Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Inasemekana kivuko cha watu 100 kilikuwa na watu zaidi ya 400,hakuna takwimu sahihi kwa chombo nyeti kinachobeba maisha ya watu.
Waafrika bado tuna safari ndefu sana
Madhara ya sheria mpya ya takwimu... Tusubiri wenye mkono wao waje na takwimu
 

Mkuu, zoezi la uokoaji wa miili au watu waliozama na meli au chombo kingine cha majini, mosi, linahusisha kuzama ndani ya maji (diving) kuitafuta miili na pili kuwatafuta kwenye sura ya maji (water surface). Hoja ulizozieleza hapo juu zinakua na mashiko pale tu ambapo zoezi la uokoaji lingekua linahusisha kusafiri kwenye uso wa maji pekee na kukusanya miili inayoelea na kuokoa wahanga wanaotapatapa hapo.

Kuvua samaki na doria (kama ulivyojaribu kurejea kwenye mfano wako hapo juu) ni shughuli zinazofanyika ama juu ya maji au kutokea juu ya maji (unatupia nyavu majini ukiwa juu) hivyo yanaweza kufanyika 24hrs tena hata kwa teknolojia duni kabisa maana unahitaji kumulika juu ya uso wa maji tu.

NB: Sijasema haiwezekani kabisa kufanya uokozi hadi usiku, la hasha, bali nimesema kwa TEKNOLOJIA YA NJIA ZETU TUNAZOZITUMIA KUOKOA, jana tusingeweza kuokoa hadi usiku (giza ni kikwazo), vinginevyo tutawapoteza waokoaji.
 
Write your reply...idadi ya vifo itashangaza dunia kama watawatoa wote maana nyomi iliyobebwa ni kubwa kuliko mnavyodhan mi nilikuwa mnadan bugolola asubuh ilishusha watu wengi zaidi ya 200
 
Nimesema wote waliohusika kusitisha zoezi hata hao wataalamu waliomshauri watasema nini kilishindikana.

Halafu si kila unaloshauriwa lazima ukubali, kama kiongozi unatakiwa ujiongeze uchanganye na zako.
 
Serikali itakwepaje hapo, serikali ina vyombo vyake vya kudhibiti usafiri na usafishaji wa nchi kavu na majini, kuna Sumatra, Msimamizi wa bandari, polisi wa doria wote hao ni serikali walishindwa kujua kuwa kivuko kumezidisha abiria.
Mkuu hiyo nilisema kinyume chake, kuna mambo mengine yanatia hasira sana, afu ukute kuna na askari wa jkt wasimamia ulinzi km kigamboni
 
Wakati wa uchaguzi RC yupo radhi kukesha akizunguka kulinda vituo usiku kucha ili wakala wa Chadema asiingie kituoni mapema ila kuokoa wananchi anakwenda kulala kwanza.
bora basi kama alienda kulala, usishangae ukija skia alikuwa bar ama kwa kimada, kama sio alikuwa busy kubet mechi za uropa!
 
Hii kitu nimejiuliza sana, nilitaka kuanzisha uzi ahsante umenisaidia mkuu. Nimewaza au lile tukio la kuzama nalo limeweka "pause" nalo linasubiri kupambazuke ndo liendelee?

Zile Boats zao za Patrol si zina mataa makubwa? Kwanin wasingetumia hizo kukesha eneo la tukio wakiopoa? Hivi aliwtoa hii kauli angekua na ndugu yake hamuoni pale angesitisha kweli?

Huyu aliesema hivi anasubiri nini kuachia ofisi?
 
Kusema ukweli ile kauli haikupaswa kutamkwa na kiongozi wa umma...ambaye mshahara wake na malupu lupu yake vinategemea kodi za umma!!!...

..inawezekana siyo uamuzi wa Mkuu wa Mkoa, bali wa wahusika wa vikosi vya uokoaji.

..kama waokoaji hawana vifaa vya kufanya kazi usiku[ktk giza], Mkuu wa Mkoa atakuwa anahatarisha maisha ya waokoaji ikiwa atawalazimisha kufanya kazi ktk mazingira hayo.

..Ni kweli kauli ya Mkuu wa Mkoa inatia hasira. Lakini lazima tutambue kwamba Tz kama nchi hatuna weledi na masuala ya uokoaji.

..Masuala ya utayari wa nchi ktk masuala ya uokoaji wanapaswa kuulizwa mawaziri wenye dhamana na vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na watendaji wao.

Cc Nguruvi3
 
NB: Sijasema haiwezekani kabisa kufanya uokozi hadi usiku, la hasha, bali nimesema kwa TEKNOLOJIA YA NJIA ZETU TUNAZOZITUMIA KUOKOA, jana tusingeweza kuokoa hadi usiku (giza ni kikwazo), vinginevyo tutawapoteza waokoaji.
Mkuu na hiki ndiyo watu wanachojadili, Ni kwanini hadi sasa pamoja na Majanga ya 1996Mv Bukoba, Zanzibar.. nk mpaka Leo hatuna uwezo wa kuokoa Gizani?
Tuko salama kiasi gani?
 
Polen wote walioguswa na msiba, tunawaombea manusura wote wapone na waokoaji wafanye kazi yao vyema,

Mungu ibariki tanzania...
 
Nimemskia mmoja wa viongozi wetu wanoishi kwa kodi zetu, akihojiwa na BBC Leo asubuhi kwamba kwanini walisitisha uokoaji. Utumbo aliojibu ndo ulio nichosha.


Kwamba, waaliingia kwenye meli na kujiridhisha kwamba hakuna alie hai ambae anahitaji msaada, isitoshe pia waokoaji walikuwa wamechoka kutokana wanatumia mitumbwi kubeba maiti hivyo tukaamua kusitisha uokoaji mpaka kesho.

Huu uongozi wa awamu hii naona kila mtu kichaaa.
 
!
!
Niliona Picha Kikiwa Juu Chini Chini Juu, Nikamuwaza Yule Mpumbavu Aliitoboaga MV Bukoba Ikazama Mazima. Wamzuie Akijitokeza Tena.
yule mpumbavu hivi alikuwa ni mwanajeshi au mfanyakazi wa hao wajinga temesa au alikuwa mvuvi tu aliyejiongeza?ila ujue kuna marine kabisa wanalipwa mishahara kuhusu mambo ya uokoaji.

Na wapo.
 
So sad aisee, mkuu ngoja kwanza tuoge maji moto na kunywa chai nzito ya maziwa si unajua tena siyo shughuli ndogo
 
Juzi jiwe si alipoga sana kelele kuhusu kukata tiketi akasema ziwe za umeme?
Inamaana yule mshkaji alifharau?
Inakuwaje hawajui kilibeba watu wangapia.
 
Kwahiyo maiti haina thamani? mtu hata akifia shimo la choo lazima atolewe azikwe kwa heshima, huwezi kumuacha ndani au kulifukia shimo kwa vile tayari ameshakufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…