Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Asante mkuu.
Unaona fahari kabisa kusema kwamba nchi haina vifaa vya uokozi na watu wetu hawana ujuzi??

Yale magari makubwa kubwa wanayoyanunua kwa mapesa mengi kwanini angalau wasiyatumie hayo mapesa kununua mawani zenye tochi?? (angalau mawani zenye tochi tu)

Uokozi wa jana ulikuwa ni kituko!! Sijui ni mitumbwi ile??
 
Pumba
 
Nimesema wote waliohusika kusitisha zoezi hata hao wataalamu waliomshauri watasema nini kilishindikana.

Halafu si kila unaloshauriwa lazima ukubali, kama kiongozi unatakiwa ujiongeze uchanganye na zako.
Anachanganyaje za kwake?anaanza kuzama nao ktk maji kuokoa wahanga?
 
poleni sana wafiwa wa ukara na bugolola,,, na mabilioni yanayotumika kwenye marudio na pesa zinazipotea bure matrilioni zingeboresha usafiri kanda ya ziwa.shida raia wanachojua ni kupiga makofi na kuvaa kofia na tshirts wanajisaau sana kwamba hawana usafiri wa uhakika miaka yote hii kuvuka tu sengerema vivuko navyo ni tatizo zito badala kukomaa nao.serikali hii ni sikivu najua mjomba hatapenda tena kuskia ndugu zake wanaangaika na vivuko tena tunamwamini sana na kwa hili atapambana kulinda raia wake wa kanda ya ziwa,sijawaelewa uyo mkuu wa mkoa hawakuwa na plan B giza likiingia si inajulikana tu giza litakuja?unasitisha uokozi wafe wengi zaidi na mbinu zipo nyingi tu?au vifaa hakuna si waseme ivo kuliko huu &*%##%^** waliousema ni maajabu ya 8 haya
 
Aliye hai anaokolewa.
Aliyekufa anaopolewa.
Kwa vile walijiridhisha kwamba waliobaki ndani ya feri wote walikuwa wamefariki, ni sahihi kusitisha uokoaji kisha wajipange kwa ajili ya uopoaji!
 
Kivuko kilishatengenezwa Boss. Hakina hata mwezi toka kitoke matengenezo. Hivyo tatizo sio mechanics za kivuko.
 
ila ukumbuke kinachofanyika hapo siyo uokoaji... ni uopoaji wa miili nahisi sidhani kama ningesema niliyoyasema kama bado kungekuwa na zoezi la uokoaji... wamejiridhisha hakuna aliye hai ndio maana wakahairisha zoezi hadi siku inayofuata (hakuna aliye hai) pointi yangu ipo hapo
 
"Hekima, Umojaa na Amanii, hiizi ni ngao zetu!. Tanzania na watu wakee!"

Kuna mtu mahali kausaliti huu mstari.
 
Majibu kama haya yanatakiwa yatolewe na mtu mpumbavu kabisa...!
 
Huyu nae hata hajui anachokiongea. Sasa kama wamejiridhisha hakuna aliye hai, huo "uokoaji" anaosema utaendelea kesho ni wa kumuokoa nani?
Mi niliwahi kusema, maisha ya Mtanzania hayana thamani yoyote. Yaani tunaishi kibahati bahati tu ilimradi siku ziende. Ingekua nchi nyingine watu wangekesha hapo mpaka wahakikishe miili yote inayoweza kutolewa imetolewa. Na ninavyowajua watanzania hawataanza uokoaji alfajiri kama wanavyosema.. hapo ni saa tatu au saa nne maanake mpaka watu waamke, wanywe chai waanze kujiandaa na kuweka mchakato wa uokozi, wapite kuona kama vifaa vimefika.. zoezi litaanza saa sita..
 
Dah kum****
 
umekurupuka kuqoute

kwanza tafuta tofauti ya uokoaji wa maisha na uopoaji wa miili ndiyo uje kuniquote tena

unaweza risk maisha ya walio hai katika kuokoa maisha ya walio hatarini

lakini kamwe huwezi risk maisha ya walio hai katika uopoaji wa miili iliyokwisha poteza uhai utasubiri mpaka mazingira yatakapokuwa rafiki ndio uendelee na zoezi

EMPTY SET
 
uwa wanazuiwa aseee umesahau lile tukio la daladala iliyopitiliza na kuzama kule kigongo ferry??wanainchi wanaojua kuogelea walizuiwa kabisa na waliomba wajitokeze wakaokoe watu wakawa hao wenyewe temesa sijui nini na walizidiwa. na hapo si mbali kabisa kwa watu wa kanda ya ziwa wanaojua kuogelea wengi wao,pia ona iyo mitumbwi ya wavuvi sasa lazima wasitize zoezi usiku hakuna hata boti lenye taa ili kuendelea na zoezi,pia shida ingine kubwa ni MABOYA YA UOKOZI jamani yanafungiwa kwenye grill na zinga la komeo na hamna shoka lililo karibu useme wakati kinapinduka mmoja aliekua hajataharuki agonge komeo atoe maboya..sielewi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…