Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kuna threads nyingine huku zinaletwa na wafiwa, wamechanganyikiwa kbs hata wanachoandika kimechanganyikiwa na hakieleweki. Poleni msiba ni wa Kitaifa.
 
Hicho kitabu hata kikipatikana kitakuwa na idadi ndogo ya wasafiri kwa sababu walikuwa wanapiga hela
 
Serikali ya wanyonge inaponunua ndege za mabilioni ya pesa za Watanzania masikini kwa ajili ya kupanda matajiri wachache na kuacha kununua kivuko cha wananchi masikini cha kiasi cha bilioni 2 ni kituko cha karne
 
Mimi toka nimezaliwa mpaka sasa bima/fidia pekee niliyowahi kuiskia bongo ni ya yule DIRECTOR TISS

..tukio la Lt.Gen.Kombe na fidia waliyolipwa familia yake ni tofauti na ajali ya MV Bukoba au MV Nyerere.

..Labda ungesema kwanini familia ya Kombe walilipwa fidia, lakini familia ya Daudi Mwangosi haijalipwa fidia.

..tukirudi kwenye mada yangu, CHOMBO chochote cha usafiri kinapaswa kuwa na BIMA ili ajali ikitokea WAATHIRIKA wa ajali hiyo waweze kufidiwa.
 
CCM endeleeni kukata viuno wakati hata pesa ya kununua chemli kumulika waokoaji hakuna ila mabilion ya kununua wapinzani na kurudia uchaguzi yapo tele
 
Kulikuwa na kitabu?
Hivi pale Ferry au Kivukoni kuna orodha mnapopanda kivuko?
 
Alternatively, tuulize pia. Waathirika na wahanga wa ajali wanaweza kuishtaki Serikali?

Maana nijuavyo kutokuwa na bima, haizuii kushtakiwa kama kwa uzembe wako umeshababisha ajali iliyoleta madhara kwa mwingine. (foreseable danger against foreseable victim)
 
Tunaomba TV stations zetu ziwe huru jamani, ajali kubwa kama hii ilipaswa iwe live almost siku nzima hasa hizi ambazo bado zoezi la uopoaji likiendelea
Naamini siku ilipotokea ajali vyombo vyetu vya habari hususan TV wangeripoti mapema watu na taasisi nyingi wangeleta hamasa hata mawazo ktk swala zima la udokozi, na hapo pengine hata lile swala la kusitisha uokoaji kwa ajili ya Giza lingepingwa mapema au yangetokea mawazo tofauti hivyo kungekuwepo na uokoaji hata usiku lakini kutokana na uwigo wa habari hivi sasa kuwa mwembamba, wengi tumechelewa hata kujua kama kumetokea ajali kubwa
Chombo pekee kilichopewa kibali cha kuonyesha taarifa ya habari uwezo wake wa vifaa na mvuto upo Chini sana
Serikali iliangalie hili haraka, tunaumia sana kukosa habari na mwendelezo wa matukio.
 
Mali zote za serikali yakiwemo magari huwa hayana bima mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…