Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kuna miili itakuwa imenasa kwenye magari na ma mizigo itapatikana kivuko kikinyanyuliwa ni suala la muda tu... yaani serikali ishabalance eti kilibeba abiria 265 waliokufa 224,waliopona 41 kwa tuliokulia ziwani na kwenye ajali km hiyo bado ni mapema kuhukumu lazima kuna miili zaidi imenasa chini
Wanasema hivyo kupunguza lawama
 
Ila tukumbuke kuwa mbunge ndie anaweza kupata taarifa kamili za watu waliokuwa ktk kivuko kuliko hata hao viongozi. Ni vyema akasikilizwa kwani taarifa nyingi anapata toka kwa wapiga kura wake.
 
Mkuu mimi sio wakupinga tu bora nimepiga kama mnavyofanya cdm. Hao watu 300 anaosema mbunge wenu, athibitishe.
Sasa kama bado wanaendelea na zoezi la kuopoa maiti atathibitishaje kabla ya zoezi kukamilika? Halafu huo ujinga wa kusema kwamba CDM wanapinga kila kitu sijui mmeutoa wapi?

CCM waliambiwa kwamba kuna hatari iko siku iko kivuko kitazama wakapinga, leo aliyewaambia ukweli ambao ndio umetokea ndio mnamwita mpingaji, nyie vipi?
 
Mkuu serikali imesema waliookolewa na kuopolewa jumla ni 265 na imesema inaendelea kutafuta miili mingine mpaka yote ipatikane kwa maana hiyo inaweza kufika 300 na ama zaidi.

Na mbunge amesema walikuwa zaidi ya abiria miatatu, japo sina hakika na takwimu zake.

Lakini ukiangalia kauli zote mbili hazipingani.....

Ila chadema wanaripotiwa kama mbunge na serikali wanapingana...
Kukosa akili hata ktk mambo kama haya ni mbaya sana, ni bora ungekaa kimya kufucha upumbavu wako. Serikali ilichotangaza ni kile walichokiona, miili iliyopatikana plus waliookolewa. Mbunge anasema watu ni wengi zaidi ya hao na taarifa anapata kwa watu waliopotelewa na ndugu zao pia bado kivuko bado kipo ktk maji na huenda miili zaidi ipo huko.. hebu tumia akili kdg tu ulizojaaliwa kufikiri!
 
Jimbo la Ukerewa lipo chini ya CDM ila ndani ya CDM kuna ubaguzi wa kijinga sana. Na uhakika hili balaa lingetokea Arusha au Kilimanjaro CDM makao makuu wangetuma mtu wa kuwawakilisha kwenye msiba.
Mkuu siyo kutuma mtu wa kuwakilisha, ni kwamba Makao Makuu yote ingehamia huko.
 
Ila tukumbuke kuwa mbunge ndie anaweza kupata taarifa kamili za watu waliokuwa ktk kivuko kuliko hata hao viongozi. Ni vyema akasikilizwa kwani taarifa nyingi anapata toka kwa wapiga kura wake.
Kuna impact yoyote kama waliobebwa sio idadi iliyotajwa na waziri bali ni 300 idadi inayotajwa na mbunge?
 
Kwani ile michango ya Msiba wa Mbwa wa Nassari mliiipeleka wapi mkuuu, hebu leta mchanganuo basi.
Yaani unachanganya mambo kabisa. Mbwa wa Nasari ni mambo binafsi wakati kuzama kwa kivuko ni suala la watanzania wote!
 
Kivuko kimepinduka mita 50 kabla ya kutia nanga kwenye gati.
Lakini mmeshindwa kuwaokoa.ujue ni karibu sana na nchi kavu.kama wangewahi mapema wengi wangepona.je kingepinduka katikati ya ziwa ingekuwaje.
 
Mtoa taarifa wa serikali na mtoa taarifa wa CDm naona wanachuki binafsi.
 
Back
Top Bottom