Ukakasi wa taarifa ya Rais Magufuli juu ya maendeleo ya ugonjwa wa COVID-19 nchini

Ina maana wewe unamwamini sana Museveni kuliko Rais wako Magufuli? Uhuru Kenyatta je naye anasema ukweli kuliko Magufuli? Kwa hiyo unataka kutuaminisha sisi kuwa Marais wengine wote wanayo yasema ni kweli isipokuwa Rais wako Magufuli tu ndiyo humwamini kwa sababu namba anazozitoa sio sahii?

Naomba nikuulize baadhi ya maswali Rais Magufuli alipotoa hotuba yake ya kwanza Bungeni Dodoma kuna mambo mengi aliyasema ambayo alikusudia kuyatekeleza. Je, katika yale aliyo yaahidi kutekeleza mangapi ameyatekeleza na magapi haja yatekeleza?

Uhuru Kenyatta amewaahidi mangapi wananchi wake na mangapi ameteleleza?
Kwa mfano mwaka uliopita aliwahutubia wananchi wake kuwa kuna ufisadi Katika kila sekta na atahakikisha kuona kuwa ufisadi unateketea, je, amefanya jitihada zozote za kutokomeza huo ufisadi alio usema?

Je, Magufuli hajatokoneza ufisadi kwa kiasi kikubwa?

Niambie nchi gani katika kanda ya EA ambayo within 5 years imejitahidi kutekeleza mambo mengi kuliko Tanzania ukiondoa Rwanda ambayo ilipewa misaada kem kem na idadi ndogo ya watu?

Unajua kuwa Kenya ni masikini sana kuliko Tanzania? Viwanda vingi vilivyoko Kenya ni aidha mali ya wazungu au wahindi. Tanzania viwanda vingi ni mali ya umma. Tulijaribu kuvitaifisha, lakini tuliyo yapata tumejionea wenyewe.

Mwisho inakuwa hivi, kama mtu haridhiki na uongozi wa mtu anaye tawala, mara nyingi mwenye kutoridhika anajitahidi ili yeye mwenyewe awe kiongozi ili arekebishe asicho kiona kizuri au kile kinacho tendwa vibaya. Vinginevyo mtu anaamua kuhama nchi na kwenda nchi nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu,lakini ingekuwa vyema kuwaeleza watanzania na dunia kuwa mmetumia strategies zipi kuupunguza
Ameeleza vizuri kuwa hata mtoto wake aliugua akapona kwa kujifukiza tu. Labda swali la kujiuliza ni amejuaje kuwa ugonjwa umepungua huku yeye mwenyewe alisitisha kupima ugonjwa kwa kuwa machine za kupimia ni batili na watalaam wa kupima kutumbuliwa? Wenye akili walihoji kama mashine in mbovu zinatoa majibu yasiyosahihi kwanini watalaam watumbuliwe huku ni Serkali yake ndo ilizinunua? Maswali na majibu ni mengi!
 
Hivi wewe kama ulikuwa unaumwa, ukipona huwezi kujua kama umepona?
Ina maana hata ukiumwa hauwezi kujua kama unaumwa mpaka ufanyiwe vipimo!! Kama ni hivyo utakuwa ni mfu!!
Sasa wewe ukiugua corona unewezaje kusema ni corona bila kupima? Utasema najisikia maumivu ya kichwa, viungo, pumzi kubana, nk dadili hizi sio kwa corona tu zaweza kuwa malaria, typhoid, etc. Ndio maana watanzania mnafanya mambo kienyeji enyeji na hamuoni haja ya kupima corona na kutoa taarifa. Mmekuwa aibu duniani kote kwa ukienyeji wenu hasa nyie ccm.
 
Kuna watu nawashangaa sana,
Utawakuta wako bize kumpinga raisi kwanini tz hakuna lockdown huku yeye kila siku yuko bize kuja mjini kutafuta ela, tena wengine wana uwezo mzuri tu wa kula hata mwaka bila kufanya kazi,
Kama wanaona raisi anakosea kutoa amri ya lockdown kwanini wasijifungie wao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uamuzi wa kwanza unatakiwa yeye atoke chato aje dar au dodoma..

Yeye amejificha kisha anataka watoto wa wengine wafe.
Kwa hiyo yeye akija dar corona itaisha?
Hata sasa hivi kuna maduka ukienda wameweka uzio ina maana hawawapendi wateja wao? La hasha ni sehemu ya kuchukua tahadhari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Duniya ina ajabu ...
Tanzania wana Magufuli lakini amewaachiya uhuru ,
Kenya tuko na Uhuru lakini ndio katupiga magufuli ..."
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Uhuru wa Magufuli ni feki sababu hatoi takwimu. Magufuli ambayo Uhuru kawapiga wakenya, nayo ni feki kwa sababu wana Uhuru mkubwa wa takwimu. Hivyo kikweli waliopigwa Magufuli ni watanzania. Wakenya kiukweli wako huru.
 
Uhuru wa Magufuli ni feki sababu hatoi takwimu. Magufuli ambayo Uhuru kawapiga wakenya, nayo ni feki kwa sababu wana Uhuru mkubwa wa takwimu. Hivyo kikweli waliopigwa Magufuli ni watanzania. Wakenya kiukweli wako huru.


Unataka takwimu za nini ambazo huna ni kueleweka pa kuzipata
 
Unataka takwimu za nini ambazo huna ni kueleweka pa kuzipata
Kweli kabisa, na hata hizo takwimu alizotoa Rais Magufuli jana, kuhusu wagonjwa waliobaki katika hospitali mbalimbali, haziaminiki. Hatujui kama hao ni watu au mapapai yaliyopewa majina ya watu. Tunajua maabara yetu bado inafanyiwa UHAKIKI!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…