Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kuanzia kesho ukaguzi wa vyombo vya majini nchi nzima na kuna uwezekano wengine kufutiwa leseni.
Ingekua ya mtu binafsi Mmiliki angewekwa ndani kwahiyo nashauri na hili Waziri mwenye Dhamana awekwe mahabusu wakati uchunguzi ukiendelea.
Sio rahisi. Waziri mwenye dhamana alikuwa mfanyakazi wa cheo cha juu wizara ya ujenzi hakuna shaka atalindwa. Nikukumbushe tu 1996 kipindi cha MV Bukoba kinazama tulikuwa bado angali vijana. Ni mapenzi ya Mungu tu kushuhudia leo tena tunawapoteza ndugu zetu kwa uzembe
 
Haki ya Mungu walahi ,kweli sisi ni shithole country yaani mkuu wa Mkoa anasema uokoaji umesitishwa mpaka kesho kwa sababu ya giza ? Kana kwamba walioko majini ni kambale sio binadamu ,kama kuna walio hai ambao wangeweza kuokolewa usiku huu badala yake wakawatoe kesho wakiwa maiti ?
Kwa kauli kama hizi naanza kuona kabisa hii ajali ina kitu nyuma ya pazia ,ni kitu gani muda utatupa jibu

Salalee!
 
Daaa Leo tu tukiwa tunatoka kuangalia mechi CCM Kirumba baada ya kuviona vivuko kadhaa nimetoka kuwaambia jamaa zangu kwamba Mimi ktk vitu ninavyohofia na sitopanda kirahisi ni usafiri Wa majini hasa nikikumbuka ajali ya MV Bukoba. Nawasha data kwenye simu nakutana na janga kama hili hadi jamaa zangu wakanipigia simu wakinbia uliyokuwa unatuambia yametokea Leo mana tulikuwa tushaachana. Nimesikitika sana kwa sababu huwa nawaza mfa maji anavyohangaika hadi kifo anakiona kabisa kwamba sasa ndio naondoka
R.I.P kwa walofariki na Mungu awaponye walionusurika. EE BABA MUNGU UTULINDE KTK SHUGHULI ZETU ZA KILA SIKU!
 
Mungu awawekee mkono ndugu zetu....

Alafu keshokutwa utasikia jiwe akisema, NILIPOKUA NAOMBA KURA SIKUSEMA NITALETA MAAFA
 
#UPDATES:Zoezi la uokoaji wa abiria waliokuwemo katika kivuko cha MV Nyerere limesitishwa kutokana na giza, na litaendelea kesho alfajiri.ambapo hadi sasa waliyookolewa wakiwa hai ni 37, waliokufa 44.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

Hivi hii si aibu hivi kwa dunia ya sasa unaweza kutoa kauli za kijinga namna hii yaani watu walale kwenye maji hadi asubuhi hii ni nchi au ni genge la shetani
Sorry mkuu hich kivukoo kulikuwa na watu wangap... Kuna sehemu nmesoma nmeona n 500 vp Kuna ukwel juu ya hilo. . Afu had zoezi linactishwa inamaana watu waliopatikana+ miili n 81 ko tuna watu 390+ hatujui walipo...,au Kuna wengine wameogelea had nchi kavu?
 
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Idara ya uhamasishaji na chipukizi UVCCM Taifa Ndugu Hassan Bomboko inasema Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Kheri Denis James (MCC) amesikitishwa na kuguswa na ajali mbaya ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere katika ziwa Victoria iliyotokea leo ambapo wapo waliojeruhiwa na wengine kufariki dunia hivyo ametoa salamu za pole kwa wote walioguswa na kuathirika na tukio hili la kuhuzunisha na kusikitisha.

Taarifa hiyo imeendelea kusema Ndugu Kheri anawaombea majeruhi kupata nafuu, ndugu na wote waliopoteza jamaa zao wawe na subira katika kipindi hiki kigumu. View attachment 872725
Huyu bora asiombe tuu
 
Sasa unashangaa nini kutokujua idadi ya watu .......kivuko cha hapo kigamboni geti likifunguliwa kila mtu spidi ndani ....kila mtu anawahi anapokwenda .....sawa na mwendo kasi utahesabu abiria wangapi wapo kwenye gari ..... ni ajari kivuko kime overload basi
Nimeelewa
Nafikiri kungekuwa na utaratibu wa kuhesabu watu na kivuko kikifika wanaingia hao hao basi
Mbona linawezekana sana.
 
poleni sana, lakini kaa kuna mbunge ambae alitoa habari ya kuwa hiki kizuko cha nyerere ni hatari kwa maisha ya binadamu hapo april 2018, BONA HAKUNA MTU AMBAE ALISHUGULIKIA HIO SWALA??? wakuu tukumbuke kuwa sisi wanadamu tuna wajibu katika maisha yetu ya kila siku, sio tu ajali kaa hii ikitokea watu wanasema ni mapezi ya mungu, huo mungu SIMUJUI, GOD GAVE US HUMAN RESPONSIBILITY, so if we dont take care of that then this are the kinds of dangers and accicdents that happen, someone MUST BE HELD ACCOUTABLE FOR THIS ACCICDENT.
 
Kama hapazidi mita 100 wakara wenzangu inakuaje washindwe kujiokoa?....maana enzi zetu hizo mita mia ilikua ni kichanga cha pili au cha tatu na ukiishia hapo nikwamba hujui kuogelea
Mkuu tatizo ni chombo kimebinuka wengine wakiwa ndani wamekaa kwenye siti na wengine imelalia kwao kikawafunika. Hapo wale wliorushwa majini kutoka upande ambao hikubinukia ndo hao unaona wanaelea ila wengine wote wamefunikwa.

Kama chombo kingesimama kwanza halafu litolewe tangzo watu wachupe majini wajiokoe chombo kitazama baada ya dakika 3 kwa mfano, nakuhakikishia wakara wote wngefika ng'ambo salama

Ghafla mbaya sana!!!
 
Hiki kivuko ni kidogo, wapeleke vivuko vikubwa kama mv.Sengerema , hako lazima kayumbe kwenye dhoruba
Kiliyumba sababu ya kona mzigo ukayumba upande mmoja.

Again kuna ile tabia ya abiria wakiona wanakaribia ng'ambo wanasimama wote wanajaa mlangoni ile nayo inaharibu equilibrium hasa kw hivi vyombo vidogo
 
Kwanini watu wafe?? Wakati kuna maboyance?
Mungu awapumzishe wote waliopoteza maisha yao.
Na huu ndo upuuzi wa kwenye haya mameli na mamitumbwi ya viktoria....eti maboya Hua yamefungilizwa kwenye chombo...ndo upuuzi wao. Hua wanaona kama usumbufu kuyapanga wakiyafungua na kuwavika watu kabla ya safari na kuyarudisha tena kama wakifika salama.
 
Soma taarifa kwa utulivu.
George Nyamaha alisema timu ya uokoaji bado inaendelea na kazi ya uokozi na kuna uwezekano idadi ya waliofariki dunia ikaongezeka.
Mtu anahesabika amekufa mpaka pale anapoopolewa na kuonekana kafa. Watu ambao bado hawajaopolewa si rahisi kuwaunganisha kwenye idadi ya watu waliokufa eti kwasababu tu hawajaokolewa pamoja na kwmba kunakua na uwezekano mkubwa kwmba watakua wamekufa na ndio maana wnasema "...idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka..."
 
Back
Top Bottom