Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Hadi jana around miili 40 ilikuwa haijatambuliwa na ndugu, hivyo walichimba hapo jana, sasa ndugu wamefika na kuchukua ndugu zao, makaburi yamebaki tupu leo. Japo hao wengine wataopatikana wanaweza zikwa hapo pia.
 
Wakati Serikali ikisema miili 224 imeopolewa baada ya kivuko cha MV Nyerere kuzama, mbunge wa Ukerewe (Chadema) Joseph Mukundi amedai idadi ya abiria waliokuwa kwenye kivuko hicho ni zaidi ya 300.
Kivuko hicho kilizama Septemba 20, 2018 mita 50 kabla ya kutia nanga kwenye gati la Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.

Mkundi ametoa kauli hiyo leo Jumapili Septemba 23, 2018, saa chache baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kusema kuwa kivuko hicho kilikuwa kimepakia abiria 265 wakati kina uwezo wa kubeba watu 101.

Akitoa mchanganuo wa vifo, Waziri Kamwelwe amesema wanawake 126, wanaume 71, watoto wa kike 17, watoto wa kiume 10 na kufanya jumla ya maiti 224.

Akizungumza na MCL Digital leo mbunge huyo amesema kulingana na mazingira na changamoto za usafiri kati ya Bugolora na Ukara, ni wazi kuwa abiria katika kivuko hicho walikuwa zaidi ya 300.

"Hili suala niliwahi kuliwasilisha bungeni lakini kilichofanyika ni ununuzi tu wa injini mpya," amesema Mkundi.

“Serikali ina majukumu mawili, la kwanza ni kununua kivuko kikubwa na pili ni kuongeza safari za kivuko kutoka safari mbili kwa siku hadi nne ili kuzuia upakiaji wa abiria kupita kiasi.”
Mkundi amesema Ukara ni kata kubwa ambayo inahitaji siku maalum ya gulio, si wananchi wake kwenda Bugolora kila wakati kwa ajili ya kununua bidhaa.

Mbunge huyo ameungwa mkono na mwenyekiti wa kijiji cha Bwisya, Oru Magero aliyesema kuwa ni kawaida kushuhudia kivuko cha Mv Nyerere kikiwa kimepakia mizigo na abiria kupita kiasi.

"Serikali isaidie wananchi wa Ukara kuwaboreshea usafiri kama sehemu nyingine za nchi yetu," amesemaMagero.
Ujumbe murua sana kutoka kwa mh mbunge kwa serikali yetu tukufu inayolenga kuwatetea wanyonge
 
Watu wanakiri kabisa kuwa ilikuwa kawaida kufanya uzembe ulioleta janga kama hili!
 
Serikali imesema hao 265 ndio miili iliyookolewa na kuopolewa, na uokoji/uopoji unaendelea mpaka miili yote ipatikane.

Sasa huyo mbunge ana Listi nzima ya waliokuwemo kwenye hicho kivuko.

Naona Chadema mmeanza kumlisha maneno mbunge kisa kashiriki shughuli nzima ya leo.
 
Sawa atuorozeshee majina yao
Chadema wanatafuta namna ya kumchonganisha mbunge na serikali, kitendo cha kushiriki shughuli nzima ya leo huenda uongozi Taifa haujaridhika.
 
Haya ndio tulikuwa tunayasema na sasa yanaanza kutimia!

Kwahiyo watu wasipochanga hayo hayatafanyika?

Hivi nani ni mshauri wa hawa watu?!

Nini wajibu wa serikali katika matukio ya aina hii?

Bajeti ya kitengo cha maafa chini ya waziri mkuu inafanya kazi gani?

Ndio maana wengine tunawafurahia sana watu kama Zitto na Lissu kwa jinsi wanavyowasema wenye mamlaka.

Watanzania amkeni hasa wale wanaodhani wapinzani wana chuki tu na hii serikali.

Kweli kama ni serikakali ya wanyonge, basi watanzania Mungu katupendelea!
Ulitaka iweje, kwani nani aliyekuambia mfuko wa maafa kazi yake ni kujenga mnara wa kumbukumbu! Tanzania kwani tuna wapinzani…tuna wapinga yote…aibu yao! Hao wahanga watapewa mkono wa pole!
 
Back
Top Bottom