Ukali wa Maisha: Wananchi waiomba Dstv ipunguze vifurushi vyake

Nilitaka ninunue DStv Leo ili nijiandae na World Cup, itabidi nisikilizie kwanza bei mpya ya ving'amuzi.
Subiria bei mpya septemba. Compact inaweza ikafika 69,000/=
 
Nunua tu, huwa wana coverage nzuri ya World Cup
Coverage huwa ni moja tu ambayo FIFA ndo wanasambaza kwa vituo vyote . Kwahiyo nachokiona mimi wa DStv ndo hicho hicho ataona wa Startimes

Labda zile pre game, half time na post game analysis ndo kila broadcaster anafanya kivyake... kwa hilo wako vizuri sana
 
World cup nadhani tv station za serikali uwa zinaruhusiwa kasoro kwetu tbc sijui uwa wana shida gani,so unaweza kuangalia world cup azam tv kwa kupitia ubc,kbs nadhani hata tv za malawi na rwanda uwa wanaonyesha pia
Bado sisi wenye dstv wembe ni ule ule unless kununua king'amuzi kingine
 
Kumbe jibu unalijua
 
Uhuru wa soko huria upo wapi hawa makaburu wamehodhi matangazo ya mpira ligi za Ulaya, kuhodhi huku mbona hakupo Ulaya, Uarabuni,marekani na hata Naijeria, Nape inabidi uje huku hawa wa ving'amuzi pamoja na makampuni ya simu yantunyonya sana.
 
Unakuta Simba SC inacheza na Zamalek hapo kwa Mkapa, KBC au NTV za Kenya wanaoesha mechi hiyo huku TBC kuna kipindi cha Bakita.

Na ZBC ya Zanzibar unakuta wanaonesha hiyo mechi

Tanzania bado tuko nyuma sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…