Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Hivi kweli mkuu wa mkoa anasitisha zoezi la uokoaji kisa giza!? Mkoa mzima hakuna uwezo wa kuweka taa ili kuruhusu uokoaji very sad! Hata kutengeneza umeme wa muda ili kumudu mazingira ya wakati huo tumeshindwa!?
Hivi usiku umekuja ghafla sana mpaka kusitisha zoezi?
Kwa hali hii kama kuna siku ajali itatokea saa 19:00 jion na hujui kuongelea basi nimekufa, yaan jua liwake!!!?
Watazania tubadilike kila mmoja kwa nafasi yake.
Sababu zinaweza kuwa:
1. Uwezo wa kuwaza nje ya box (zaidi kutoka kwa viongozi)ni mdogo= viongozi wajinga.
2. Uwezo wa waokoaji ktk hali ngumu zozote ni mdogo= wanajeshi dhaifu
3. Uoga wa waokoaji ktk mazingira magumu ya giza=wanajeshi waoga.
4. Viongozi kutojali uhai/maisha ya watu= viongozi kujali business zao.
* hakika viongozi/ watawala wanaohusika na hili inabidi wawajibishwe mara moja kwa kauli za kizembe kama hizo.
 
Andiko hili linazidi kunitonesha sana, Nchini Kenya vyombo vya habari vimeripoti habari hizi haraka sana na kusitisha baadhi ya ratiba zao Mfano MILELE FM ya Kenya, TBC wako bize na kipindi cha miziki cha ZINAZO KIKI, inauma sana RC anaongezea kwa kusitisha zoezi kuwa GIZA limeingia. MTU aliyelelewa kwenye utamaduni wa KITANZANIA unapata wapi ujasiri wa kuingia kitandani ukalala wakati Wanadamu wenzako wawe maiti au hai unajua wako majini? Zaidi we ni kiongizi kwenye dhamana ndani ya mkoa. Kama Mh Rais aliwahi kukiri kuwa huwa anafanaya kazi hadi usiku kucha sasa wewe RC ujasiri huo wa kusitisha kuopoa maiti au watu hai ukaenda kumkumbatia mkeo unatoka wapi.
Labda ingekua kimezamia kwao ndo angeona hali hiyo hawezi kulala
 
Hivi RC, Msimamizi wa bandari Mwanza, RPC, DC, Kiongozi wa Zimamoto leo walipata usingizi kweli? huku roho za Watanzania zikiteketea ziwani? I cant imagine uongozi wa dizaini hii, na utasikia hakuna atakayewajibika.


Mkuu walilala sana, tatizo lao sio wananchi sana bali kipaombele chao ni ccm kutangazwa washindi wa uchaguzi. Ingekuwa ni kupambana ccm itangazwe washindi usiku, hao wote uliowataja wasingeondoka eneo la tukio.
 
kwahyo wewe ulitaka atoe jibu gani kwa mfano?

waokoaji wameingia kwenye kivuko wakajiridhisha hakuna aliye hai.. na zoezi likabadilika kutoka uokoaji kuwa uopoaji

kuendelea na zoezi ilikuwa ni kuhatarisha usalama wa hao waopoaji .. sidhani kama kungekuwa na watu walio hai ndni ya kivuko zoezi lingesitishwa sema tu lisitishwa kwa sababu wanejiridhisha hakuna akiye hai

sema kuna watu mnajifanya mnajua kuongea na kuongoza nchi wakati hata familia ya kuiongoza bado hujaipata..

embu basi sema ulitaka waendelee kutoa maiti hadi usiku wa manane? unajua changamoto za uokoaji majini?
 
Tuna helkopta zinaruka juu kulinda wateule,nchi jirani zina vifaa kedekede mf. Kenya. In a matter of hour or two, watakuwa wamefika site!! Kipindi cha Mkapa na MV Bukoba, kuna kikosi kilitoka Zenj na SA walifanya kazi day& night. Nashauri, pamoja na juhudi zote, tusitangulize visingizio vya giza!! Tuongeze juhudi na tuimarishe mahusiano mema na majirani zetu ili tunakotindikiwa tupate msaada. Mungu weka mkono wako katika hili.

Mimi hoja yangu imejikita kwenye usahihi wa kusitisha zoezi siku ya jana kwa sababu ya giza, na nikaeleza kwamba ilikua ni sawa kufanya vile kutokana na njia ambazo zilikua zinatumika. Na ili zoezi lisiendelee "kulala" ni lazima tu "improve the methods" ili ziwe fanisi na salama kwa waokoaji hasa wakati huo wa usiku na tuwaotoe ndugu zetu (hai au la) kule chini. Na mapendekezo uliyoyatoa hapo juu ni ya msingi kabisa ili kufanikisha zoezi zima. Kwa sababu yoyote ile, kwa uzembe au makosa ya mtu yeyote yule, kama njia za uokozi zilizokua zikiendelea kutumika hazikua salama na fanisi hiyo jana usiku, ilikua sahihi kusitisha zoezi lile hadi asubuhi. Suala la kwanini bado tunatumia njia "za kizamani" kufanya uokozi ni suala jingine (with respect to maamuzi ya jana)
 
Asiye sikia la mkuu huvunjika guu hawa wahenga walikuwa magenius.
 
kwani wamekufa watu wangapi hadi sasa kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika? Nimesoma skynews wanasema zaidi ya 200 wanahofiwa kufa.
Ila nilichojifunza
1:Wapinzani wasipuuzwe na wanatakiwa kuwepo ili wasaidie kuonyesha hatari ambazo zisingesemwa vizuri na CCM. Mbunge alionya kuwa haya yatatokea.
2:Nilitegemea Tangu MV BK izame tungekuwa na Disaster management plan ya uhakika humo ziwani. Nashangaa kuona watu wanaokolewa na mitumbwi na sio Boti za uhakika za uokoaji.
3: Kwa jinsi ilivyozama nakubaliana na huyo mkuu kupona mtu pale ni asilimia ndogo, ila excuse ya uchovu sijawahi kuisikia popote duniani.

Tujitahidi kutoa taarifa zenye faraja kwa Umma. Kusema tutaendelea kesho hata dunia inayofuatilia tukio hili inatuona hatujali watu wetu.
Maoni
 
Kwa kauli aliyotoa jana RC nimeamua tu nikae kimya mana sina neno zaidi ya matusi ya nguoni kwa viongozi wote, acha tu maumivu ya kauli hiyo nikae nayo moyoni. Yani miili ya binadamu wnzako unahalalisha iwe chakula cha samaki??
 
mkeo akiwa leba tu hulali sembuse ndugu yako kulaliwa na meli kwenye maji? tuna shida na huu uongozi wa sasa. mtaelewa tu maana muda huwa hauna ghilba.

Mkuu, tatizo linaanzia kwenye uwezo wetu wa kufanya uokozi, si suala la nani amelaliwa na meli kule. Naona kama unajaribu kutuaminisha kwamba kwa siku ya jana kulikua na uwezekano wa kuendelea kufanya uokozi hadi usiku (bila kuathiri usalama wa waokoaji) lakini roho mbaya na kutokujali kwa viongozi ndio wakaamua kusitisha zoezi. Haya yanaweza kuwa si mawazo mema sana mkuu.
 
Mkuu ninajitahidi sana kuepusha malumbano na wewe , kwa hili naomba kwanza usome habari nii [Habari ipo mwanzoni kabisa mwa bandiko, sijaitafuta mahali na wala sijasema imetoka mamlaka yoyote.

Nilichofanya ni kuangalia uhalisia wa mtoa taarifa hiyo

Nikasema hivi, kituko kina uwezo wa tani 25 kwa mujibu wa mtoa mada hapo juu
Kina uwezo wa kuchukua watu 100 na magari 3, kwa mujibu wa mtoa taarifa hapo juu

Kisha nikafanya tathmini yangu kwa kutumia namba hizo.
Nikasema hivi, tukifanya assumptions ya wastani wa uzito wa abiria ni kilo 70, kwa abiria 100 ni sawa na kilo 7,000 au tani 7

Kisha nikauliza, magari 3 yenye uzito gani? Kwa maana kuwa uzito wa saloon, Van, truck n.k. vinatofautiana.

Kisha nikasema tufanye assumption ya tani 4 kwa magari 3 ni sawa na tani 12
Ukijumlisha ni sawa na 7+12 ambazo ni tani 19, chini ya tani 25
Kwahiyo kwa namba alizoweka mleta mada suala la uzito kuwa mkubwa, kwa mujibu wa mleta taarifa haliwezekani. Hapo ndipo asili ya neno haiwezekani

Unatakiwa usome bila prejudice na uelewe nini kinazungumziwa.

Nasema prejudice kwa sababu hii uliyoandika hapa Wapi kuna siasa katika hayo niliyoeleza hapo juu? Kama tathmini yangu kwa mleta mada si sahihi mambo unayosema yanaingiaje?

Unaposema ninahujumu usijui una maana gani kwasababu hakuna mahali nimesema lolote kuhusu serikali au mamlaka yoyote na namba hizo zilizowekwa na mleta mada
Nilichofanya ni kumjibu mleta mada

Nia na dhamira yako si nzuri hasa unaposema kuna lengo la kuchonganisha serikali na wananchi au malengo maalumu. Kwakweli umenisikiisha sana kwa haya

Unajaribu kueleza kitu ambacho hakipo lakini kwa prejudice yako juu yangu unachomeka ieleweke hivyo, ulichofanya ni kuchukua maneno yangu out of contents and context just to suit you ill intention against me. Na sijui chuki hii inaletwa na nini hasa

Kwa mtu asiyefuatilia au kusoma kwa details kauli zako ni za hatari sana

Mkuu unatambua kwa muda mrefu nimejiepusha na mijadala na wewe, kwa hili naomba radhi kukujibu nimelazimika kutokana na kauli zako zenye nia mbaya sana

Kama una reservations nyingine it's ok usitumie hili ku infiltrate hoja zako ili ionekane ni mtu mbaya sana. Nadhani utafurahi sana nikapatwa na majanga yoyote yale
Hivi vivuko huwa vinajaza mpaka inasikitisha!
Usifikiri hao watu wako kama wewe na kuchukua tahadhari! NO WAY!
Mara nyingine unaona kabisa watu wanafanya mambo na ni completely suicidal act!
Kama wanavyo panda mshikaki kwenye bodaboda au pickup kwa Nyuma!
Mambo mengine huwa yanabadilika kwa wakati wake, lakini kuinyoshea kidole Serikali ni kutafuta LAANA KUTOKA KWA MAMA TANZANIA walahi!
Be realistic kijana mdogo ehhh jamani!
That’s all
 
Hivi vivuko huwa vinajaza mpaka inasikitisha!
Usifikiri hao watu wako kama wewe na kuchukua tahadhari! NO WAY!
Mara nyingine unaona kabisa watu wanafanya mambo na ni completely suicidal act!
Kama wanavyo panda mshikaki kwenye bodaboda au pickup kwa Nyuma!
Mambo mengine huwa yanabadilika kwa wakati wake, lakini kuinyoshea kidole Serikali ni kutafuta LAANA KUTOKA KWA MAMA TANZANIA walahi!
Be realistic kijana mdogo ehhh jamani!
That’s all
 
Waliopo eneo la tukio wanasema sio zaid ya 100m
So kilikuwa kimekaribia sana kufika mwisho ?, lakini haya matukio yamekuwa yakijirudia rudia sana, (kumbuka MV bukoba, na kule mto kilombero) mpaka jana saa 2 usiku walikuwa hawajajua ni watu wangapi waikuwemo ndani ya kivuko, yaani wasimamizi wanashindilia watu as if ni mizigo, Tutafakari.
 
Hakuna Cha ajabu katika Awamu hi,

Si munakumbuka hate tetemeko la kagera rais mwenyewe kwa kinywa chake alitamuka kwamba hakuahidi kuketa tetemeko katika ahadi zake

Kwahiyo naamini hata hii ajali hakuiahidi
 
hawa tutawalaumu bure niliwahi kumsikia Mbunge wao akiomba Engine Mbili mpya za kufungwa kwenye hicho kivuko maana zilizopo zinazima Mara kwa Mara na walilipotezea wakati abiria wanalipia ila kuweka mazingira ya usalama wao yapo chini kabisa
kivuko sijaona hata maboya yakielea kwa ajili ya kusaidia abiria waliomwagwa...
 
So kilikuwa kimekaribia sana kufika mwisho ?, lakini haya matukio yamekuwa yakijirudia rudia sana, (kumbuka MV bukoba, na kule mto kilombero) mpaka jana saa 2 usiku walikuwa hawajajua ni watu wangapi waikuwemo ndani ya kivuko, yaani wasimamizi wanashindilia watu as if ni mizigo, Tutafakari.
Ndio kilikuwa kimekaribia kabisa kufika, tayari abiria walikuwa wamejiandaa kuteremka
 
Tushukuru nchi yetu haipatwi na majanga makubwa na ya kutisha kulinganisha na nchi zingine zinazopigwa na mafuriko, matetemeko na vimbunga vya hatari. Bado hatujawa tayari na ukabilianaji wa majanga na uokoaji.
 
Back
Top Bottom