Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Dalili zimeanza kuonesha, baadhi ya Wanasiasa kudai watu flani wawajibike,wajiudhuru, mawazo ambayo yako kisiasa zaidi, ni kweli ipo sababu iliyopelekea kutokea ajali hiyo mbaya, sababu zinaweza kuwa ni za uzembe wa kibinadamu,au za kitaalamu(mechanical problems), hivyo kwenda moja kwa moja kwenye(human error) tutakuwa hatuwatendei haki wataokumbwa na sakata.

Itakuwa kisiasa zaidi, hivyo kabla ya yote Mashauri uchunguzi wakina ufanyike, isije kutokea kama ile ya Muhimbili kupasua kichwa badala ya mguu na mguu badala ya kichwa, maamzi ambayo yalipelekea kuwapoteza !adakitari bingwa wa mifupa na wenye uwezo mkubwa, ambao Mara moja Botswana iliwachukua hadi leo wanafanya maajabu huko.

Ikumbukwe mfano Prof. Kinasha alieleza kwamba alikuwa ameshafanya upasuaji wa kichwa kwa watu 1,008 na wote walipona, na huyu ambaye ni bahati mbaya alikuwa wa 1,009. Sasa akahukumiwa kwa kosa moja tu !!!!

Hii ilikuwa kisiasa zaidi ikiongozwa na Prof. Mwakyusa, Sikatai kuwa uzembe ni mbaya na unaweza kugharimu maisha ya watu, jambo ambalo kamwe halikubaliki wala kuvumilika.

Lakini pia sikubaliani kuona kuwa watu wanaadhibiwa kwa mintarafu ya kisiasa, watu kutafuta kiki za kuonekana na jamii kwamba wamechukua hatua. Ajali hutokea kokote kule hata Ulaya na marekani, mfano Nyambizi ilizama, je nani aliwajibishwa?

Ndege aina ya Conctord iliua watu kibao je nani alifukuzwa kazi? Tusilione limetokea hapa kwetu, sasa ukawa muda wa wanasiasa kuishutumu Serikali nakuitaka kufukuza watumishi wake kwa madai kwamba wamefanya uzembe.

Kikubwa hapa ili Wanasiasa waoneshe kukomaa kwao wanatakiwa kuitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya sababu zilizopelekea ajali hii mbaya. Huu ni Ushauri tu na si vinginevyo.
Kwahiyo umeona siasa? Aliyewahi kukosoa na kuelekeza alikuwa na malengo ya kisiasa. Kukosa taa hata tochi za kusaidia kunusuru uhai nazo siasa et. Mstarini kwa mamba kenge hawakosi.
 
Nilitegemea kwa wakati huu KUB Mbowe angekuwa kisiwani Ukerewe kujumuika na mbunge wa jumbo hill ambaye ni wa Chadema pamoja na timu nzima ya viongozi wa serikali na vyombo vya dola. Kwanini Mbowe kamuacha mbunge wake akiwa mpweke katika wakati huu mgumu!
Kuna mbinu za kumtanguliza,acha mwenyekiti ajifiche,tabia yenu ya kutanguliza watu Mungu hapendi
 
Nilitegemea kwa wakati huu KUB Mbowe angekuwa kisiwani Ukerewe kujumuika na mbunge wa jumbo hill ambaye ni wa Chadema pamoja na timu nzima ya viongozi wa serikali na vyombo vya dola. Kwanini Mbowe kamuacha mbunge wake akiwa mpweke katika wakati huu mgumu!
mavi mkanye nyinyi , ahangasike mbowe, why?! Mnapoteza 80 bn Tsh kununua wapinzania badala ya vivuko 6! Rubbish! Mwifwa
 
Hivi vivuko vinabeba sana kupita uwezo wake sio hicho tu kuna vivuko vinabeba mizigo na watu hadi vinakema.

Usimamizi na umakini unatakiwa kwenye vivuko vyote nchini, pia sijajua kama MV Nyerere haikuwa na maboya.
 
Mbona bendera hazipepei nusu mlingoti.Kuna nini kinaendelea Tanzania.
Kwa HEKIMA yake rais amelizunguzia LIVE TBC na kutangaza siku za maombolezo likiwemo hilo ulilolitaja!
 
  • Thanks
Reactions: Gut
sasa kama

sasa kama serikali ni makini kama wanavyojitapa kupata idadi ya abiria inaweza kuchukua muda gani. Sema ni visasi vt=ya chama tawala kwa ambao hawakuwapigia kura , maana ndo yamekuwa maneno yao na leo yanatokea

Ukisema ni visasi vya chama tawala unakuwa unakosea.

Tuangalie zaidi wasimamizi wa kivuko je walikuwa wanafanya kazi yao kwa kufuata sheria na kanuni za uchukuzi?

Mbona daraja la kivukoni linasimamiwa vizuri tu?
 
Nilitegemea kwa wakati huu KUB Mbowe angekuwa kisiwani Ukerewe kujumuika na mbunge wa jumbo hill ambaye ni wa Chadema pamoja na timu nzima ya viongozi wa serikali na vyombo vya dola. Kwanini Mbowe kamuacha mbunge wake akiwa mpweke katika wakati huu mgumu!
May be ajali ingekuwa imetokea kanda yake!! Yuko busy anaongea na waandishi wa habari.
 
Nilitegemea kwa wakati huu KUB Mbowe angekuwa kisiwani Ukerewe kujumuika na mbunge wa jumbo hill ambaye ni wa Chadema pamoja na timu nzima ya viongozi wa serikali na vyombo vya dola. Kwanini Mbowe kamuacha mbunge wake akiwa mpweke katika wakati huu mgumu!
Kwanini mkuu wa nchi naye hayupo huko kuwafariji wananchi wake?
 
hapo pele ni mbunge tu aliyetoa tahadhari mapema wengine wote vidampa tu hadi magufuli mwenyewe
 
Tatizo serikali, wote tunaishi kwa kuangalia serikali inasema nini.!
 
Tukamate na yeye, maana ni serikali yake ndio ina jukumu la kuhakikisha miundombinu ya KISASA ya uokozi pamoja na wataalamu waliofuzu kwa hilo. Mbona pesa za kununua waungao mkono juhudi pamoja na madege zipo?? KARNE HII uokozi unasitishwa eti sababu ya GIZA!!? Kwani tume ngapi zilishaundwa tangu MV Bukoba na vifo vya KIZEMBE kabisa vimeendelea.
 
Nimesikitika sana,sikutarajia kabisa hadi nikawaza labda jana ilikuwa ndoto tu kuhusu ajali kwani si TBC ,star TV na wengine ni mziki wala hakuna hata updates,

"Labda vyombo vya habari vimezuiliwa kufanya lolote kuhusiana na ajali hii" hapa ndo nilipoamua kutune BBC .
 
Nilitegemea kwa wakati huu KUB Mbowe angekuwa kisiwani Ukerewe kujumuika na mbunge wa jumbo hill ambaye ni wa Chadema pamoja na timu nzima ya viongozi wa serikali na vyombo vya dola. Kwanini Mbowe kamuacha mbunge wake akiwa mpweke katika wakati huu mgumu!
Lile zuio la kutokutoka dar bila kibali maalum mmelisahau???

Mbowe ndio mwenye kikosi cha uokoaji???

Yule aliegonga twiga mlikimbizana usiku na mchana na machopa Leo hawa mnakosa taa za kuwaokolea ???

Vichaa on fleek
 
Nilitegemea kwa wakati huu KUB Mbowe angekuwa kisiwani Ukerewe kujumuika na mbunge wa jumbo hill ambaye ni wa Chadema pamoja na timu nzima ya viongozi wa serikali na vyombo vya dola. Kwanini Mbowe kamuacha mbunge wake akiwa mpweke katika wakati huu mgumu!
Chief comforter ndiye anatakiwa kuwa kule. Mbowe hana serikali wala dola walioathirika ni wananchi wa.vyama mbali mbali na wasio na vyama wala siyo CHADEMA tu na ni msiba wa kitaifa siyo wa mbunge!
 
Back
Top Bottom