Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Wapinzani wataendelea kuikosoa na kuielimisha Serekali ila kiburi cha serikali ya Ccm mavuno yake ndio hayo.Hela wanazotumia kununua Wapinzani zingeweza kununua vivuko hata viwili.
Kwa nini hao wapinzani wananunulika? Hivi umejifunika kitambaa cheusi usoni huoni kuwa hili ni tatizo pia?
 
Subiri tume itakuja na majibu. Utapata majibu ya kwanini kimezama, mbunge ameongea sababu nyingine na ajali imeletwa na sababu tofauti.
Wewe Sababu ya ajali umeijuaje kama unasema tusubiri tume tupate majibu kwa nini kivuko kimezama?
 
Nimejiuliza sana ili swali hasa baada ya kusoma katika gazeti la Chadema liitwalo Tanzania Daima kwamba uongozi unakaribia kumsajili maalim Seif katika chama chao. Ndiposa najiuliza mgombea urais mtarajiwa ndio kipaumbele cha Chadema kiasi cha kumtelekeza mbunge wa Ukerewe my Joseph Mkundi?!!!
Rais amewakataza kutafuta kiki za kisiasa. Au ulidhani anaongelea upande mmoja tu?
 
Kwa kweli hili swala lina ukakasi sana. Kwanza majeneza tu ya wafiwa yalikuwa ni aibu!. Kweli kama serikali ilishindwa nini basi hata kuchonga au kununua majeneza at lest yenye hadhi!!? Mpaka wawahifadhi marehemu kwenye masanduku yaliyo midhili ya tool boxes" za mafundi gereji!!?
Halafu bado tena rambi rambi waipangie matumizi!??.

Pia sijui kama hata wafiwa waliochukua miili ya ndugu zao wamepewa hata ka nauli cha kuisafirisha!!?.

Serikali ya awamu ya 5 ibadilike kwa kweli. Haya mambo yanatuaibisha watanazania wote kwa ujumla.
 
Sasa nn maana ya rambi rambi? Hii serekali inataka kujiongezea mzigo wa dhambi kila siku!! 7rambirambi ni kwa ajili ya kuwafariji wafiwa hiyo ya kujenga ukuta kwani serekalini hakuna MFUKO WA MAAFA?
Wanataka kurudia yale yale ya luck vicent. Watafanya wananchi waogope kuchangia maana wameshasema hela huwa zinaenda wapi.
 
Kukamata mitambo ya gongo zinatumika helikopta!
Kamati ya ulinzi inatumia mtumbwi kufika eneo la ajali ikae kutoa maamuzi ya kuomba msaada!
Maji mnayataka yapige pause kusubiri likamati lenu la kisiasa linalotumika kudhibiti upinzani?

Hii kamati ingeweza ikafanya kikao kwa Skype ikapitisha angalau azimio la kuomba msaada haraka.
Tungeokoa maisha.
Kichwacho kimejazwa makamasi usitegemee kuwaza kitu kizuri isipokuwa makamasi.
jogi, huyajui maji
 
Mnara wa kumbukumbu ni sehemu ya heshima kwa marehemu na faraja kwa ndugu
Mnara unawafariji vip.wanandugu? Mzee wako akifariki tukimjengengea mnara nyumbani utasaidia nn?
Ni vyema hizo fedha zingeelekezwa kwa familia husika maana kuna mayatima na wajane zikawasaidie kusongesha gurudumu la maisha.
 
Kuokoa watu mpakaa Kamati iundwe,!??? mama...eee zaoo kabisa wapuuzii walee...yanii yanatia hasiraa balaaa
"rikiboy, wapi umesikia kamati iliundwa? kamati ya ulinzi na usalama ipo siku zote
 
Sasa wewe hiyo subiri kivuko kiinuliwe utaona maajabu yake, kunaweza kuwa na watu mia moja na ushee wamekwama ndani, mark my word! Kuna tukio la kustaajabisha zaidi linakuja baada ya kivuko kubinuliwa.
Kwa hiyo unataka usemeje?? Acha ujuaji..watu wameingia chini wametafuta..unadhani wangewaacha tu kama wameonekana..au wangekuwa na nia mbaya si wangeacha hicho kivuko hata mwezi..
 
Ulitaka iweje, kwani nani aliyekuambia mfuko wa maafa kazi yake ni kujenga mnara wa kumbukumbu! Tanzania kwani tuna wapinzani…tuna wapinga yote…aibu yao! Hao wahanga watapewa mkono wa pole!
Sidhani kama wapinzani wanaingia kwenye hii mada maana mheshimiwa rais alishasema msiba huu usiwe uwanja wa siasa.
Nafikiri anachohoji mtoa post kwann hiyo pesa ya mchango isiwafikie walengwa direct instea ya kujenga mnara?
 
mtanzania-dondosha-magazeti.jpg
 
Back
Top Bottom