Kwanza napenda kutoa pole sana kwa msiba mkuu uliowapata ndugu zetu wa Visiwa vya Ukerewe na Ukara (UK)baada ya ajali ya Meli ya MV Nyerere. Huu ni msiba ambao umewagusa Watanzania wote bila kujali itikadi zao za Kidini na Kisiasa.
Hata hivo katika mazingira yasiyoweza kuepukika lazima tuseme kuwa CHADEMA watakuwa wameathirika kwa kiwango kikubwa sama kwa vile hii ni ngome ya CHADEMA kwa maana ya jimbo la CHADEMA ambapo Mhe. MbungeJosedph Mkundi ndiye chaguo la Wana Ukerewe.
Mhe. Mkundi aliwahi kuzungumzia ubove wa MV Nyerere lakini kwa vile ni Mbunge wa CHADEMA Serikali na CCM yake walimpuuza kuwa hana hoja kwa vile yeye anatoka upinzani!!!
Tumemsikia Mhe. Rais akitoa salamu za rambirambi na maombolezo ya siku 4 kwa msiba huu mkubwa na akaonya kwamba Wanasiasa wasitake kutafuta KICK za kisiasa kutokana na ajali hii. Sijaelewa Rais ana maanisha nini watu kutafuta kick za Kisiasa....?!Maana kama Watanzania na Wanasiasa wana anza kuhoji kwanini ajali imetokea wakti tayari kulikuwa na viashiria vya Kivuko cha MV Nyerere naMbunge wa eneo husika alipeleka taarifa hiyo Mwezi April, 2018(mwaka huu)Bungeni lakini haikufanyiwa kazi....1!!
Leo ajali imetokea Watz na Wana- UK wanahoji kulikoni lakini Raisi anawaambia Wanasiasa waache kutafuta kick za Kisiasa...!!!Hivi nani anayetafuta Kick za Kisiasa hapa? Je, ni Mbunge aliyepeleka hoja hii Bungeni kabla ya ajali kutokea au ni Serikali ambayo haikuchukua hatua kuzuia kuzuia ajali hii isitokee au ni Rais anayeanza kutoa vitisho kwa Watanzania na Wanasiasa wasihoji, kudadisi na kukumbushia alichosema Mbunge wa Jimbo husika??
Angalia hotuba ya Rais Magufuli akiwa Ukerewe hivi majuzi tarehe 4 Septemba, 2018. Magufuli hakuzungumzia lolote kuhusu hichi Kivuko cha Ukerewe.....Hii hotuba ni sawa na kula matapishi...maana hapa anaponda Wabunge wa Upinzani akiwemo Mbunge wa UK kuikataa Bajeti ya Serikali hivyo HASTAHILI KUPEWA MRADI wowote ukiwemo huu wa kukarabatu au kukibadilisha Kivuko cha MV. Nyerere kilichpata ajali. Je, nani anatafuta kick hapa?
Dhambi ya Ubaguzi wa Itikadi za Kisaisa inalitafuna Taifa......Hatari sana.