Habari ya mda huu wanajanvi!
Bila kupoteza mda, kutokana na kauli iliyo tolewa na muheshimiwa Rais juu ya maendeleo ya ugonjwa wa Corona hapa nchini.
Kwa mtu mwenye mtazamo mpana kimsingi ni kauli inayo pelekea mtu ajiulize maswali mengi na pengine yasiwe na majibu:-
Ikiwa Rais yeye mwenyewe kwa kinywa chake alikili kuwa mashine za kupimia virusi vya Covid-19 zina matatizo, imewezekanaje akazipata takwimu hizo za wagonjwa wa Corona?
Amewezaje kuziamini takwimu hizo kama ni sahihi?
Ikiwa maendeleo dhidi ya udhibiti wa ugonjwa wa Corona nchini ni mazuli, inakuwaje madereva wa magari ya mizigo kutokea upande wa Tanzania wakutwe na maambukizi ya virusi vya Covid-19?
Inamaana Kenya, Uganda, Rwanda, Zambia wanahuhadaa ulimwengu kuwa idadi kubwa ya watanzania wameathirika na virusi vya Covid-19. Wanafanya hivyo kwa faida ya nani?
Muheshimiwa Rais anapofikilia kutoa maamuzi juu ya ufunguzi wa vyuo nchini, anahuakika gani kuwa maambukizi yameisha mitaani. Ametumia mbinu gani kuwapima wananchi wote nakuthibitisha hilo?
Linapo kuja swala la kufunguwa vyuo hapa nchini Rais atambue kwamba kuna wanafunzi wanaotokea nnje ya nchi na wanasoma hapa nchini.
Kimsingi Rais anatowa maamzi kwa kupaniki na bila ya kushirikisha akili yake. Rais anataka kila mtu akubaliane na mawazo yake.
Kuwa Rais hakukufanyi wewe uonekane una akili nyingi na mitazamo mipana kuliko wananchi wote unao waongoza. Hata mtu wa mwisho darasani kwenye mitihani anaweza akapewa dhamana ya kuwa kiongozi.
Kalibuni kwa maoni...
Not everyone is willing to take the risk!
Ina maana wewe unamwamini sana Museveni kuliko Rais wako Magufuli? Uhuru Kenyatta je naye anasema ukweli kuliko Magufuli? Kwa hiyo unataka kutuaminisha sisi kuwa Marais wengine wote wanayo yasema ni kweli isipokuwa Rais wako Magufuli tu ndiyo humwamini kwa sababu namba anazozitoa sio sahii?
Naomba nikuulize baadhi ya maswali Rais Magufuli alipotoa hotuba yake ya kwanza Bungeni Dodoma kuna mambo mengi aliyasema ambayo alikusudia kuyatekeleza. Je, katika yale aliyo yaahidi kutekeleza mangapi ameyatekeleza na magapi haja yatekeleza?
Uhuru Kenyatta amewaahidi mangapi wananchi wake na mangapi ameteleleza?
Kwa mfano mwaka uliopita aliwahutubia wananchi wake kuwa kuna ufisadi Katika kila sekta na atahakikisha kuona kuwa ufisadi unateketea, je, amefanya jitihada zozote za kutokomeza huo ufisadi alio usema?
Je, Magufuli hajatokoneza ufisadi kwa kiasi kikubwa?
Niambie nchi gani katika kanda ya EA ambayo within 5 years imejitahidi kutekeleza mambo mengi kuliko Tanzania ukiondoa Rwanda ambayo ilipewa misaada kem kem na idadi ndogo ya watu?
Unajua kuwa Kenya ni masikini sana kuliko Tanzania? Viwanda vingi vilivyoko Kenya ni aidha mali ya wazungu au wahindi. Tanzania viwanda vingi ni mali ya umma. Tulijaribu kuvitaifisha, lakini tuliyo yapata tumejionea wenyewe.
Mwisho inakuwa hivi, kama mtu haridhiki na uongozi wa mtu anaye tawala, mara nyingi mwenye kutoridhika anajitahidi ili yeye mwenyewe awe kiongozi ili arekebishe asicho kiona kizuri au kile kinacho tendwa vibaya. Vinginevyo mtu anaamua kuhama nchi na kwenda nchi nyingine.
Sent using
Jamii Forums mobile app