Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

mbona dakika hii mkuu wa nchi yupo live anaongelea hiyo habari??!
au ulitaka 24 hours waoneshe tukio moja tu
Mkuu nimemsikiliza na huo ndo uongozi.
Katika hilo Rais Magufuli ni lazima apongezwe.
 
Keeping your mouth shut can be the best way to conceal your unhinged state of mind!
Huyo jamaa hujamuelewa ungemuelewa usingemjibu hivo
Yeye amejibu kwa akili za jiwe.mara kadhaa jiwe amekua akipendelea waliomchagua na kikiri kabisa hadharani
 
Daaah Poleni sana wafiwa ila haya mambo ya kuzidisha abiria lazima wahusika watafutwe!!
 
Kwani hii ndio ajali ya kwanza ya uzembe hadi watu wawajibike?!. MV Bukoba aliwajibika nani?. MV Spice Island amewajibika nani?.
Kifo cha Daudi Mwangosi, amewajibika nani?!. .
Kifo cha Akwiline amewajibika nani?!
Mpaka watu wangapi wafe ndipo watu wawajibike?.

Utamaduni wa kuwajibika, umekufa na Nyerere!,
Mimi ni muhanga wa uwajibikaji, wakati wa Nyerere, baba yangu, Mzee Andrew Mayalla, ndiye alikuwa RSO wa Mwanza, kuna mahabusu wawili, Masanja Makulla Mazengenuka na Issack Mwanamkoboku, walikufa mikonani mwa polisi katika mahojiano baada ya kutuhumiwa kuhusika na mauaji ya vikogwe.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hasssan Mwinyi alijiuzulu!,
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Mzena, alijiuzulu!,
Mkuu wa jeshi la Polisi, IGP, Pundugu alijiuzulu!.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Peter Kisumo, alijiuzulu!
RSO wa Mwanza, RPC, RSO na OCD kwanza walistaafishwa kwa manufaa ya umma, kisha wakafunguliwa mashitaka ya Kesi ya Mauaji Mwanza!.

Uwajibikaji ni enzi za Nyerere!.

Ingekuwa Nyerere yupo, hata mtu aliyeuza Nyumba za serikali kwa kuwagawia hata vimada wake, hadi kuuza nyumba za line police!, asingethubutu hata kuwaza kuchukua fomu!. Mtu amelitia taifa hasara ya kulipishwa fudia kibao kwa maamuzi tuu ya papara!.Mtu amenunua kivuko mtumba kwa mabilioni ya shilingi, halafu hakikufanya kazi!.

Kuwajibika kumekwenda na Nyerere, sasa ni zama za kupeana pole tuu!.

Poleni kwa yote!.

P.
Umefunguka bayana mkuu
 
Unaweza kuomboleza unaambiwa inatumia maafa kisiasa,nani anakuambia uendelee kutamgaza. Hamna shida update tutapata tu CNN, BBC, Sky news nk
Sidhani kabisa janga kama hili kuliportiwa live na vyombo vya habari litakuwa ni la kisiasa .Huo ni UOGA watu wameijengea wenyewe.tu.
 
Dalili zimeanza kuonesha, baadhi ya Wanasiasa kudai watu flani wawajibike,wajiudhuru, mawazo ambayo yako kisiasa zaidi, ni kweli ipo sababu iliyopelekea kutokea ajali hiyo mbaya, sababu zinaweza kuwa ni za uzembe wa kibinadamu,au za kitaalamu(mechanical problems), hivyo kwenda moja kwa moja kwenye(human error) tutakuwa hatuwatendei haki wataokumbwa na sakata.

Itakuwa kisiasa zaidi, hivyo kabla ya yote Mashauri uchunguzi wakina ufanyike, isije kutokea kama ile ya Muhimbili kupasua kichwa badala ya mguu na mguu badala ya kichwa, maamzi ambayo yalipelekea kuwapoteza !adakitari bingwa wa mifupa na wenye uwezo mkubwa, ambao Mara moja Botswana iliwachukua hadi leo wanafanya maajabu huko.

Ikumbukwe mfano Prof. Kinasha alieleza kwamba alikuwa ameshafanya upasuaji wa kichwa kwa watu 1,008 na wote walipona, na huyu ambaye ni bahati mbaya alikuwa wa 1,009. Sasa akahukumiwa kwa kosa moja tu !!!!

Hii ilikuwa kisiasa zaidi ikiongozwa na Prof. Mwakyusa, Sikatai kuwa uzembe ni mbaya na unaweza kugharimu maisha ya watu, jambo ambalo kamwe halikubaliki wala kuvumilika.

Lakini pia sikubaliani kuona kuwa watu wanaadhibiwa kwa mintarafu ya kisiasa, watu kutafuta kiki za kuonekana na jamii kwamba wamechukua hatua. Ajali hutokea kokote kule hata Ulaya na marekani, mfano Nyambizi ilizama, je nani aliwajibishwa?

Ndege aina ya Conctord iliua watu kibao je nani alifukuzwa kazi? Tusilione limetokea hapa kwetu, sasa ukawa muda wa wanasiasa kuishutumu Serikali nakuitaka kufukuza watumishi wake kwa madai kwamba wamefanya uzembe.

Kikubwa hapa ili Wanasiasa waoneshe kukomaa kwao wanatakiwa kuitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya sababu zilizopelekea ajali hii mbaya. Huu ni Ushauri tu na si vinginevyo.
Umesahau CCM walipora msiba wa wanafunzi Arusha na msiba wa mapacha walioungana Iringa hata huu wanajipanga kuupora, ni kawaida yao huwa hawapendi kushirikisha wengine wanataka nguo za kijani tu.
 
Sidhani kabisa janga kama hili kuliportiwa live na vyombo vya habari litakuwa ni la kisiasa .Huo ni UOGA watu wameijengea wenyewe.tu.
Kuogopa awamu hii muhimu kwa mjinga huenda kichekp kwa mwerevu kilio. Maafa ya kagera watu wameipeleka matulubai wakiambiwa wanafanya siasa.
 
Nimesoma kwa kina andiko lako Pascal Mayalla, naamini mtu yeyote aliyesoma shule na hiyo elimu ikamstaarabisha hawezi kukubaliana na hoja yako kwamba eti watu hawawajibiki kwa makosa ambayo ama ni moja kwa moja wamehusika au ni kwa migongo ya wsnawaongoza, Tumeshuhudia, akina Tibaijuka. Muhongo, Kitwanga. Nape, Nchemba, Je hao walipowajibika ilikuwa enzi ya Baba wa Taifa hili? Hasira yako hakika inatokana na ndugu yako kuwajibika ? Au inatokana na chuki yako binafsi? Binafsi nakufahamu sana pengine kuliko hata unavyojifahamu wewe. Kila Mara mandiko yako huwa ni ant system, lakini unasahau kuwa Taifa hili limekusomesha , linakupa fursa ya kujivinjari mitandaoni kwa gharama nafuu kabisa, kuwa na shukrani kwa Serikali yako. Siyo kila siku kuibeza.
Tofautisha 'kuwajibika' na 'kuwajibishwa', hao wote uliowataja hakuna aliyewajibika bali waliwajibishwa
 
Mkuu mamlaka zimeona huu ni muda muafaka, Mchana zoezi la uopoaji wa miili lilikuwa linaendelea

Hakuna cha Muda muafaka mamlaka zimekuwa zinajivuta sana kuhakikisha waliokwama wanaopolewa..

Fikiria kusitishwa kwa zoezi la uopoaji Miili hapo jana, kweli Watanzania wenzetu wapo chini ya maji mamlaka zinapata usingizi...Hii ni aibu.
 
Back
Top Bottom