa wote? Hivi hawa wote wamebaguliwa na kunyimwa nafasi za kazi licha ya kuwa na elimu sawa na watu wa makabila hayo matatu? Nitafurahi kuona ushahidi wa hilo.

B. Wahaya ni mara mbili ya Wazaramo na ni mara 12 ya Wakwere. Wachagga ni mara 10 zaidi ya Wadigo na Wandengereko combined! Wanyakyusa ni mara tano ya Wadigo na Wandengereko combined! Makabila hayo matatu combined ni zaidi ya makabila hayo nane ya kwanza! Sasa mtu aniambie iweje makabila madogo moja moja yawe na watu wengi maofisini kupita makabila haya matatu moja moja? Kama kabila lako lina watu 68,000 na wote wasomee uhasibu, na wote waajiriwe na serikali bado kuna watu zaidi ya milioni moja upande wa uchagga ambao nao wanataka nafasi hizo!!!! Hivyo hata kama nafasi zote za ajira za serikali zipewe watu wa makabila hayo nane, still makabila ya Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa wanao watu wengi zaidi kuwazidi waajiriwa hao wapya!!! Unless makabila madogo madogo wazaane kwa wingi na kufikia idadi ya makabila hayo matatu, na wakati huo huo watu wa makabila hayo matatu waache kuzaana wakiwasubiri hao ndugu zao... there will never be parity!!!! Huo ndio ukabila mnaouzungumzia!!

C. Kama kuna watu katika Tanzania ambao wanaweza kudai ukabila na kuonewa ni Wasukuma, Wanyamwezi, Wagogo, Wamakonde na Wapare ambao wote wana idadi zaidi ya milioni moja? Ni kwanini makabila hayo matano hayajaingia katika nafasi nyingi? Je hii yote ni njama za Wanyakyusa, Wahaya, na Wachagga?

Kisha nimekwambia tazama matokeo ya shule na vyuo vyetu toka 1970's utakuta watu wa makabila yote wamesoma je kuna ushahidi zaidi ya huo ama unataka nitafute matokeo ndipo utaweza kuamini hali wewe mwenyewe ni mfamo mmojawapo.

Ndio umeniambia, ila ushahidi hukutoa na mimi si mmojawapo!

Watu kama wewe na mimi na Dau Mikael na wengine wote ndio tunaowazungumzia.

Sifikiri mimi niko kundi hilo!

Hesabu ya Wachagga kupungua ama kuongezeka ni wazi zimepungua kwa sababu Tanzania tuna idadi ndogo sana ya shule na nafasi hazitolewi kwa sababu ya kuhudhulia shule!..

Najaribu kuuona huu "uwazi" wa wachagga kupungua. Je wamepungua kwenye population kitu kilichosababisha wao kupungua mashuleni na vyuoni.

Kisha mshikaji kuna studies zimefanywa nyingi tu zimeonyesha wazi kuwa wazee maskini wasiokuwa na elimu huwahimiza watoto wao shule kuliko wale wenye uwezo na mara nyingi watoto toka familia zenye uwezo wanapuuza shule ispokuwa kinachowashinda maskini ni uwezo wa kulipia shule hizo. hizi ni studies za in general.

Please cite one study for me, iliyofanywa Tanzania..! general studies can be applied anywhere hata msituni.

Kikubwa kuliko yote ni pale unapokimbia swala la TRA kwa visingizio vya kuzungusha issue. Tumesema kwa tafsiri yako ya mwanzo hakuna UKABILA lakini unapo question Ukabila kwa maswali unayotoa basi hakuna kitu UKABILA duniani tukifuata maswali hayohayo!... Wazungu wa South wanakila haki ya ku-claim kama unavyosema wewe.

Wala sijakimbia, huwezi kuchagua kitengo kimoja, mipaka miwili na ofisi tatu kujenga maoni ya jumla! Kwa watoto wa chekechea inaweza kuwafanya waduae, ila kwa watu wazima tunaoweza kusoma katikati ya mistari tunasema:

- Tupeni vitengo vyote vya TRA na viongozi wake
- Tupeni wakuu wa vituo vyote vya mipakani na ofisi zote za mikoa za TRA
- Tuonesheni kuwa wote walioajiriwa hawana elimu (sizungumzii walioteuliwa). Nionesheni Mhasibu TRA anayefanya kazi ambaye hajasomea uhasibu n.k

Hatubishi alimradi tunabisha tu, na haturukii treni hili la ukabila kwa vile watu fulani wanaimba nyimbo mzuri. Naomba mnishawishi kwa hoja zenye nguvu badala ya maneno ya mvuto! Narudia tena hakuna ukabila wa kibaguzi Tanzania kama jumuiya nzima, isipokuwa ule uliomo ndani ya wale wanaoutafuta. You can't conclude and then find the evidence to support your conclusions! Na pia mimi si mtoto mdogo ambaye sielewi kuwa kuna watu mmoja mmoja ambao wanasukumwa na ukabila na watu hawa hawako kwenye makabila hayo matatu tu, wapo na wa makabila mengine kama tulivyoshuhudia mumu humu!
 
"3. haya mambo yameumbwa na Mungu..Biblia inasema ‘mwenye nacho huongezewa"
Mwendapole you are really a $%^&*()!
 
Mzeee IO,

Heshima yako mkuu, please hiyo lugha nzito ndugu yangu huuu mjadala unatuelimisha wengi hapa na tunaufuatilia kwa makini na kuna data tunzichota hapo,

chonde chonde, hiyo lugha yako ni nzito mno bro na sio healthy kwa majadiliana ya wastaaarabu kama hii forum, na ninajua kuwa wewe ni bigger than hiyo lugha uliyoitumia kum-describe mwana forum mwingine just because maoni yake hayafikiii level ya acceptance by you,

Kama huwezi mjadala ndugu yangu kaa pembeni kama sisi tunaouangalia kwa pembeni lakini tunaelimika, personally I am very offended na matusi yako mwishoni mwa message yako!
 
Najitahidi kweli kuona haya majibu wazi.

Very good! nimesubiri mmoja wenu alete hii point kwa sababu nimeshasema ukabila mnaozungumzia ni wa "idadi ya watu wa kabila moja mahali pa kazi" na wala si hisia ya kujiona bora, kustahili zaidi, na kukandamiza watu wa makabila mengine. Ukabila huu mnaouona nyinyi unatokana na kulinganisha na idadi ya watu wa makabila mengine? Je kuna wasomi wengi wa Kisukuma na Kinyamwezi (makabila makubwa zaidi Tanzania?) Hebu tuangalia idadi ya makabila makubwa zaidi Tanzania (unaweza kupata info hapa www.ethnologue.com) Makisio ya 2000

- Wahehe est. 750,000
- Wandengereko est. 110,000
- Wazaramo est. 656,000
- Wadigo Est. 88,000 (Tanzania, 300,000 Kenya)
- Wairaqw Est. 462,000
- Waluguru Est. 692,000
- Wazanaki est. 62,000
- Wakwere est. 98000

- Wasukuma est. 3,200,000 (kabila kubwa zaidi)
- Nyamwezi est. 2,000,000 (kabila la pili kwa ukubwa likifunganga na Wachagga) ni ndugu za wasukuma
- Wagogo Est. 1,300,000 (Wanawazidi Wanyakyusa kidogo kwa wingi)
- Wamakonde est. 1,100,000
- Wapare est. 1,000,000


Haya makabila hayo matatu

- Haya est. 1,200,000 (1991)
- Chagga est 2,000,000
- Nyakyusa est. 1,000,000


MKJJ Bravo

Pia hebu sasa tuangalie idadi ya mashule ya sekondari nchi nzima katika kila mikoa. Nijuavyo mimi Mkoa wa Kilimanjaro ndio wenye mashule mengi zaidi kulikoko mkoa wowote Tanzania (sina exact number).

Sasa hiyo peke yake inaanisha wachagga wakiwa kwao (kwa maana ya Kilimanjaro peke yake) wana nafasi kubwa zaidi ya kusoma kuliko kabila lingine lolote. Then, weka pia idadi ya watoto wa kichagga ambao wako nje ya Kilimanjaro, huko nako pia wanapata nafasi sawa na makabila mengine. Fact inakuja kuwa wazi kuwa wachagga wamesoma kuliko makabila mengine. Wamesoma kuliko walipata nafasi nyingi zaidi za kusoma kuliko makabila mengine. Kwa nini then tukija kwenye ajira watu mnasema kuna ukabila.

Nakubaliana kabisa na hoja ya Mwanakijiji kuwa ukabila kwa maana ya uwingi wa kabila fulani katika ofisi/idara fulani huo sio ukabila. Ukiangalia fugures za makabila hapo juu utakuta (nasikitika sana sina figures za mashule) ila kama sikosei idadi ya shule zilizoko Kilimanjaro ni sawa na shule zote za Unyamwezini na Usukumani, combined...!! Idadi ya hayo makabila hayo 2 ni 5.2 milion na idadi ya wachagga ni 2mil...!!

Kuna watu humu wana fananisha na ule ubaguzi wa rangi kule South na Amerika, kama MKJJ alivyosema ule uko tafauti kabisa na Ukabila huu ambao wengi hapa wana uzungumzia. Wazungu weupe kule South wao walijiona WANA HAKI ZAIDI kwa sababu wao ni Weupe. Cv yao ilikuwa rangi ya ngozi yao sio vyeti vya shule...weusi walikuwa wanasimama kwenye mabasi kule USA ili wazungu wakae...huo ndio ubaguzi. Hii definition yenu ya kusema uwingi wa kabila fulani sehemu fulani ubaguzi..haina maana hata kidogo.

Naomba kutoa hoja.
 
Yebo Yebo.. kabisa.. wautafutie jina jingine.. lakina kuuita ukabila hilo sijakubali na ninatumaini nimeweza kuwashawishi watu wachache kubadili mtazamo wao. Na itafurahisha zaidi kama watakuja na kukiri kuwa walikuwa wamepotoka kihoja. But that will be expecting too much.
 
Cheers MKJJ

Nimeelimika sana na mjadala huu.


Kwa hizo figures hapo juu...je ni sahihi kuwa na makisio kuwa Wachagga ndio kabila kubwa zaidi Mkoani Dar es salaam..?

Maana ni ukweli ulio wazi kuwa wachagga wengi waliondoka kwao Kilimanjaro kuliko makabila mengine kwa sababu ya matatizo ya Arthi.
 
Takwimu ulizotoa ni sawa na less than 50% ya idadi ya Watanzania, Je hii inamaanisha ni makabila mengine madogo madogo. Kama ni hivyo kwa nini tusijue idadi yake kwani ni almost nusu ya nchi hatuioni.

Jina lingine la tabia hii kama Ukabila unachukiza kwa nini wanaufanya - Tuwaulize wataalamu wa lugha fasaha.
 
Yebo Yebo... unaenda kasi sana...nilikuwa nasubiri majibu ya watani zangu hapa.. halafu tuje kwenye hilo la uhamaji wa Wachagga... but you are moving in the right direction... tutaufunua ukweli kwa kutumia nguvu za hoja kuwa ukabila uko mawazoni mwa watu tu!!
 
Takwimu ulizotoa ni sawa na less than 50% ya idadi ya Watanzania, Je hii inamaanisha ni makabila mengine madogo madogo. Kama ni hivyo kwa nini tusijue idadi yake kwani ni almost nusu ya nchi hatuioni.

Jina lingine la tabia hii kama Ukabila unachukiza kwa nini wanaufanya - Tuwaulize wataalamu wa lugha fasaha.


Dua, ina maana hakuna makabila mengine yenye kufikia idadi ya milioni moja!!! Ukiondoa hayo niliyoyataja, unless niruke makabila mawili matatu... nitatafuta nipate uhakika...ila lengo langu ni kuonesha kuwa watu wa pwani kwa idadi hawawafikii makabila hayo, na pili hata makabila mengine ambayo ni mengi idadi yao haionekani sana mahali pa kazi na katika ajira, swali ni kwanini?
 
Yebo yebo,
Mbona mshikaji unataja mambo kama vile tuko Kenya au Nigeria!.. yaani kwa sababu kuna shule nyingi Kilimanjaro unasema kuna sababu ya kuwa na Wachagga wengi shuleni?... Hii unazungumzia shule zipi za primary! je hii ndio elimu inayohitajiwa kuajiriwa TRA?..sielewi kabisa kinachokusudiwa ktk mifano hii.

Yebo Yebo, unaelewa vizuri kwamba shule za secondary zinachagua watu kutokana na Kushinda mitihani na hakuna mahala popote panaposema kwamba kabila lenye watoto wengi shule za msingi wana nafasi kubwa ya kwenda sekondary kuliko kabila yenye watoto wachache!..Hizi ni hesabu za Kigagagigikoko! huko Kenya na Nigeria. Wee tupe hesabu ya wanafunzi wa vyuoni leo kwa makabila yake! Vipi jamani mbona mnapindisha mambo kwa lugha isiyokuwa na mahesabu?..

Sasa nakuombeni nyie mtuambie UKABILA ktk ajira huwa unatokea vipi? just that kisha mimi nitashika nafasi yenu kuzua hoja zisizokuwa na msingi.

Mwanakijiji,
Ikiwa shule zipo 10 zenye kuchukua idadi ya wanafunzi 1000 na kati ya wanafunzi hao asilimia 70 ni Wachagga wa kuteuliwa kutokana na mfumo wa elimu wa zamani. Kumbuka hata uzawa wa mtu ilikuwa ni shida kusajili shule Kilimanjaro ama Mwanza kama wewe sio mwenyeji wakati wa mkoloni. Mkoloni alitutenganisha kwa makabila na dini ili kuweza kututawala vizuri. Leo hii huwezi kunambia asilimia itabakia ileile ikiwa shule hizo 10 zitaanza kusajili wanafunzi toka makabila mengine hali nafasi zilizopo bado ni 1000..simple maths!
 
Mwanakijiji.

hakuna sehemu nimesema uliajiriwa TRA au kitengo cha serikali.
ila kabila lako unajua limebebwa sana na ukabila na ni moja lililozungumzwa sana kwa tabia hiyo chafu.na wewe kwa vile jamaa zako wengi wamelelewa kwenye hii tabia mbaya ndio maaana utatetea kwa kila sababu kuwa ukabila hakuna.

nimekupa mfano hai kuwa mdogo wake kamishina wa ushuru na forodha George Lauwo(mchagga) kapewa kitengo cha container bila kuwa na elimu inayositahili, na Benny lusege ana masters tena toka UK,alipeekwa sehemu mbaya isiyostahili elimu yake na akaishia kuchomewa moto nyumba yake. huyu Benny si mswahili mwenzangu lakini hakutendewa haki kutokana na ukabila uliopo TRA. wewe si unajitia mwandishi wa habari kwanini usipanye utafiti wa suala hili au kuwatafuta wahusika? na majina yote nimekuwekea humu!

YEBO YEBO.

SUALA LA kusema Kilimanjaro kuna shule nyingi hivyo wahitimu wengi ni wachagga sio kweli shule nyingi ni za bweni na watu wanatoka pande zote za nchi.
nakupa mfano bagamoyo kuna shule inaitwa Marian girls ambayo ni top ten kila mwaka, jee ina maana wazaramo wa bagamoyo ndio hao waliofanya vizuri? basi utakuta darasa zima hakuna hata mtu toka mkoa wa pwani. ila ukiuliza utaambiwa shule iko bagamoyo tena pwani.
nenda hata Kibiti sekondary wengi ni watu toka mbali.

Miakel phillimon.

kwani Mbowe alipopewa uenyekiti chadema alikuwa na qualification gani? ambayo watu wengine hawana? alipewa kisa mchagga tena school less! na sasa kajilipua UK. TIZAMA wenyeviti kama Professor Lipumba waliopata kwa shule zao.
najua wewe ni chadema na ulienda huko kwa kusukumwa na ukabila na una madaraka makubwa huko waliokupa hayo madaraka walijua una hisia nzuri za ukabila.
 
Back
Top Bottom