Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Just imagine capacity yake ilikuwa watu mia, ina maana kila wakati walikuwa wakiwasilisha mauzo ya 100 lkn wanabeba zaidi ya abiria 300, hii excess ilikuwa inawakilishwa kwa nani? je, mizogo excess ilikuwa inawakilishwa kwa nani? tunapofanya uchunguzi wa hili jambo turudi juma kuuliza walianza kubeba hii excess tangu muda gani na walikuwa wanaiwakilisha kwa nani? iundwe tume kuchunguza kwanza hizi pesa zilikuwa zinaenda kwa nani, na hao watu wakamatwe na wafilisiwe. Mods msiunganishe huu uzi, tuanzie hapa kwa uchunguzi ili wale samaki wakubwa wapatikane.

Wewe Ofisini Kwako hapo ulipo hupigi Hela tena pengine hata kwa Kuwadhulumu na si ajabu hata Kuwaroga wenzio? Tuanzie hapa Kwanza tafadhali.
 
Poleni kwa wafiwa wote kwa kupotelewa na ndugu, jamaa na marafiki.

Raha ya Milele uwape ee Bwana na Mwanga wa milele uwaangazie, Roho za Marehemu wote wapate rehema kwa Mungu na wapumzike kwa Amani.

Majeruhi wote nao tunawaombea waweze kupona kurejea katika hali zao za kawaida.

Ni lini tunajifunza kutafuta chanzo na sio matokeo? Na ni lini tutaacha kuishi kwa mazoea?
 
Kwanza napenda kutoa pole sana kwa msiba mkuu uliowapata ndugu zetu wa Visiwa vya Ukerewe na Ukara (UK)baada ya ajali ya Meli ya MV Nyerere. Huu ni msiba ambao umewagusa Watanzania wote bila kujali itikadi zao za Kidini na Kisiasa.

Hata hivo katika mazingira yasiyoweza kuepukika lazima tuseme kuwa CHADEMA watakuwa wameathirika kwa kiwango kikubwa sama kwa vile hii ni ngome ya CHADEMA kwa maana ya jimbo la CHADEMA ambapo Mhe. MbungeJosedph Mkundi ndiye chaguo la Wana Ukerewe.

Mhe. Mkundi aliwahi kuzungumzia ubove wa MV Nyerere lakini kwa vile ni Mbunge wa CHADEMA Serikali na CCM yake walimpuuza kuwa hana hoja kwa vile yeye anatoka upinzani!!!


Tumemsikia Mhe. Rais akitoa salamu za rambirambi na maombolezo ya siku 4 kwa msiba huu mkubwa na akaonya kwamba Wanasiasa wasitake kutafuta KICK za kisiasa kutokana na ajali hii. Sijaelewa Rais ana maanisha nini watu kutafuta kick za Kisiasa....?!Maana kama Watanzania na Wanasiasa wana anza kuhoji kwanini ajali imetokea wakti tayari kulikuwa na viashiria vya Kivuko cha MV Nyerere naMbunge wa eneo husika alipeleka taarifa hiyo Mwezi April, 2018(mwaka huu)Bungeni lakini haikufanyiwa kazi....1!!

Leo ajali imetokea Watz na Wana- UK wanahoji kulikoni lakini Raisi anawaambia Wanasiasa waache kutafuta kick za Kisiasa...!!!Hivi nani anayetafuta Kick za Kisiasa hapa? Je, ni Mbunge aliyepeleka hoja hii Bungeni kabla ya ajali kutokea au ni Serikali ambayo haikuchukua hatua kuzuia kuzuia ajali hii isitokee au ni Rais anayeanza kutoa vitisho kwa Watanzania na Wanasiasa wasihoji, kudadisi na kukumbushia alichosema Mbunge wa Jimbo husika??

Angalia hotuba ya Rais Magufuli akiwa Ukerewe hivi majuzi tarehe 4 Septemba, 2018. Magufuli hakuzungumzia lolote kuhusu hichi Kivuko cha Ukerewe.....Hii hotuba ni sawa na kula matapishi...maana hapa anaponda Wabunge wa Upinzani akiwemo Mbunge wa UK kuikataa Bajeti ya Serikali hivyo HASTAHILI KUPEWA MRADI wowote ukiwemo huu wa kukarabatu au kukibadilisha Kivuko cha MV. Nyerere kilichpata ajali. Je, nani anatafuta kick hapa?


Dhambi ya Ubaguzi wa Itikadi za Kisaisa inalitafuna Taifa......Hatari sana.
 
Vifo vinginevyo vinatokana na uzembe, Abiria wangelikua na uvumilivu ili kile kivuko kitie nanga na ndipo waanze kuteremka taratibu, basi isingelitokea janga hili, hii ndiyo ilitokea wakati wa MV Bukoka! Tusipokuwa na taadhali sasa ni zamu ya kivuko cha MV Jitegemee kinachotoa huduma kati ya Maisome - Kahunda- Nkome.
 
duh kwa kweli inasikitisha sana. yaani unapigwa na unapangiwa namna ya kulia mweh...
 
Unakuta mtu anashangaa idadi na anapost huku akiwa ndani ya mv magogoni iliyofurika
 
chuki za namna hii hazijawahi kumwacha mtu salama! haya ya wapiga kura wangu yanahusikaje hapa sasa!?!
Sio chuki Hero, hiyo ndio hali halisi kwa sasa hapa nchini, Mwl nyerere aliwahi kusema, Tunahitaji Utawala Bora, Siasa safi na Watu ili kuyatafuta maendeleo ya kweli, sasa hivyo vitu vikikosekana mambo yanakuwa sio sawa, inawezekana nyie wanufaika na mfumo huu mnaona Sawa tu.
 
Ivi nchi hii tumerogwa?

Inakuwaje serikali inashindwaje kuhudumia watu 200 waliofikwa na maafa mpka wachangishe watu? Tena kwa vitisho.

Nashangaa waziri wa ulinzi anadai serikali haihusiki na kuzama kwa meli ila kumbuka kuwa kivuko ni cha serikali tena kwa kusema atakaye sema serikali inahisika atakamatwa.

Ivi hela za uchaguzi zinatoka wapi ila za maafa hazipo?
 
Back
Top Bottom