Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Amefariki. Inauma sana.
Nategemea kusikia naodha naye amefariki maana nasikia naodha lazima awe mtu wa mwisho kutoka chomboni.

Sasa mpk watu wote hao wamekufa nategemea naye amefariki otherwise ajibu maswali yote yatakayo husisha kuzama kwa kivuko hiki.
 
Mlikopeleka akili zenu nyie watu Mungu ndo anajua, hivi kwelikuna binadamu anaweza kukaa ndani ya maji tokea saa nae mchana hadi usiku akawa hai? anapumua kwa matamvua? kivuko kimepinduka karibuna ufukweni ho watu waliokuwa wakitapata usiku kucha uliwaona pekeako? according to you ni hekima kurisk uhai wa walio hai (waokoaji)ili kurecover maiti?!!! upuuzi wa hali ya juu.
Well said walahi
 
Abiria wenyewe walilalamika kudaiwa vitambulisho. Jana majibu yakapatikana.
Na ndo tabia ya Mtanzania.
Kitambulisho anaacha kwenye begi la nguo nyumbani.
Kikihitajika mtu analalama tu.
Yaani mtu analiwa na sangara sisi tunatfta tu mtu kumbe hayupo.
Tubadilike!
 
Jamani mlitaka sfanye nini wakati hakuna vifaa vya kuokolea muda huo?? Na sio kwamba atakuwa alijiamulia tu mwenyewe, hao wazamiaji hawana vifaa vya kufanyia kazi kwenye mwanga itakuwa gizani?? Ni aibu kwa nchi, hatuko tayari kwenye majanga!! Ya nchi kavu tu yanatushinda itakuwa ya majini??
Ulitaka waokoaji nao wafe kwa kukosa vifaa vya kuokolea usiku hyo ndipo ujue walikuwa na uchungu wa watu waliozama, Na wewe jitafajari umeteleza [emoji102] [emoji102]
 
Ila hii ishu ya kuuana kwa makusudi au sijui nimeseme kuuana na kujiua wenyewe sijui itaisha lini, hata mv bukoba tatizo lilikuwa ni kuzidisha watu, na hii nayo hivyo hivyo, hivi kweli kivuko cha kubeba watu 100 kinabeba watu 400? hakuna ukaguzi kwenye hivyo vituo?
 
Ndio hapa tunapoongelea kila siku uwepo wa system imara itakayokuwa inasimamia mambo kama haya na kumaliza maujinga kama haya ili watu makini na maisha ya watu. Tuna mawaziri, makatibu, RC's ,DC's, DED, RAS nk woote hawa wanafanya nini kushindwa kusimamia mambo serious kama haya?
tatizo ni kuwa tuna watu maofisini ambao sio pro active. yaani hawawezi kufanya jambo mpaka waambiwe. na pia kuna viongozi maofisini (maboss) sio pro active na wapo rigid wanapenda kufanya kazi kwa namna ile ile as long as hakuna ubaya uliowahi kutokea. pia hatupendi kujifunza kwa wenzetu walioendelea wao huko kwao mbona hakuna matatizo kama kwetu? tukijifunza tutajua namna ya kukabiliana na matatizo. watu kama sumatra/polisi wawe na utaratibu wa kukagua chombo chochote kile kinachohudumia raia. tena kwa kushtukiza. afsa atakaekutwa hafati utaratibu apelekwe mahakamani na akidhibitika afukuzwe kazi. kuna watu wengi wanapenda kuajiriwa na wana weledi ila nafasi ni chache. mtu akilijua hilo hatafanya masihara kwenye sehemu yake ya kazi.
wenzetu huwa wanaenda mbali zaidi mfano kama abiria hana kitambulisho asikatiwe tiketi. na asisafiri. ukikamatwa umemsafirisha abiria asie na kitambulisho ni kesi inayoweza kusababisha kampuni yako kufungiwa.
 
Ila hii ishu ya kuuana kwa makusudi au sijui nimeseme kuuana na kujiua wenyewe sijui itaisha lini, hata mv bukoba tatizo lilikuwa ni kuzidisha watu, na hii nayo hivyo hivyo, hivi kweli kivuko cha kubeba watu 100 kinabeba watu 400? hakuna ukaguzi kwenye hivyo vituo?
Umenena
 
Tusilaaumu sana maan ndio asilimia kubwa tunavyoendesha mambo yetu. Mfano ingekuwa hakuna ajali naamini kuna watu hapa wangeambiwa watoe taarifa zao zote wangelalamika.

Pia kwa asili ya uendeshaji vivuko tanzania iko hivyo hivyo..hivi ni nani Kigamboni huwa anaandikisha majina?
 
Jamani mlitaka sfanye nini wakati hakuna vifaa vya kuokolea muda huo?? Na sio kwamba atakuwa alijiamulia tu mwenyewe, hao wazamiaji hawana vifaa vya kufanyia kazi kwenye mwanga itakuwa gizani?? Ni aibu kwa nchi, hatuko tayari kwenye majanga!! Ya nchi kavu tu yanatushinda itakuwa ya majini??
Vifaaa vyakukesha kulinda kura za chama penda vipo lakin?
 
Back
Top Bottom