Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Pole sana Kwa wafiwa,kama kweli chanzo ni kuzidisha mzigo wahusika nadhani watawajibika
 
Bado kunhitajika data zaidi ili kujibu swali lako. Huenda hayo magari matatu yalikuwa malori mawili yenye uzito wa tani 15 kila moja
 
POLE HAISAIDII tufanye mikakati ya kuwaokoa na kutoa elimu kwa majanga kama haya
 
Ukerewe island and ukara island viewed on map
 
Usipopigwa ban na hii kauli yako basi nitaamini kabisa wakina Maxence Melo wote ni chadema. Hii sio kauli ya kuitoa wewe mtoto wa kiume mwwnye akili na utashi wako. Pole sana mkuu.
kaka tupo kwenye majonzi siasa za nini hapa, chadema imefikaje
 
Poleni sote watanzania. Pole kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
 
Mkuu ningependa mjua huyu engineer tafadhali?
 
Mkuu najaribu waza kwa sauti kwa utawala huu mkuu wako akitoa order hata kama ni ya hovyo huna Budi kutekeleza hivo naanza hisi kabisa kuna uwezekano haya maamuzi yakipuuzi yalitolewa Na mkubwa Fulani wengine wote wakaitikia japo ni jambo la kipumbavu Na aibu kubwa......
Ni juzi tu tumeona Thailand ilivyopigania maisha ya wale watoto waokoaji hawakulala usiku Na mchana walipiga Kambi pale mpaka walipo fanikiwa Sasa apa kwetu hili limechafua sana taifa
 
HIVI UNAPOSEMA KUWA ZOEZI LA UOKAJI LIMESITISHWA MPAKA KESHO KWA SABABU YA GIZA KUINGIA HUKU WATU WAKIWA WANAPIGANIA UHAI WAO CHINI YA KIVUKO KWENYE MAJI UNATEGEMEA NINI? SIJAWAHI KUONA MKUU WA MKOA BOGASI KAMA MONGELLA AISEE.DAH SHAME UPON HIM KUMBE NILIVYOAMBIWA KUWA YEYE NA MZEE JIWE WANAPISHANA MPAKA IKAFIKIA MZEE KUMTIMUA KWENYE NYUMBA YA MKUU WA MKOA AKAKAE URAIANI LEO NDIO NAAMINI.ANGEKUWA MAKONDA NDIO MKUU WA MKOA WA MWANZA AISEE WATU KARIBIA WOTE WANGEEZA KUOKOLEWA NA TENA WAKIWA HAI KABISA.MONGELLA EBU JIWAJIBISHE KABLA TINGATINGA HALIJAKUKUMBA.
 
Dah hii nchi ni ngumu sana.
"Et mkata tiketi alizama kwenye maji pamoja ma mashine aliyokatia tiketi kwahio hatuwezi kujua idadi kamili iliyokuwemo kwenye kivuko"
daah ni kweli mkuu nilikuwa ukerewe mwezi wa 6 nikavuka ukerewe kivuko cha rugezi kwenda kisorya ya bunda, nilishangaa kuona yule kaka aliyenikatia ticket ukerewe na ndio huyo huyo anakata ticket kisorya kurudi ukerewe, mkataji ticket ana mashine kama ya efd au maxi malipo kufika kisorya ni huyo huyo anakatisha kwani tulivuka nae, nikashangaa, lakini hiyo sio sababu kwani efd au maxi malipo si ipo networked, hivyo waliokata ticket tunaweza tukawajua vile vile idadi yao
 
mkuu samahani sana kama utakuwa umenielewa vibaya.... hizi uzi mods wameziunganisha mimi hyo coment sikutoa kwenye uzi huu niliitoa kwenye uzi mwingine kabisa ambao hayo maelezo yangu yalikuwa yanaingia
 
Yeyote aliyehusika kuruhusu ubebaji huo wa abiria awajibishwe.
Red: Wakazi wa kigamboni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…