Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Hivi vivuko vinabeba sana kupita uwezo wake sio hicho tu kuna vivuko vinabeba mizigo na watu hadi vinakema.

Usimamizi na umakini unatakiwa kwenye vivuko vyote nchini, pia sijajua kama MV Nyerere haikuwa na maboya.
Kitu kimepinduka mkuu.....unapataje boya hapo .......
 
Inawezekana umesoma ila na wewe elimu yako haijakusaidia ova
 
Unatumia mabilioni ktk chaguzi zisizokuwa za lazima, huku watanzania zaidi ya 20O. Wakifa kwa uzembe.
 
Ilishafanyiwa ukarabati na ikawekewa injini mbili mpya na mwezi July 2018 ikaanza kazi. Kama you are not informed you better ask!
 
Kumbuka kuna mizigo,magari na vitu vizito
 
Ingetumika busara kuomba msaada Kenya tungeokoa zaidi ya walio okolewa.
Kawa wavuvi wasiokua na vifaa wala taaluma ya uokoaji waliokoa 37. Watu waliosomea na kubobea wangeweza kuongeza idadi ya walio hai mara nyingi tu. Tisione aibu kuazima kama hatuna watalam
 
Hivi hizi ajali za meli Tanzania huwa ni kafara au vipi? Yaani toka 8mchana mpaka Giza kinaingia hakuna hata helicopter ya kurandaranda
 
Haswaa.
Kama mpaka sasa waliopatikana hai na waliokufa jumla yao ni 176, na serikali inasema kile kivuko kilibeba watu zaidi ya 400, hiyo ina maana kuna zaidi ya miili 234 bado ipo ndani ya maji, otherwise tunachezewa akili.
 
Tanzania inachosha tu, mita 50 ziue watu wote hao!
Mm nadhani hilo litakuwa kafara LA wao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…