Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere kumemlazimu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri Denice James kusitisha ziara yake ya siku tano ya kukagua uhai wa Jumuiya na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2015-2020 katika maeneo yanayowahusu vijana ili kushiriki zoezi la uokoaji.
View attachment 873271
Usahihi n kwamba zoezi la oujkoaji lilisitishwa jana na mkuu wa mkoa. Kinachoendelea ni uopoaji wa maiti.
Naomba ikibidi barua ifanyiwe masahihisho.
 
Ni jambo jema kila lakheri.Wapatikane vijana wenye sifa,kuogelea na ukakamavu,sio mradi vijana wa kufanya selfie.
 
Kazi ya uokozi haijakamilika unatangaza namna ya kufanya mazishi na yawe ya namna gani huyu waziri bana nilidhani angekuwa field akishughulikia namna ya kuokoa habr za mazishi atoe hata waziri wa habari kuonyesha hata kwa kufake kuwa alisaidia yeye anaandaa mazishi na viongozi gani wahudhurie

Hizo gharama za mazishi kwanini mchana wa jana wasingenunua taa ili zisaidie kuondoa giza walilodai kuwa kikwazo kwa wao kuokoa sijui mawaziri wetu wapo kujibu tu maswali bungeni au vipi maana kwenye vitu vya msingi ambapo tungeona uwajibikaji wao hatuuoni kabisa kwa waziri makini hii ilikuwa sehemu ya kushughulika kwelikweli habari za mazishi angetangaza hata mkuu wa mkoa
 
Sio picha ya tukio mkuu.
Wanahabari wetu ni wavivu sana,sijui ndivyo wanavyofunzwa huko vyuoni?
Au ndio tabia ya kupenda kuwa wakwanza kutoa taarifa.
Mkuu Kweli Tupo Kwenye Mtanziko
Hadi Picture Jamani
Bora Umetufumbua Macho
Nimeona Television Zetu Zote Zimeingia Kwenye Mtego
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema mazishi ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya Mv.Nyerere iliyotokea Septamba 20 huko kisiwani Ukara, Ukerewe mkoani Mwanza yatakuwa ya kitaifa ambapo viongozi wakuu wa kitaifa wanatarajia kushiriki mazishi hayo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe.
Akiongea na ITV Mhandisi Kamwelwe amesema shughuli za mazishi hayo zitagharamiwa na Serikali na kwamba utaratibu kamili wa eneo yatakapofanyika mazishi hayo utatolewa baadaye.

Hata hivyo Mpaka sasa zoezi la uokoaji na uopoaji wa miili ya watu waliokuwa kwenye kivuko cha MV.Nyerere linaendelea ambapo miili 94 ya watu imeopolewa na waliookolewa wakiwa hai wanazidi 40.

Vikosi vya uokoaji mkoa wa Mwanza vimeongezewa nguvu na vikosi vya mkoa wa Mara katika eneo la tukio ili kuongeza kasi ya kuopoa miili ya watu waliopinduka na kivuko hicho.

Aidha uongozi wa wakala wa meli mkoa wa Mwanza umetambua wafanyakazi wa kivuko watano ambao wamepoteza maisha akiwemo nahodha, fundi, Karani, mlinzi na mkuu wa kivuko, Kivuko hicho kilikuwa na wafanyakazi wanane.

Mamia ya wakazi wa Ukerewe wamekusanyika nje ya kituo cha afya cha Bwisya kutambua miili iliyoopolewa kwenye ajali ya kivuko cha MV.Nyerere iliyotokea wakati wakisafiri kutoka kisiwa cha Bugorora kwenda Ukara kwenye gulio.

Mwandishi wetu aliyepiga kambi katika eneo hilo ametueleza kuwa wengi wa walioopolewa hadi sasa ni wanawake.
Taarifa naipokea lakini ingekuwa na maana sana kama wangeshulikia tatizo la kivuko baadala ya kusubiri utaratibu wa maziko ya waTZ wenzetu. Waziri hicho kivuko kilishalalamikiwa bungeni kitambo sana. Ona sasa unakuja na habari ya kuzika watu!!!!!!! Please step back and rethink.
 
Kuwajibika kwa uzembe ni lazima siyo ombi kwa ajali ya mita 50 kabla ya kutia nanga ''Ajali inatokea saa 8 uokoaji usio kamilifu uanze rasmi saa 12 ni aibu
 
Dah majuzi waziri mmoja alipata ajali ilipatikana helicopter ya fasta kumuwahisha muhimbili, Jana mamia ya ndugu zetu maskini wanaangamia taa tu ya kumulika ili kuendelea kuwaokoa ndugu zetu maskini inakosekana na zoezi la uokoaji linasitishwa tukiwa hatujui hatma ya ndugu zetu...nawaza kama hawa voingozi wetu wanajali maskini au wanajaliana wao kwa wao
utawala huu haujawahi kumjali mtanzania. achana na tamthilia za kwenye tv
 
Vijana ni tanuru LA fikra na jeshi la akiba, hongera UVCCM kwa uamuzi mzuri, mwacheni olesosopi awe propaganda machine na kibaraka wa mbowe. Mmeonyesha njia, wale waachane na vipressconference vyao
 
Jamani mlitaka sfanye nini wakati hakuna vifaa vya kuokolea muda huo?? Na sio kwamba atakuwa alijiamulia tu mwenyewe, hao wazamiaji hawana vifaa vya kufanyia kazi kwenye mwanga itakuwa gizani?? Ni aibu kwa nchi, hatuko tayari kwenye majanga!! Ya nchi kavu tu yanatushinda itakuwa ya majini??
Lakini pesa za kuwanunua akina Waitara na Mtatiro zipo, si ndio?
 
Hahahaha nimecheka sana,yaani hawa UVCCM kwasasa kazi yao ni kuokoa na kuwatakia la heri wanafunzi wanapofanya NECTA,hawana jipya.
 
Back
Top Bottom