Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Idara ya uhamasishaji na chipukizi UVCCM Taifa Ndugu Hassan Bomboko inasema Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Kheri Denis James (MCC) amesikitishwa na kuguswa na ajali mbaya ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere katika ziwa Victoria iliyotokea leo ambapo wapo waliojeruhiwa na wengine kufariki dunia hivyo ametoa salamu za pole kwa wote walioguswa na kuathirika na tukio hili la kuhuzunisha na kusikitisha.
Taarifa hiyo imeendelea kusema Ndugu Kheri anawaombea majeruhi kupata nafuu, ndugu na wote waliopoteza jamaa zao wawe na subira katika kipindi hiki kigumu.
View attachment 872725