Ukali wa Maisha: Wananchi waiomba Dstv ipunguze vifurushi vyake

Ukali wa Maisha: Wananchi waiomba Dstv ipunguze vifurushi vyake

Nilitaka ninunue DStv Leo ili nijiandae na World Cup, itabidi nisikilizie kwanza bei mpya ya ving'amuzi.
Subiria bei mpya septemba. Compact inaweza ikafika 69,000/=
 
Nunua tu, huwa wana coverage nzuri ya World Cup
Coverage huwa ni moja tu ambayo FIFA ndo wanasambaza kwa vituo vyote . Kwahiyo nachokiona mimi wa DStv ndo hicho hicho ataona wa Startimes

Labda zile pre game, half time na post game analysis ndo kila broadcaster anafanya kivyake... kwa hilo wako vizuri sana
 
World cup nadhani tv station za serikali uwa zinaruhusiwa kasoro kwetu tbc sijui uwa wana shida gani,so unaweza kuangalia world cup azam tv kwa kupitia ubc,kbs nadhani hata tv za malawi na rwanda uwa wanaonyesha pia
Bado sisi wenye dstv wembe ni ule ule unless kununua king'amuzi kingine
 
Coverage huwa ni moja tu ambayo FIFA ndo wanasambaza kwa vituo vyote . Kwahiyo nachokiona mimi wa DStv ndo hicho hicho ataona wa Startimes

Labda zile pre game, half time na post game analysis ndo kila broadcaster anafanya kivyake... kwa hilo wako vizuri sana
Kumbe jibu unalijua
 
Kupitia ukurasa rasmi wa Dstv huko Instagram, wananchi wengi ambao ni wateja wa Dstv wameomba kupunguziwa gharama hasa kwenye vifurushi kutokana na ukali wa maisha.

Wengine wakaenda nbali zaidi, kuwa wanatumia king'amuzi cha Canal hivyo hawako tayari kunyonywa na gharama kubwa za Dstv.

Wakati hayo yakiendelea, chini ya kapeti kuanzia septemba 1 kutakuwa na mabadiliko ya bei mpya za vifurushi kutoka Dstv ambapo nimedokezwa kuwa gharama zitapanda kidogo.
Kwahyo mjiandae kwa maumivu zaidi.

View attachment 2312409View attachment 2312410View attachment 2312411View attachment 2312412
Uhuru wa soko huria upo wapi hawa makaburu wamehodhi matangazo ya mpira ligi za Ulaya, kuhodhi huku mbona hakupo Ulaya, Uarabuni,marekani na hata Naijeria, Nape inabidi uje huku hawa wa ving'amuzi pamoja na makampuni ya simu yantunyonya sana.
 
Back
Top Bottom