July mwaka huu Serikali ilikarabati kivuko cha MV Nyerere, kwa hivyo suala kuhusu ubovu wa kivuko halina mashiko.
Hawa wahusika wanaoruhusu kundi kubwa la watu zaidi ya 400 kwenda kujazana kwenye meli yenye capacity ya watu 100 tu wachukuliwe hatua stahiki na kuwajibishwa kwa kusababisha vifo vya kutisha kwa uzembe na ulafi wa pesa uliopitiliza.
Nina uhakika hizo fedha haramu za watu 300 waliobaki zilitiwa mifukoni mwa wajanja wachache.
Huduma muhimu na nyeti kama ya maji, watu wanakwambia hawana idadi ya wasafiri!!! Kweli?
Tiketi anakata nani hasa? Kwa kweli ni uhuni wa kutisha uliogharimu maisha ya watu ambao wenye mchango mkubwa kwa Taifa hili na wengine wanategemewa na familia zao.
Tanzania ni nchi ambayo haina nidhamu ya usafiri katika maeneo yote kuanzia kwenye daladala, mabasi, magari ya wanafunzi, mpaka usafiri wa maji.
Watu wanajazwa kama siafu!!
Marehemu wote wapumzike kwa amani.