Tunajitahidi sana kuwapeleka Mashuleni, tatizo ni Mfumo. Mfumo unatukandamiza sana Wandengereko.Kwanza tunasoma ktk mazingira magumu, pata picha shule nyingi za mkoa wa pwani walimu ni wachache sana tena niwale wenye ufaulu wa chini ndio wanao tupwa kwetu, huwezi amini zipo baadhi ya shule zina walimu mmoja mmoja, we unafikiri kitazaliwa nini hapo? Wenzetu munapigania shule za mikoa yenu ziwe na maabara wakati kijijini kwangu mtoto mpaka anamaliza la saba hajawahi kalia dawati kilasiku ni kulima shamba la mwalimu tu, je hapa utazalisha wasomi kweli? Kunamengi sana ndani ya nchi hii lakini watu tuko kimya tu. Wasiwasi wangu kuna bomu mbeleyetu linakaribia kulipuka, hivyo tusishangae tukijikuta tumeungana na Sudani kusini ktk kulizima bomu hilo.