Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Watakuwa wamekamilisha zoezi la kutoa miili yote.Ulitaka wafanye hiyo kazi kwa siku ngapi?
 
Inasikitisha sana mkuu! Kila mwenye akili timamu sasa na aamini kwamba Serikali inayojipambanua kuwa ni ya wanyonge haiguswi kwa namna yoyote na unyonge wao. Nadhani hata shetani hakupata usingizi wa kutosha usiku huo, ila Serikali ya Awamu ya Tano, Serikali ya Wanyonge ililala usingizi wa pono, huku ikitarajia asubuhi ikaendelee 'kuokoa' wahanga wa ajali ambao iliamua kuwaacha jana kwa sababu ya GIZA! Na ikaamini itawakuta hai! Maajabu hayataisha duniani.
 
Wataka itumike kiuchumi au?kiongozi kuwajibika sini swala la kawaida sana kwenye uongozi
 
Makosa ya kujirudia haya..hamna kinachoweza kufananishwa na uhai wa mtu..y hatujirekebishi??
 

Jamani hivi vyombo waache kuvipa majina ya viongozi. ni fedheha kwa baba wa Taifa kwa hiki lilichotokea kuhusiana na MV Nyerere. Please!
 
Pole Hivi Punde ni masikitiko makubwa. Tuwaombee wapumzike kwa amani.
Sky Eclat Mwifwa jana nilisema jamani haiwezekani meli/kivuko kikawa upside down na kimejaa watu wakafa watu 6 tu, nikashambuliwa na ISIS . The toll now is over 126! So sad, I lost my sister in Mv Bukoba. Nilipoona Mv Bukoba iko upside down nikakata tamaa maana dada likuwa over 60 yrs na hajawahi kuogelea na alikuwa second class vyumbani, halafu mtu anasema atapona
 
Ukisema kuna sababu ya kibinadamu na nyingine ya mechanical utakuwa unakosea sana kwa sisi ambao tumechukuwa mechanical engineering.Tafsiri ya ajali kitaalam ni UZEMBE.Kwahiyo hapa kuna makosa yakibinadamu tu kutokana na kuwa binadamu ndiye mwenye kuhakiki chombo na kufata au kujuwa fatigue ya chombo.Ukweli ukisema utasikia hiyo ni siasa, lakini ukweli huohuo ukizungumzwa upande wa pili huwa mnashangilia na kurukaruka.Tuwe serious na maisha ya wenzetu.
 
Hao attendant wamesoma hkl unategemea nini?
 
Pole Mkuu


Hapa kiasi chake umewafurahisha wapenda kukutusi.

Nakufuatilia kwa karibu.
 
Mp.uuzi ww....u dont even think
 
Ulikoenda siko.MTU akielimika ndo kuwa na uwezo was kuchambua mambo kama alivyofanya paskali.Wewe unasukumwa na ushabiki kiasi kwamba naanza kuwa na wasiwasi na elimu yako.Kumbuka ni wajibu wa serkali kuelimisha watu wake na usichukulie kama fadhila kama wanavyosoma watu wa theolojia ya dini kwamba wakipata elimu hiyo si rahisi kuwa against na Mungu.Njoo na hoja pevu ili tusihoji juu ya elimu yako.
 
Zitaliwa, msitoe. Waombeeni tu waliofiwa, waliokufa , majeruhi Mungu awape kila lililo jema kwa kila kundi. Mambo ya rambi rambi achana nayo, zitaliwa au kupelekwa kusikojulikana.
Mungu wasaidie wote kwa faraja inayowafaa. AMEN

TUMEGUSWA WOTE: KAMA UMEGUSWA WAPELEKEE WAFIWA/WAHUSIKA MOJA KWA MOJA MAJUMBANI KWAO
 
Na hii ndo inaleta shida sana hapa nchini,mtu kuhitaji kudanganywa na si kupewa ukweli,kiasi mmezoea kudanganya na kudanganywa ndo imekua sehemu ya maisha yetu,kimefika kipindi cha ukweli na uwazi nao hamuutaki na mnashauli mkuu wa mkoa angedanganya eti hiyo ndiyo hekima na busara.kweli uongozi wa sasa una kazi kubwa sana kueleweka kwa wananchi.ndiyo maana wananchi wengi ukipita vijiweni na sehemu za kazi wanawaza kauli ya kuwalidhisha ili wafurahi hata kama ni uongo.wakipewa ukweli kwa kua ni mchungu wanauchukia,mkuu wa mkoa yupo sawa kabisa kusema ukweli wa kilichopo kuliko kudanganya
 
Wanaokoa nini wakati usiku uokozi ulisitishwa kisa giza?Mambo mengine hovyo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…