SOLDIER GENIUS
JF-Expert Member
- Mar 3, 2015
- 358
- 241
Rest in peace...lakini kwann hatujifunzi kwa mv bukoba na mv spice?..maana chanzo ni kile kile cha kuzidisha mzigo...dah something is wrong with someone responsible
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama jana mchana Septemba 20, 2018 imefikia 126 huku uokoaji ukiendelea.
Akizungumza wakati akihojiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) leo saa 10:30 jioni, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Issack Kamwelwe amesema miili 36 tayari imetambuliwa na ndugu na jamaa wakati kazi ya kuitambua iliyosalia ikiendelea.
Amesema hadi leo mchana waokoaji walikuwa wameipata miili 76 na waliporejea tena kuanzia saa 10 jioni walifanikiwa kupata mingine na kufanya idadi yake ifikie 126.
Soma Zaidi: Lowassa, CUF wawalilia waliofariki dunia kuzama kwa MV Nyerere
Leo saa 5 asubuhi, ilielezwa kuwa miili iliyokuwa imepatikana hadi muda huo ilikuwa 42, jana ilipatikana 44 na kufanya idadi yake kufikia 86, baadaye mchana kuongezeka hadi 94.
Waziri huyo ameahidi kutoa taarifa nyingine saa 12 jioni ambayo itatoa mwelekeo halisi kama kazi ya kuopoa miili mingine itaendelea au kuahirishwa hadi kesho.
“Bado kazi ya kusaka miili zaidi inaendelea. Nitazungumza tena baadaye jioni na tutaeleza kama tunaweza kuendelea na kazi hii au itatubidi kuahirisha hadi kesho,” amesema.
Soma Zaidi: VIDEO: Mbatia: Ajali ya MV Nyerere ni ya kujitakia
Hata hivyo, leo mchana Kamwelwe wakati akihojiwa na TBC amesema uokoaji utasitishwa saa 12 jioni.
Kuhusu uokoaji, amesema wazamiaji hawajakumbana na ugumu wowote zaidi ya kukuta mizigo ambayo hulazimika kuitoa kwanza ili waweze kutoa miili.
Kamwelwe amesema kila wakati wamekuwa wakiwasiliana na na Rais John Magufuli ambaye amekuwa akifuatilia tukio hilo kwa ukaribu mkubwa.
“Mheshimiwa Rais macho yake yote yako huku na kila mara nimekuwa nikiwasiliana naye,” amesema.
Inasikitisha sana mkuu! Kila mwenye akili timamu sasa na aamini kwamba Serikali inayojipambanua kuwa ni ya wanyonge haiguswi kwa namna yoyote na unyonge wao. Nadhani hata shetani hakupata usingizi wa kutosha usiku huo, ila Serikali ya Awamu ya Tano, Serikali ya Wanyonge ililala usingizi wa pono, huku ikitarajia asubuhi ikaendelee 'kuokoa' wahanga wa ajali ambao iliamua kuwaacha jana kwa sababu ya GIZA! Na ikaamini itawakuta hai! Maajabu hayataisha duniani.Hilo la kukimbilia mbele ni kweli linasababisha Inbalance but lazima kuna sababu nyingine kubwa, taarifa zilizopo (japokuwa sijui kama ni za kweli) ni kwamba kulikuwa na abiria kiasi cha 400 na uwezo wa kivuko ni abiria 100, Serikali hii ambayo jeshi lake la polisi huwa linatumia Intelligensia ya hali ya juu kufanya maamuzi ya kuzuia mikutano ya wapinzani inashindwaje kuona udhaifu huu ?, hii ni serikali mzigo, wadau wanuliza hivi angekuwemo mama yake na JPM wangesitisha uokoaji jana ?
Wataka itumike kiuchumi au?kiongozi kuwajibika sini swala la kawaida sana kwenye uongoziDalili zimeanza kuonesha, baadhi ya Wanasiasa kudai watu flani wawajibike,wajiudhuru, mawazo ambayo yako kisiasa zaidi, ni kweli ipo sababu iliyopelekea kutokea ajali hiyo mbaya, sababu zinaweza kuwa ni za uzembe wa kibinadamu,au za kitaalamu(mechanical problems), hivyo kwenda moja kwa moja kwenye(human error) tutakuwa hatuwatendei haki wataokumbwa na sakata. Itakuwa kisiasa zaidi, hivyo kabla ya yote Mashauri uchunguzi wakina ufanyike, isije kutokea kama ile ya Muhimbili kupasua kichwa badala ya mguu na mguu badala ya kichwa, maamzi ambayo yalipelekea kuwapoteza !adakitari bingwa wa mifupa na wenye uwezo mkubwa, ambao Mara moja Botswana iliwachukua hadi leo wanafanya maajabu huko. Ikumbukwe mfano Prof. Kinasha alieleza kwamba alikuwa ameshafanya upasuaji wa kichwa kwa watu 1,008 na wote walipona, na huyu ambaye ni bahati mbaya alikuwa wa 1,009. Sasa akahukumiwa kwa kosa moja tu !!!! Hii ilikuwa kisiasa zaidi ikiongozwa na Prof. Mwakyusa, Sikatai kuwa uzembe ni mbaya na unaweza kugharimu maisha ya watu, jambo ambalo kamwe halikubaliki wala kuvumilika. Lakini pia sikubaliani kuona kuwa watu wanaadhibiwa kwa mintarafu ya kisiasa, watu kutafuta kiki za kuonekana na jamii kwamba wamechukua hatua. Ajali hutokea kokote kule hata Ulaya na marekani, mfano Nyambizi ilizama, je nani aliwajibishwa? Ndege aina ya Conctord iliua watu kibao je nani alifukuzwa kazi? Tusilione limetokea hapa kwetu, sasa ukawa muda wa wanasiasa kuishutumu Serikali nakuitaka kufukuza watumishi wake kwa madai kwamba wamefanya uzembe. Kikubwa hapa ili Wanasiasa waoneshe kukomaa kwao wanatakiwa kuitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya sababu zilizopelekea ajali hii mbaya. Huu ni Ushauri tu na si vinginevyo.
Taarifa nilizozipata haraka sasa hivi ni kuwa watu wengi sana wanahisiwa kufa maji baada ya kivuko kubinuka juu chini, chini juu katika kisiwa cha UKARA wilayani Ukerewe.
View attachment 872210
View attachment 872806
Wakazi wa Ukerewe wakiwa mita chache kutoka kivuko kilipozama
====
Taarifa Kwa Umma Kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme-TEMESA Kuhusu Kuzama Kwa Kivuko Cha MV.Nyerere
View attachment 872340
Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria kimezama huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hazijajulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara. Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka.
Amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho.
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho na yuko njiani kulekea huko na watatoa taarifa baadaye.
Kivuko cha MV. NYERERE kilinunuliwa na kuanza kutoa huduma mwaka 2004. Kilifungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 191 JULY 2018. Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja.
UPDATES: 1900HRS
=> Watu watano wamekufa na wengine 32 wameokolewa mpaka sasa ila hali zao ni mbaya kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere.
=> "Mtu Hajalipwa Mshahara Halafu Anasikia Trilion 1 Imepotea Inauma" -Joseph Mkundi
Mbunge Joseph Mkundi akitahadharisha kuhusu kivuko cha MV Nyerere Apr 24, 2018
Alikuwa akichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano iliyopo chini ya Waziri wake, Profesa Makame Mbarawa.
UPDATES:
Rais Magufuli atuma salamu za RambirambiAJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE: WATU 44 WAMEFARIKI, ZOEZI LA UOKOAJI LASITISHWA HADI KESHO
"Nimeshtushwa na kusikitishwa sana na ajali ya MV Nyerere, nawapa pole wote waliopoteza jamaa zao na nawaombea wote walionusurika kupona haraka, kwa wakati huu nawaomba tutulie wakati juhudi za uokoaji zinaendelea"
Mbali na idadi hiyo ya waliofariki, Watu 37 wameokolewa katika ajali huku hali zao zikiwa mbaya
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema zoezi la uokoaji limesitishwa kutokana na giza kuingia
10:40 - MIILI 86 IMESHAOPOLEWA MPAKA SASA
Idadi ya vifo katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere, Mwanza imefika watu 86 huku uokoaji ukiendelea, RC John Mongella amethibitisha
11:41 - IDADI YA WALIOOPOLEWA YAFIKA 94
Idadi ya vifo katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere, Mwanza imefika watu 94 huku uokoaji ukiendelea, RC John Mongella amethibitisha
11: 43 Chanzo cha kuzama kwa mujibu wa DC wa Ukerewe
DC Ukerewe amesema kivuko kilikuwa kimebeba zaidi ya abiria 400, kilivyokaribia kufika mwaloni(kutia nanga) nahodha akapunguza spidi hivyo abiria wakakimbilia upande wa kushukia ili wawahi kutoka, kivuko kikazidiwa uzito na kupinduka.
12:40 - MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKA 100
Miili ya waliokufa na kuopolewa mpaka sasa yafika 100.
12:49 - IGP SIRRO: UTAMBUZI WA MAREHEMU UNAENDELEA
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simoni Sirro amesema utambuzi wa marehemu katika ajali ya MV Nyerere mkoani Mwanza unaendelea kwa miili iliyoopolewa.
Litafunguliwa Jalada maalum la kuchunguza tukio la kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere
13:03 - Idadi ya miili iliyoopolewa yafika 125
Idadi ya miili iliyoopolewa kwenye kivuko cha Mv Nyerere imefikia 125 mpaka sasa
13:20 - WAZIRI ISACK KAMWELWE: ZOEZI LA KUOPOA MIILI ILIYOKWAMA LITAKAMILIKA SAA 12 JIONI LEO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema shughuli ya uokoaji wa watu walionasa kwenye kivuko cha MV Nyerere inatarajiwa kukamilika leo saa 12 jioni
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema mazishi ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya Mv.Nyerere iliyotokea Septamba 20 huko kisiwani Ukara, Ukerewe mkoani Mwanza yatakuwa ya kitaifa ambapo viongozi wakuu wa kitaifa wanatarajia kushiriki mazishi hayo.
Hao attendant wamesoma hkl unategemea nini?Nimesikitika sana kusoma kwamba sababu ya kivuko kupinduka ni abiria kukimbilia upande mmoja ili wawahi kushuka kivuko kikitia nanga, hivyo kupelekea kivuko kuzama. Abiria wanatakiwa kupewa elimu ya jinsi uwiano wa uzito ulivyo muhimu kwa kivuko kuelea majini.Nashauri kwenye vivuko kuwe na "vessel attendants" kama ilivyo kwa "flight attendants" kwenye ndege ambao kazi yao ni kuelekeza abiria nini cha kufanya waingiapo kivukoni, wakati gani wa kuanza kujiandaa kushuka, kuonyesha jinsi ya kuvaa boya(maybe thru a tv screen)n.k. Hii ajali insingetokea iwapo kungekuwa na watu wa kuwazuia/elekeza abiria kusubiri walipo hadi kivuko kitie nanga.
Anyway, yameshatokea. Nawapa pole wote walioguswa kwa karibu na maafa haya.
RIP marehemu wote.
Mbona umebadilisha avatar picture??Akijiuzulu ..
Nakunya hapa mpk magogon
Mp.uuzi ww....u dont even thinkKigTE="Aleppo, post: 28449505, member: 170541"]Si utani ngoja nikutajie listi
1. Kingunge alitembelewa mwishowe akavuta
2. Maria na Consolata mwishowe akavuta
3. Samuele Sita mwishowe kavuta
4. Yule aliyechora nembo ya taifa mwishowe kavuta
5. Mzee Majuto naye alivuta
6. Mzee mmoja wa CCM (jina nimelisahau) naye kavuta
7. Wengine niliowasahau nao wamevuta
Yaani hawaponi kabisa!
Duh nimeaanza kumuogopa kwa kweli ata nikiumwa nikimsikia anakuja ntakimbia na dripu zangu maana maisha matamu
Ulikoenda siko.MTU akielimika ndo kuwa na uwezo was kuchambua mambo kama alivyofanya paskali.Wewe unasukumwa na ushabiki kiasi kwamba naanza kuwa na wasiwasi na elimu yako.Kumbuka ni wajibu wa serkali kuelimisha watu wake na usichukulie kama fadhila kama wanavyosoma watu wa theolojia ya dini kwamba wakipata elimu hiyo si rahisi kuwa against na Mungu.Njoo na hoja pevu ili tusihoji juu ya elimu yako.Nimesoma kwa kina andiko lako Pascal Mayalla, naamini mtu yeyote aliyesoma shule na hiyo elimu ikamstaarabisha hawezi kukubaliana na hoja yako kwamba eti watu hawawajibiki kwa makosa ambayo ama ni moja kwa moja wamehusika au ni kwa migongo ya wsnawaongoza, Tumeshuhudia, akina Tibaijuka. Muhongo, Kitwanga. Nape, Nchemba, Je hao walipowajibika ilikuwa enzi ya Baba wa Taifa hili? Hasira yako hakika inatokana na ndugu yako kuwajibika ? Au inatokana na chuki yako binafsi? Binafsi nakufahamu sana pengine kuliko hata unavyojifahamu wewe. Kila Mara mandiko yako huwa ni ant system, lakini unasahau kuwa Taifa hili limekusomesha , linakupa fursa ya kujivinjari mitandaoni kwa gharama nafuu kabisa, kuwa na shukrani kwa Serikali yako. Siyo kila siku kuibeza.
Nafurahi kuona ombi langu linatekelezwa kwa vitendo!Sio leo, siku zote niko hivyo mimi ni mkweli daima.
TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali Wachunguzwe, Wafumuliwe! - JamiiForums
P.
Na hii ndo inaleta shida sana hapa nchini,mtu kuhitaji kudanganywa na si kupewa ukweli,kiasi mmezoea kudanganya na kudanganywa ndo imekua sehemu ya maisha yetu,kimefika kipindi cha ukweli na uwazi nao hamuutaki na mnashauli mkuu wa mkoa angedanganya eti hiyo ndiyo hekima na busara.kweli uongozi wa sasa una kazi kubwa sana kueleweka kwa wananchi.ndiyo maana wananchi wengi ukipita vijiweni na sehemu za kazi wanawaza kauli ya kuwalidhisha ili wafurahi hata kama ni uongo.wakipewa ukweli kwa kua ni mchungu wanauchukia,mkuu wa mkoa yupo sawa kabisa kusema ukweli wa kilichopo kuliko kudanganyaH
Hakuna anayemchukia RC wa Mwanza wala hakuna atakaye furahia au kufaidika na kuadhibiwa kwa mkuu Huyo. Unachopaswa kujua huwa kuna kitu kinaitwa HEKIMA au BUSARA, hata kama pasingekuwepo na njia yoyote ya kutoa msaada unapaswa kiongozi usome nyakati na hali ikoje.Taifa lote lilikuumbwa na Taharuki kila sikio LA Mtanzania mwenye wasaa wakati huo nahisi lilikuwa huko, ni bora kabisa angekaa kimya akawaondoa watu wake kimya kimya bila hata kuujulisha umma. Hapa kilichotakiwa ni busara tu na hekima ndugu yangu. Zaidi hata angeufumba umma kuwa hali ya HEWA ni mbaya kuliko kutumia kigezo cha GIZA.