Inatia uchungu sana unapogundua mtu uliyekuwa unamheshimu kuwa ni mtu makini na mwenye busara ndani ya JF ni "bwege na mlamba viatu" Mimi nimefiwa na ndugu zangu kwa uzembe wa serikali siwezi kupokea maoni ya kipumbavu kama haya ya kwako mleta mada na vimada wenzio. Naijua MV Nyerere, naijua MV Ukara. Najua matatizo yake siku nyingi na jinsi tatizo la usafiri lilivyo kubwa Ukara na Ukerewe kwa ujumla. Najua upuuzi wa wapuuzi wanaoshughulikia usafiri wa majini ndani ya ziwa Victoria. Kama ajali ingetokea siku 2 nyuma Mimi nisingekuwa naandika hapa na picha ya maiti yangi ingekuwa mitandaoni ingawaje wengine wasingejua huyu ndiye Bila bila. Kazi yangu imenipeleka katika visiwa hivi vya Ukerewe, Ukara, Kweru, Ilugwa, Kamasi nk. Naongea ninachokijua, hivyo watu wanapolaumu serikali wanajua wanachokiongea kwa jinsi kifo kilivyokuwa usoni mwetu kila siku tunayopanda kivuko hiki. Nanyamaza ila Mungu anawaona nyie wenye HERI.