Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Haya ndio tulikuwa tunayasema na sasa yanaanza kutimia!

Kwahiyo watu wasipochanga hayo hayatafanyika?

Hivi nani ni mshauri wa hawa watu?!

Nini wajibu wa serikali katika matukio ya aina hii?

Bajeti ya kitengo cha maafa chini ya waziri mkuu inafanya kazi gani?

Ndio maana wengine tunawafurahia sana watu kama Zitto na Lissu kwa jinsi wanavyowasema wenye mamlaka.

Watanzania amkeni hasa wale wanaodhani wapinzani wana chuki tu na hii serikali.

Kweli kama ni serikakali ya wanyonge, basi watanzania Mungu katupendelea!
 
Nani achangie hela zikajenge mnara?

Wanatumia kick ya kujenga mnara ili wapige hizo hela
 
Unataka watoe ili mzitafune rambirambi..
Dawa yenu ni kutoa majeneza na sanda tuone kama mtayataifisha na majeneza
 
Sasa nn maana ya rambi rambi? Hii serekali inataka kujiongezea mzigo wa dhambi kila siku!! 7rambirambi ni kwa ajili ya kuwafariji wafiwa hiyo ya kujenga ukuta kwani serekalini hakuna MFUKO WA MAAFA?
 
Cha ajabu zaidi watu wamefunikwa na meli wenyewe wanapita na mahedikopta juu, sasa sijui walisikia kuna wahanga wako huko angani!!!!?
 
Bwana Mkubwa, naona umefungua kinywa mapema mno. Sidhani kama watu watachanga tena. Rambirambi huliwa na wafiwa. Laiti ungelisema zitawasomesha hata mayatima walioachwa. Ni mawazo yangu tu jamani mnisamehe kwa domo kaya hili
 

Mkuu sipingi usemayo, lakini haya mambo yanazidi kushika kasi, na njia zinazokubalika zinapuuzwa. Ngoja watumie mbinu ambayo haitawaacha wananchi na vilema. Je unahitaji cdm wafanyiwe unyama kiasi gani ndio mambo yabadilike? Walitangaza kujitoa, je hao ccm walijali? Uliona wale akina Butiku na kina Warioba wakifungua mdomo kama walivyofanya kabla ya uchaguzi wa 2015? Kama wapinzani wanafanyiwa unyama na hatua hazichukuliwi kwanini wasichukue njia nyingine itakayosababisha wananchi na wengine wenye ushawishi kutaka mambo yawe sawa?

Rais anazunguka anahubiri kwamba sehemu ambayo kuna mpinzani ni mtoto wa jirani unategemea nini. Hao viongozi wenye ushawishi kwanini hawakemei hili? Sasa hivi ni jambo la kawaida kabisa kuona vyombo vya dola kuwafanyia unyama wapinzani na imegeuka ni sahihi. Sasa inabidi watu wachore mstari kwa kutumia mbinu nyingine itakayogusa jamii nzima. Nadhani umeona michango ya huo msiba mpaka sasa, yote haya ni matokeo ya huu mwenendo wa awamu hii ya tano. Narudia tena viongozi wa cdm watangaze kimachomacho kwamba umoja wetu tuliotambia haupo tena, hivyo hakuna mwanacdm kumzika mwanaccm na kinyume chake. Mkuu huyo mbunge anajua hali halisi ilivyo, ni bora huu mwenendo uwe wazi sasa kuliko kufumbia macho kisha huko mbeleni nchi yetu itumbukie kwenye machafuko.
 
Wangeenda mngesema wameenda kwenye siasa.Aibu maccm na manguo msibani aibu aibu hovyo kabisa.
 
Live TBC jioni ya leo,Kuna kauli katoa waziri uchukuzi,wakiwa na CDF,sio njema kabisa .... Shughuli inagaramiwa na serikali,vifaa nk asiwepo yeyote wa kudai malipo huduma yeyote hata cent....!!!! ....mfano mtambo kufua upepo umeletwa Jeshi!!!!....serikali mkoa na kuu tumejipanga vizuri...... Sijui lugha hii ya kibabe kaitoa wapi!!! Nijuavyo katika janga tunathamini msaada wowote kwa garama yeyote ili mradi kuokoa maisha kwanza.
 
Wakati Serikali ikisema miili 224 imeopolewa baada ya kivuko cha MV Nyerere kuzama, mbunge wa Ukerewe (Chadema) Joseph Mukundi amedai idadi ya abiria waliokuwa kwenye kivuko hicho ni zaidi ya 300.
Kivuko hicho kilizama Septemba 20, 2018 mita 50 kabla ya kutia nanga kwenye gati la Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.


Mkundi ametoa kauli hiyo leo Jumapili Septemba 23, 2018, saa chache baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kusema kuwa kivuko hicho kilikuwa kimepakia abiria 265 wakati kina uwezo wa kubeba watu 101.



Akitoa mchanganuo wa vifo, Waziri Kamwelwe amesema wanawake 126, wanaume 71, watoto wa kike 17, watoto wa kiume 10 na kufanya jumla ya maiti 224.



Akizungumza na MCL Digital leo mbunge huyo amesema kulingana na mazingira na changamoto za usafiri kati ya Bugolora na Ukara, ni wazi kuwa abiria katika kivuko hicho walikuwa zaidi ya 300.



"Hili suala niliwahi kuliwasilisha bungeni lakini kilichofanyika ni ununuzi tu wa injini mpya," amesema Mkundi.



“Serikali ina majukumu mawili, la kwanza ni kununua kivuko kikubwa na pili ni kuongeza safari za kivuko kutoka safari mbili kwa siku hadi nne ili kuzuia upakiaji wa abiria kupita kiasi.”
Mkundi amesema Ukara ni kata kubwa ambayo inahitaji siku maalum ya gulio, si wananchi wake kwenda Bugolora kila wakati kwa ajili ya kununua bidhaa.


Mbunge huyo ameungwa mkono na mwenyekiti wa kijiji cha Bwisya, Oru Magero aliyesema kuwa ni kawaida kushuhudia kivuko cha Mv Nyerere kikiwa kimepakia mizigo na abiria kupita kiasi.



"Serikali isaidie wananchi wa Ukara kuwaboreshea usafiri kama sehemu nyingine za nchi yetu," amesemaMagero.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…