Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
tindo Acha kutetea huu ujinga, huwezi kukataa kwenda kuwafariji ndugu au jamaa zako sababu ya kuogopa kudhalilishwa. Maadui wanapatana kwenye misiba, ndugu misiba ndio inawakutanisha. Je umeona Mbunge wa CDM wa Ukerewe akidhalilishwa?
CDM wapo radhi kushiriki mikutano ya Magufuli ya majimboni kwao ila sio msiba, kweli ?
Haya maneno unayosema yangekuwa na maana iwapo Magufuli naye angekuwepo. Huyo mbunge hajadhalilishwa kutokana na kile alichozungumza bungeni kuhusu hicho kivuko. Kama misiba ingekuwa inapatanisha tusingeona huu udhalimu unaondelea hapa nchini. Hakuna haja ya kuonyesha mshikamano wa kinafiki huku unafanyiwa udhalilishaji. Hata hiyo mikutano ya Magufuli hakuna haja ya viongozi wa cdm kushiriki tena kwani yote hutumika kuwadhalilisha na ushahidi upo. Tena sasa ni vyema kutangaza kabisa hakuna mwanacdm kumzika mwanaccm wala mwanaccm kumzika cdm. Bila kuchukua hatua stahiki huu mwenendo uliopandikizwa na kiongozi wa nchi utaendelea kufumbiwa macho.