Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

mwanangu samvulachole
wengi hawakubali kuwa kuna ukabila, pia hawakubali kuna udini, lakini mwnangu mwenyewe mimi nilibahatika kufika IFM, makabila matatu ndio yanayosoma wahaya, wachaga na wanyakyusa, nisisahau wajita na wasukuma.
mimi nishaambiwa kwanini usikae nyumbani ukauza duka kama vile wao ndio wenye haki ya kusoma na sisi tusisome.
natoa mfano mwanangu
kuna baba moja kapasi la saba, kapasi form 4 kwa one mwanangu, form 6 kwa 2 ya point kumi, mwanangu chuoni nilijiuliza kapasi vipi, mwanangu kachukuwa miaka mitano kapewa cheni.
kwanini nasema kapewa cheti mwanangu kwa sisi tuliosoma uhasibu partnership ndio refufu mshikaji kesho mtihani ananiuliza basics za kilakitu, nilifunga vitabu nikaenda kulala, mshikaji kapasi ikabidi nijiulize.
kwa hiyo mwanangu ukweli hawakubali.
mfano wa sasa hivi kufananisha vatican na iran,
kwanini wasifananishe uingerteza na iran kwamba zote ni nchi za kidini
inabidi waende shule
hawajui kama uingereza oinasema dini yake ni ukristo, kusema iran ni ya kiislamu kwao ni kosa. hoja vatican ni nchi

acheni kutoa sababu za kipumbavu
 
Mwanakijiji wewe ni guru,expert,mtaalamu unaongea kwa evidence, unaijua nchi yako, ninaamini unaipenda nchi yako na wewe ni mtanzania kwelikweli.
God Bless Tanzania
 
Nimefuatilia hii thread na watu wengi wanauliza hard data kuhusu elimu. Ifuatayo ni data za elimu toka sensa za serikali ya Tanzania (2002) ambao inaonyesha level of education attainment (Std 1 to University) by region. Kwa ujumla Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi wano soma zaidi ya shule za msingi. Je hoja za Kilimanjaro, Kagera na Mbeya kuwa na wasomi wengi zipo hapa? Ingetowa mwanga kujua kati ya watoto wanaosoma zaidi ya shule ya msingi hapo Dar, je ni wangapi wana asili ya Kilimanjaro, Kagera au Mbeya? (see attached file).
 
Attachments

  • Tz_edu02.JPG
    Tz_edu02.JPG
    86.1 KB · Views: 105
Manta,

..kutokana na data zako Kilimanjaro wako nyuma ya mkoa mmoja tu wa Tanzania Bara, Dar-Es-Salaam.

..Zanzibar nao naona wana viwango vizuri tu, ingawa wao ni NCHI, siyo mkoa!!
 
Manta,

..kutokana na data zako Kilimanjaro wako nyuma ya mkoa mmoja tu wa Tanzania Bara, Dar-Es-Salaam.

..Zanzibar nao naona wana viwango vizuri tu, ingawa wao ni NCHI, siyo mkoa!!

Na kama Kilimanjaro wako nyuma ya mkoa wa Dar-es-salaam basi linganisha population ya mikoa hiyo miwili then figure it out.
 
Tonga said:
Na kama Kilimanjaro wako nyuma ya mkoa wa Dar-es-salaam basi linganisha population ya mikoa hiyo miwili then figure it out.

Tonga,

..jibu lako limenifanya nitafakari mambo mengi zaidi.

..nadhani my first reading on ZNZ might in be wrong.

..kuhusu DSM kumbuka kwamba wana-attract 'wasomi' wengi toka mikoani.

..hizi figures sidhani kama zinatosheleza kujibu maswali tuliyonayo.

..lakini lazima niseme huu ni mwanzo mzuri.
 
Jamani, mimi nilishawai kuhudhuria sherehe moja hivi, ilikuwa ya watu wa Iringa ya kuwaaga watu wa university. nilijifanya na mimi mtu wa kule(wa njomba ambako kuna kabila la wabena).. huwezi amini, alikuja Luhanjo,akaja Ana makinda naibu spika, akaja makweta,akaja Deo mwanyika wa Barrick n.k. magari ya wakubwa hadi ulinzi ulikuwepo kwenye kijibaa fulani hivi. mambo yaliyokuwa yakiongelewa pale, aisee, ni ukabila wa hali ya juu. wanaongea ati ni namna gani ya kuwasaidia watoto wa njomba na iringa kwamba ukimaliza tu Chuo wawasiliane ili wasaidiane kwenye kupata kazi. nashangaa ninyi mnawaongelea tu watu wa mbeya,kilimanjaro na wahaya. aloo, wabena na wahehe nao noma kishenzi, tena majina yao wewe sio rahisi kujua ametoka wapi, ila wao jila na mhehe au mbena yeyote wanajua anakotoka likishatajwa tu. ilinisikitisha sana.

Jamani, kwani shule nyingi ziko wapi hivi? mkoa unaoongoza kwa shule za secondary, wakwanza kilimanjaro, kuna kipindi ilifuata Iringa,ikaja mbeya,na Dar es salaam. wahaya kwao hamna shule sana, wanakimbilia kuja kusoma Dar and mikoa mingine. Mimi ningesema kwamba, Ukabila Tz upo kwa hali ya juu sana huko maofisini. na makabila ambayo labda hayajapata nafasi ni watu wa sumbawanga wanaoongoza kwa uchawi,mtwara lindi,kogoma,Dom na Tanga. Songea kuna shule za seminari kibao, na wanaoenda shule kule ni wakatoliki zaidi kuliko wengine.

Pale chuo kikuu, faculty of law, wamejaa wachaga,wapare na wangoni. faculty zingine huko ndo kabisaaa, wahaya na wanyakyusa kibao. sasa, sijui.
 
Tonga,

..jibu lako limenifanya nitafakari mambo mengi zaidi.

..nadhani my first reading on ZNZ might in be wrong.

..kuhusu DSM kumbuka kwamba wana-attract 'wasomi' wengi toka mikoani.

..hizi figures sidhani kama zinatosheleza kujibu maswali tuliyonayo.

..lakini lazima niseme huu ni mwanzo mzuri.
From there at least we can see the good conclusion.And we can make it,if we want it at all.
 
si hoja ukabila, nafikiri uwiano wa kimaeneo ndio jambo bora kwa nchi changa kama hii.Utaratibu unaotumika hata kuchagua darasa la vii kwenda shule maalum kama kibaha unazingatia maeneo zaidi kuliko ufaulu halisi kutegemea fursa.Hata uteuzi wa serikali zote ulitegemea msawazo wa nchi nzima na kwa upeo wangu ndo kati ya mambo mazuri yanayoondoa mitafaruku..kama madokta wa kichaga,kihaya, na kinyakyusa tayari wapo watatu mahali kuna uzuri gani kumchagua wa 4,watfutwe sehemu nyingine.
 
Kama ofisi nyeti ya bunge wamechuliwa watendaji toka darasa moja chuo kimoja.st.augustine. waliofanya hivyo ni Dap Nombo na katibu wa bunge kashilillah.huo ni ufisadi wa hali ya juu.someni thread ya bunge lakumbwa na kashfa.muone uozo wa ofisi nyeti za serikali.
 
Ndugu zangu yote yaliyojadiliwa yanaukweli . Pia na historia inachangia. Mfano wilaya yangu tulikuwa nyuma sana kielimu mpaka miaka ya tisini ndio tukaanza kuibukia. Nipokuwa chuo kikuu miaka ya 2000 nilihudhiria mkutano wa wanafunzi wanaotoka walaya yangu, karibu asilimia 95% walikuwa wanasomea shahada za uwalimu. Pamoja na kuwa wengine walikuwa na pass nzuri lakini walikuwa hawako tayari kujiunga na kozi za fani nyingine. Sababu kubwa ni uwezekano wa kupata ajira mara wamalizapo masomo hivyo wengi kujisalimisha mapema kwenye fani ya ualimu na kuwaacha wachache wenye uthubutu kuopt hizo kozi. Nimewahi kufundisha shule moja ya kilimanjaro, majority ya wanafunzi wangu wengi A-Level walitaka kujiunga chuo kikuu wasomee masomo ya biashara au uhasibu. Ukifika vyuo vikuu kwenyewe hali inajionyesha pia ambayo nayo inakuja kujirefrect kwenye ajira na hasa pale ajira zinapokuwa za shida. Implication ni kuwa fani kama za uhasibu au biashara majority ya wanafunzi wanatokea maeneo machache ya nchi. Ukija kuongezea na uhaba wa ajira basi ndio kabisa nani wa nani inaanza, na watakaoamua aajiriwe nani ni wale wanaoshikilia ofisi. Mara chache pale ajira zinapokuja kutangazwa kwa uwingi kama ilivyo kuwa hivi karibuni TRA na idala nyingine, swala la upendeleo kwenye kuajili linakuwa limepungua. Upendeleo unapoamia kwenye kupanga nani awekwe wapi. Na yote yanafanyika kwa watu walioko juu kuhakikisha kuwa himaya zao zinalindwa.

Hivyo kubreak through cylce ya namna kazi ipo. Inahitaji kiongozi mwenye vision na asiye fisadi ambaye anajua Tanzania ya namna gani tunayotaka kuijenga. Mfano anapofanya uteuzi, analetewa majina labda matano na yote ni ya kabila moja, anafanya jitihada gani kujua kama kuna minorities kwenye hilo shirika na ni watendaji kazi wazuri ambao pia wanasifa za kepewa hiyo na fasi ila kwa uchache wao majina yao hayawezi kupenya?
 
makabila mengine ya mezubaa
mfano Igunga wanampa ROSTAM alafu wanalalamika wachaga , wachaga hawawezi kumpa rostam.
nenda kilimanjaro na arusha ni wachagga ndio wanamiliki biashara nyingi, nenda singnida, tabora na moro utakutana na kina nani....

kilimanjaro hamna waindi kwa ajili wachaga ni very competitive. (kama waindi wamewashindwa makabila mengine sio raisi kuweza kushindana nao na ndio maana wanatumia kadi ya ubaguzi)
na hizo takwimu zinaonyesha dar 0.8, unguja mjini 0.8, arusha 0.7, halafu kilimanjaro 0.4 lakini humu ndani mmekua mkisema ikitoka dar inafuata kilimanjaro (bias against kilimanjaro) No price for guessing where am from

enough is enough against wachaga maana yake mtoa mada ametaja mkoa wa kilimanjaro tu....
serikali imeweka passmark kubwa mkoa wa kilimanjaro kupunguza idadi yao matokeo yake wanafunzi wanaotoka kil. wamekua wakisoma sana(wameongeza ushindani wakati mikoa mingine ikipunguza ushindani), na wazazi wa kilimanjaro wakaanzisha shule za wazazi.

ukiondoa shule wachaga ambao hawajasoma wanamiliki baa, na maduka mengi dar na huu nao ni ubaguzi??? mtu ajibu hili
hata ma shoe shiner wengi ni wachaga hawakubali kukaa bila ajira, hata wauza chips wote huu ni ubaguzi. hizi ni conspiracy zisizokua za ukweli

mchaga akijenga mkoa anaofanyia shughuli zake atajitahidi ajenge na kwao pia makabila mengine hayakumbuki kwao
 
Mzee Mwanakijiji
"..the work of the civil servants and people in the parastatal organizations does require education..it so happened that the Tanzanians who had the opportunity for higher education under the colonialists were mostly Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa. And because most of the education was provided by missionaries, most of these people are also Christians. That was our inheritance. These conditions will change, but they have not changed yet. And for these reasons, when we get rid of the Europeans who were doing responsible jobs, and give these jobs to Tanzanians, the people who get them come mostly from one or other of these three tribes

Mwanakijiji hivi unataka kiniambia kuwa tangu tu uhuru "these conditions" have not yet changed. Don't hide behind Nyerere's rhetoric MK. Hali imebadilika sana na makabila mengi sana yameelimika sana kuliko hata hao wala ndizi, lakini tatizo ni kuwa wao wana historical advantage. Wamekuwa wanarithishana na kupendeleana hadi kesho, Hivi unataka kuniambia kuwa wenye sifa za kuwa TRA au treasury ni wachaga tu. In 1960's ningekubali, lakini in 2009? no. au wenye sifa za kuwa NIC ni wanyakyusa tu? no wonder wameiua na sasa wana jifanya wanaonewa.

Unjau kabisa ndani ya moyo wako kuwa makabila haya ya wala ndizi wana ubaguzi wa hali ya juu wa kupendelea watu wa makabila yao. These feel more secure wheh they are surrounded by people from the same tribe. MK wewe ni mlandizi and that is what you feel you can not deny it. MK ukiwa na nafasi ya kuajiri na nikaja mimi mzaramo mwenye experience ya 5 yrs, na mla ndizi mwenzako mwenye same ducation as mine but exp ya 1 year itakuwa ni muujiza kama utaniajiri mimi mzaramo.

Walandizi are very bureacratic, dishonest, ndio chanzo cha rushwa iliyokithiri civil serivice ya TZ an bureacuracy. Serikali inaoongezwa na civil service (technocrats) haiongozwi na wanasiasa, politicians come and go. Kwa hiyo kwa sbb civil service imekuwa chini ya walandizi since independence, backwardness ya TZ is part to blame on uzandiki wa walandizi. Na nina waambia siku mlandizi akishika nchi, tutafute pa kutokea. Tell me MK kwa nini Nyerere aliapa mlandizi asichukue nchi?
 
Hii mada haifai kuwekwa inachochea watu fulani kuwachukia wengine mwanzo ndio huo makabila halafu mkimaliza mnaingia mambo ya Udini ni hatari kwa taifa hili kama mtu ni mtanzania na anitumikia nchi yake kwa mojo mmoja kwanini leo kuwe na ukabila unaotengeza nchi sio ukabila isipokuwa ni uzalendo wamtu tusigeuke kama wale Viongozi wa kule ZANZIBAR kila wakiwa mikutanoni utawasikia wakiwashambulia ndugu kutoka pemba lakini ukingalia karibu wote wamekwenda kuchukuwa visura na kuwaowa ambao wenye asili ya pemba kutokea mwenywe Rais amani na mawaziri wake kila mmoja anataka vyakungara
 
Hebu tuambie kile ulichoambiwa nasi tupime ukweli wake.
Tupe tu majina ya hao wachagga/wanyakyusa/wahaya na post walizonazo.
hapa hachukiwi mtu; ni hoja zako tu mwanangu zinaongea na kuipa hoja yako hiyo popularity

Suala la ukabila/udini lipo wazi kabisa katika taasisi nyingi tu, kwa wale waliowahi kufanya kazi kiwanda cha sigara wanakumbuka enzi za Mzee Msangi mambo yalikuwaje pale, yeye mwenyewe alipitia mgongo wa Mh. PM kipindi hicho Mh. Msuya. Bima tunakumbuka enzi za Mzee Mwaikambo wale ndugu zangu wa Mwa.... walijazana bima. Mfano mwingine kipindi cha nyuma pale UD sijui sasa hivi hali ikoje utakuta tangazo notice board eti wanafunzi wa kabila flani wana mkutano wao, hizi zote ni elements za ukabila. Mungu atusaidie.
 
Mzee Mwanakijiji
"..the work of the civil servants and people in the parastatal organizations does require education..it so happened that the Tanzanians who had the opportunity for higher education under the colonialists were mostly Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa. And because most of the education was provided by missionaries, most of these people are also Christians. That was our inheritance. These conditions will change, but they have not changed yet. And for these reasons, when we get rid of the Europeans who were doing responsible jobs, and give these jobs to Tanzanians, the people who get them come mostly from one or other of these three tribes

Mwanakijiji hivi unataka kiniambia kuwa tangu tu uhuru "these conditions" have not yet changed. Don't hide behind Nyerere's rhetoric MK. Hali imebadilika sana na makabila mengi sana yameelimika sana kuliko hata hao wala ndizi, lakini tatizo ni kuwa wao wana historical advantage. Wamekuwa wanarithishana na kupendeleana hadi kesho, Hivi unataka kuniambia kuwa wenye sifa za kuwa TRA au treasury ni wachaga tu. In 1960's ningekubali, lakini in 2009? no. au wenye sifa za kuwa NIC ni wanyakyusa tu? no wonder wameiua na sasa wana jifanya wanaonewa.

Unjau kabisa ndani ya moyo wako kuwa makabila haya ya wala ndizi wana ubaguzi wa hali ya juu wa kupendelea watu wa makabila yao. These feel more secure wheh they are surrounded by people from the same tribe. MK wewe ni mlandizi and that is what you feel you can not deny it. MK ukiwa na nafasi ya kuajiri na nikaja mimi mzaramo mwenye experience ya 5 yrs, na mla ndizi mwenzako mwenye same ducation as mine but exp ya 1 year itakuwa ni muujiza kama utaniajiri mimi mzaramo.

Walandizi are very bureacratic, dishonest, ndio chanzo cha rushwa iliyokithiri civil serivice ya TZ an bureacuracy. Serikali inaoongezwa na civil service (technocrats) haiongozwi na wanasiasa, politicians come and go. Kwa hiyo kwa sbb civil service imekuwa chini ya walandizi since independence, backwardness ya TZ is part to blame on uzandiki wa walandizi. Na nina waambia siku mlandizi akishika nchi, tutafute pa kutokea. Tell me MK kwa nini Nyerere aliapa mlandizi asichukue nchi?

mimi sizadhani kama tumefikia mahali pa kulalamika kwamba ukabila umekithiri TZ ila kama kuna dalili basi tujaribu kuziondoa. Nakumbuka Prof. Beda wa pale UCC-UDSM alilaumiwa kwamba eti anaukabila pale UCC lakini yeye alikuwa akiuliza "hivi mnaolalamika eti siwapi vyeo kwa kuwa siyo wahaya je wakati mnaomba kazi kwenye mkataba kulikuwa na kipengele kinasema utapewa cheo flani baada ya kuajiriwa?", Wengi tulishindwa kujibu swali hilo.
 
mara nyingine nafikiria kuwa kama sehemu nyingi wachagga, wahaya wasukuma na wanyakyusa wamekuwa wengi wakifanya kazi tangia tupate uhuru na mpaka leo 'maendeleo' yetu ni kidogo basi haya makabila hayawezi kukwepa lawama za sis kufikia hapa.

lakin tukumbuke wamekuwa chini ya nyerere, mwinyi, mkapa na sasa kikwete ambao si kutoka makabila hayo

mashirika mengi na viwanda kibao vimekufa au viko hoi. je, tuyalaumu makabila yaliyokuwa yamejazana humo? uwezo wao ulikuwa unaanzia wapi na kuishia wapi? maraisi, viongoz wa chama (ccm), na wa serikali hawakuwa na influence katka kundesha mashirika na viwanda vyetu?

naamini ukiangalia sana utakuta wa kulaumiwa ni siasa yetu na uongoz wa juu kabisa ambao ndio ulikuwa unatoa mwelekeo wa jins gani tuendeshe mashirika na viwanda vyetu. miongozo ambayo ndio imetufikisha hapa
 
Back
Top Bottom