Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Mkuu huyu ni shuhuda au manusura?

Lakini pia umejuaje kwamba huyu mwandishi alikuwemo kweli kwenye hio ferry? Maana sidhani kwa akili za kawaida mtu anusurike ajali kama ile ambapo hata simu yake iliharibika kwa kuingiliwa na maji, leo hii tayari kapata nyingine, (tena kule ukara hakuna duka la smartphone hadi avuke aende Ukerewe) na hapo hapo kapata ujasiri wa kuandika kwenye mitandao eti sijui ni shuhuda?

Nimeona hii post yake kwenye uzi flani nikaipuuza ila wewe naona umeibeba nzima nzima na kuifungulia uzi. Sasa tuthibitishie kuwa kweli yule alikuwemo kwenye ferry.
 
Bahati nzuri umenielewa kwamba nilikisia tu
 
Kama ile dala dala iliyotumbukia kigongo ferry pale jijini mwanza. Dereva alimpa deiwaka.
 
Leo kuna mtu katolewa akiwa hai siku ya 3, waite kunguni wenzio wa kijani muweke kikao kujitetea. Halafu Nani alikwambia kwenye maafa cha kwanza ni usalama wa waokoaji? Usidanganye watu hapa.
 
Huyu jamaa yuko vizur alijitengenezea mazingira mazir ya emegency hongera sana
 
Ulikuwa kwenye eneo la Tukio? Si uendelee tukuone ulivyo jasiri
Aibu yenu na Mkuu wa Mkoa. Siyo tu kuwa kwenye eneo la ajali, nilivuka na hiyo meli asubuhi toka Bwisya kwenda Bugolora kabla ya ajali mchana.
 
Ulipinga tangu awali, na nilikuunga mkono. Wengine wakasema eti haiwezekani mtu kuwa hai masaa 4 baada ya ajali, Leo MTU katoka akiwa hai baada ya masaa zaidi ya 44! Aibu hii Mingela jiuzulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…