Unaweza kuwa na hoja mkuu ila binafsi nina tatizo na jinsi unavyowasilisha hoja zako. Watanzania tuko 45mil ila kati hao, wanaofaa au wenye uelewa wa mambo ya mpira wa miguu kwa kiwango cha kuchukua uongozi wa juu katika level ya kitaifa hawawezi kufika hata 1000 (please correct me if I am wrong). Kwa hiyo hatuwezi kuangalia walioteuliwa kwa population ya watanzania wote 45mil.
Hoja ambazo zingetusaidia sisi wengine tunaofuatilia mjadala huu ni kama hizi hapa:
1. Je nafasi husika zilitanganzwa kwa umma?
2. Watu wangapi na wenye sifa zipi waliomba hizo nafasi (tuwekee sifa za waliopata + waliokosa)
3. Kazi ya kutangaza nafasi, kuchuja majina, kufanya usaili na uteuzi ilifanywa na nani?
4. Je, wale waliofanya kazi hiyo walikuwa huru au waliingiliwa na wakubwa wa TFF kwa maslahi binafsi?
5. Je, taratibu za ajira katika nafasi za utendaji ndani ya TFF zinasemaje?
6. Kuna ukiukwaji wa taratibu umefanyika katika hatua yoyote?
7.
8.
Hata hivyo, ikitokea nafasi kuu za juu katika taasisi moja kujazwa na watu wenye haiba/dini/kabila moja hata kama wana sifa za kutosha siyo jambo zuri.
Ila kwa sasa ningeomba tupewe uchambuzi wa hoja badala ya kuwamwagia watu tuhuma bila uchambuzi wa kutosha kusupport allegations zinazotolewa.
Pia naamini Ndugu
Jamal Malinzi atakuja kutupatia ufafanuzi zaidi,