Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Hili ni janga.
Alafu meli inazama mita 100 toka ktk gati? Huu ni uzembe wa hali ya juu kwa timu ya uokoaji kushindwa kuokoa idadi kubwa ya watu.
 
TANZANIA TUNASAHAU HARAKA SANA, BAADA YA MIAKA KADHAA UTASIKIA KIVUKO KINGINE KIMEZIDISHA TENA MIZIGO NA WATU.
 
Huu ni msiba mkubwa sana na nafikiri ktk awamu hii ndo wa kwanza mkubwa kabisa! Nategemea kumuona Rais wetu mpendwa na makamu wake na ikiwezekana na waziri husika wawe Mwanza kujionea wenyewe ikiwemo kuwawajibisha wahusika wote ikiwezekana na mkuu wa Mkoa kuwekwa pembeni!
Mi nasapoti. Rais ajiuzulu, aiwezekani watu wengi wafe hivyo halafu na Rais yupo
 
yule mpumbavu hivi alikuwa ni mwanajeshi au mfanyakazi wa hao wajinga temesa au alikuwa mvuvi tu aliyejiongeza?ila ujue kuna marine kabisa wanalipwa mishahara kuhusu mambo ya uokoaji.

Na wapo.

!
!
Yule Jamaa Alifanya Jambo La Kijinga Mno Aisee. Hawa Wanalipwa Kuvunja Matofali Kwa Kichwa Ila Shughuli Hakuna. Kungekuwaga Na Vita Vya Kirafiki Tungejipima
 
Nategemea kusikia naodha naye amefariki maana nasikia naodha lazima awe mtu wa mwisho kutoka chomboni.

Sasa mpk watu wote hao wamekufa nategemea naye amefariki otherwise ajibu maswali yote yatakayo husisha kuzama kwa kivuko hiki.
 
Nimesikitishwa sana na taarifa ya mkuu wa mkoa wa Mwanza akisema eti zoezi la uokoaji wa maiti na wahanga wa ajali ya kivuko cha MV Nyerere ihairishwe kwa sababu ya giza.
Najaribu kuwaza mpaka miaka hii na karne hii ambayo sayansi na technology ni kubwa lakini bado Giza linakuwa ni changamoto kwa nchi ya Tanzania.

Kupitia matangazo ya DW,wanasema mpaka jana saa mbili usiku walikuwa wakisikia milio ya watu wakingonga gonga kwa ndani kuashiria kuwa bado wapo hai.
Hii ina maana kama zoezi la uokoaji lingekuwa linaendelea hadi usiku huenda na wao wangeokolewa.

Kuna mbunge wa upinzani alishawahi kutoa tahadhari lakini haikupewa uzito wa juu.Hii tabia ya kupuuza puuza itaendelea mpaka lini?

Anyway,Wapunzike kwa Amani
 
poleni sana! uzembe umehusika watu wangeweza kuokolewa 50mita sio mbali
Na wananchi pia tuko wazembe sana. Kuna vitu tunachukulia poa tu au tunaona ni sehemu ya starehe. KUJIFUNZA KUOGELEA. Watumiaji wengi wa hivi vivuko asilimia kubwa ni wakazi wa hayo maeneo, yaani kutumia vivuko ni sehemu ya maisha yao ya kila siku kama sio kila wiki. Maji ya ziwa, bahari ni sehemu yao, wajifunze kuogelea. Kuogelea ni kama kujifunza baiskeli, ukijua umejua. Hausahau hata usipoogelea miaka mingi kisha ghafla ukatupwa majini.
Watu wangepona wengi hapa kama wangekuwa wanajua kuogelea, umbali huo ni mfupi sana kupoteza watu wengi kiasi hiki.
 
Back
Top Bottom