Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

H Hakuna anayemchukia RC wa Mwanza wala hakuna atakaye furahia au kufaidika na kuadhibiwa kwa mkuu Huyo. Unachopaswa kujua huwa kuna kitu kinaitwa HEKIMA au BUSARA, hata kama pasingekuwepo na njia yoyote ya kutoa msaada unapaswa kiongozi usome nyakati na hali ikoje.Taifa lote lilikuumbwa na Taharuki kila sikio LA Mtanzania mwenye wasaa wakati huo nahisi lilikuwa huko, ni bora kabisa angekaa kimya akawaondoa watu wake kimya kimya bila hata kuujulisha umma. Hapa kilichotakiwa ni busara tu na hekima ndugu yangu. Zaidi hata angeufumba umma kuwa hali ya HEWA ni mbaya kuliko kutumia kigezo cha GIZA.
 
Points
 
Hakuna kitu kilihuzinisha kama Mhe. RC kusitisha zoezi la uokozi kwakweli. Ina maaana uwezo wake wa kufikiri ulikomea pale......
Temesa kutumia Jenereta na kununua SportLight za 240,000/= ambazo zingefanya eneo hilo kuwa mwanga wa kutosha alishindwa???
Alishindwa kuitisha karabai 50 za wavuvi wa dagaaa eneo zima lingegeuuka mchanaaaaa na Uokozi ungeeendelea vizuri.
Ktk hili ningekuwa mwenye mamlaka RC wa aina hiii HAPANA.
 
Ukiiwazia sn hii ajali kwa ujumla huwezi kujijibu vzr na hata huenda usipate mtu wa kukusaidia kupata majibu yenye msaada hadi uelewe. Taarifa za awali zinasema ni kuzidisha uwezo wake wa mizigo,huenda ika-play kwa kusogea tu karibu na ukweli lkn upande wangu nakuwa sijaridhika kabisa. Kwa tuliowahi kusafiri na ile ferry na kwa muundo wake,napata shida kuamini kwamba ikiwa kweli ilikuwa overloaded na ndiyo sabb yake kuzama,basi ingeweza kuzamia katikati ya safari yake ambako kuna mawimbi makubwa sn. Nikikadiria distance iliyopo Bugorola-Ukara ni almost 50-60km na imeenda kuzama ikiwa ishayapita mawimbi makubwa ambayo yangeweza kuidhuru mapema. Ukubwa wa mashaka yangu pia ni namna gani tukio la kuzama liliweza kutokea kwa ghafla sn ferry nzima ikawa imetumbukia na kupinduka!! Mimi niendelee kuvuta subira tu nikiwa na majonzi makubwa lkn nikitazamia taarifa ya uchunguzi itakuja na majibu yaliyo sahihi zaidi na si kuimbiana huu wimbo wa ilizidisha abiria na mizigo. Imani yangu,pamoja na hiyo bado tutapata sababu nyingine itakayosapoti hii tuliyonayo.
 
Wakati wa tetemo la ardhi Bukoba na watoto waliofariki kwa ajali Arusha,serikali ililalamikiwa kubadirisha matumizi ya rambimbirambi. Badala ya kupatiwa wahanga moja kwa moja ikaelezwa kuwa kiasi kitajenga miundombinu. Wananchi walilalamika kamba ile ni kazi ya serikali.

Leo watanzania tumepatwa na janga kubwa limetuumiza na halitapoa milele. Ni budi tukakumbushana mambo muhimu wakati wa msiba.

Tukahamasisha pia wale waliojiapiza kutotoa rambirambi kwa misiba ya kitaifa kama hii. Serikali ijitafakari iepuke kusema rambirambi zitajenga miundombinu ya kifuko.

Nyongeza

Rais Magufuli ameguswa sana na msiba huu,naamini yupo njiani kuja kuwapa pole wananzego.

Nyongeza 2

Siasa zitaepukwa msibani,kila mtu ana haki ya kutoa pole,awe Lowasa,Mbowe au Sumaye

Kwa niaba ya wanaJF wote, tunasema tumeumia sana.
 
Pia alie kuwa kiongozi wa bunge siku mbunge wa Ukerewe alipo uliza swali akajibiwa utumbo kwa sababu za ijinga na ushabiki wa kipimbavu wa wabunge wa Ccm nae aachie ngazi.
Ki uhalisia Ccm na serikali yake wanatakiwa kulaaniwa kwa hili tatizo
 
Habari ya mchana wana Jamvi

Natanguliza pole kwa ndugu wote waliofikwa na msiba wa kufa maji jamaa zao wa karibu.
Mungu awape faraja ya kipekee.

Kwa namna moja nimeshangazwa na maamuzi yaliyo fanywa na baadhi ya viongozi wetu Mwanza baada ya ajari kutokea.

Maamuzi ya kusitisha safari ya meli (boti) za Mv Clarias (serikali) na mv Nyeunge (mwarabu) zilizo kua zikifany safari yake kutoka Nansio kwenda Mwanza muda wa mchana ili kwenda kusaidia swala la uokoazi. Ambapo meli ya Mv clarias ilikua tayari imeanza safari ya Kueleke Mwanza ikabid irudi ishushe Abiria na kuelekea eneo la tukio vile vile Nyeunge ilifanya vivyo ivo pamoja na kushusha Magari yalio kua yakivushwa.

Sawa ni Jambo jema
Ila habari ya kusikitisha ni kuwa mpaka muda huu hizo meli hazijarudi kuendelea na Huduma yake ya kuvusha watu kati ya Nansio (Ukerewe) -Mwanza watu wamekwama watu wameshindwa kufika ma offisin watu wameshindwa kuvusha biashara zao watu washindwa kwenda kuona wagojwa wao, walio kua wakienda mbali wameachwa na ndege na hasara nyingine nyingi.

Je serikali haina mbadala wowote wa uwokozi kiasi kwamba Huduma za kijamii zimesimama?
Kwa nin serikali asinge agiza meli za mizigo zisaidei uokoaji izo za abiria zikaendelez Huduma?
Kwa nini wa si ruhusu meli moja itoe huduma na iyo moja iendelee na uokozi wa miili?

Au ni maamuzi ya bila kufikiria ya Viongozi wetu?

SAWA AJARI IMETOKEA ILA LAZIMA MAISHA YAENDELEE

PUMZIKENI KWA AMANI NDUGU ZETU . TUTAWAKUMBUKA DAIMA [emoji120]
 
Mkuu
Picture Ile Jana Imezagaa Baadhi Yetu Tukasema JW Wapo Kazini Kumbe Hakuna Siyo Ya Tukio


Mungu Awape Pumziko La Milele
Sio picha ya tukio mkuu.
Wanahabari wetu ni wavivu sana,sijui ndivyo wanavyofunzwa huko vyuoni?
Au ndio tabia ya kupenda kuwa wakwanza kutoa taarifa.
 
Katibu wa UVCCM Mwl Raymond Stephen Mwangwala (MNEC) kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndugu Hassan Bomboko amewaelekeza makatibu wa mikoa ya kanda ya ziwa iliyopo jirani na mkoa wa Mwanza haraka sana kujiunga na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri Denice James (MCC) katika kusaidia zoezi la uokoaji.
 
Hivi huyu waziri bado yuko kwenye wadhifa wake na hana mpango wa kujiuzulu?? Shameee
 
Kama zoezi limeisha hii ya waliookolea WANAZIDI 40 ndio nini?
Yaani mpaka aibu Walahi
 
Uamuzi wa busara,nampongeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…