Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Si pingi kwa ubaya Ila kwa kuepusha mabaya..

Enyi watanzania.. kweli mimi naunga mkono wachache ambao wanapinga uchangiaji wa rambirambi kwaajili ya ajari mbaya iliyotufika watanzania wote kwa ujumla wetu .

Sababu mpaka sasa hakuna taarifa zilizo weza kuthibitisha ni watu wangapi walio kuemo katika meli(kivuko) #hivyo familia zinazo passwa kuhaniwa ni unknown

Pili imekua kamchezo wananchi kutoa rambirambi Na rambirambi kupelekwa kusiko julikana
#yalinihuzunisha yaliyotokea kwenye maombolezo ya wadogo zetu *wa kwa mgambo the don. Wa A. Town*

Tatu.. still hakuna muongozo wowote ulioafikiwa wa kuweza kuzitambua familia zilizo patwa Na misiba


It's too early for that watanzania msije pigwa mkaambiwa pesa hazijulikami zilikoenda

Nawasilisha ..
 
FIKRA ZANGU KUHUSU KUPINDUKA KWA MV NYERERE.

Na Sir Taylor.

Habari ndugu zangu, kwanza nianze kwa kutoa pole kwa ndugu,jamaa,marafiki na kwa Taifa zima kwa kufikwa na janga hili baya kabisa linahusu UHAI wa binadamu.Mungu aendelee kutupa roho ya amani na utulivu katika kipindi hiki kigumu.

Kuna mambo mengi ya kuongelea au kutoa maoni katika hii ajali,ntaongelea baadhi kadri ntakavyoona inafaa.

Niongelee KUPINDUKA kwa kivuko,kwanza hapa lazima tujenge picha ya process ya ĶUPINDUKA na sio KUZAMA.Kupinduka kwa meli ni kitendo cha ghafla au niseme cha papo hapo tofauti na kuzama ambapo huu huwa ni mchakato kidogo.Na hapa ndipo utaona utofauti wa UOKOAJI na UOPOAJI.Meli au kitu chochote cha majini kinapozama uwezekano wa kuokoa huwa mkubwa sana coz hii ni process na hapa utaona nahodha anaweza toa taarifa kwa abiria na mamlaka mbalimbali kwa ajili ya msaada. Hapa ni rahisi abiria wanaojua kuogelea kujitupa majini na kuogelea na wale wasio na uwezo kutafuta vifaa vya kuogelea na kujitosa majini kuokoa UHAI wao.

Zoezi la UOKOAJI hapa sio gumu sana kama vifaa vipo vya kutosha na kuna umakini mkubwa.

Tukija katika Hili lililopo saizi ni kwamba kivuko KIMEPINDUKA.Hili ni swala la ghafla,sio nahodha au nani anaweza toa taarifa ya dharula kwa ajili ya msaada.Utaona ni vigumu kwa abiria kuwa na mda wa kuvaa vifaa vya kuogelea na ni wachache sana kama hata tulivyoona walifanikiwa kuruka na kuanza kuogelea au wengine kupita chini chini na kutokea upande wa pili.Na kwa tukio kivuko kilikua karibu na bandari so nafikiri hata kina chake sio kirefu zaid ambapo naweza sema wengi kivuko kimewakandamiza chini.

Tukija swala la UHAI wa binadamu,binadamu hawezi kaa kwa saa nzima chini ya maji bila vifaa vyovyote vya upumuaji na akabaki HAI. Kama kivuko kilipinduka saa 8 ni vigumu sana kufika saa 9 huko chini ya maji watu wakaendelea kuwa HAI. Na kingine lazima tujue mazingira ya kivuko,kivuko hakina sehemu kwamba kikipinduka au kuzama kuna sehemu binadamu anaweza ajifiche asipatwe na maji.

Kama nilivyozungumzia Hali halisi ya tukio,tuje kwa mamlaka husika juu ya ushughulikiaji wa tukio hili.Ni vigumu sana baada ya nusu saa kupata watu walio HAI, hivyo kilichokuwa kinafanyika ni UOPOAJI na sio UOKOAJI.Huu ndio uhalisia wenyewe ingawa kwa nature ya binadamu hata kama anajua mgonjwa wake hawezi pona lakini ni lazima aendelee kumpambania tu kwa vyovyote vile,hivyo hata katika tukio hili kuna watu ambao bado walikua wanaamini huko chini ya maji kuna ndugu zao bado wako HAI.

Swala la serikali kupitia RC kusema wanasitisha UOKOAJI kisa GIZA,ilikua ni kukosa BUSARA tu coz hata walichokuwa wanakifanya sio UOKOAJI. Hata kama serikali ilijiridhisha kuwa hakuna aliyehai huko chini lakini bado sio BUSARA kwa watu walioweka matumaini ambayo ni hewa kuwa kuna ndugu zao watakua HAI huko chini eti ni GIZA so tutaendelea kesho. Huyu RC amekosa BUSARA na hata upande wa kisiasa tunasema hana UTASHI WA KISIASA.Kwa BUSARA tu serikali ingeweza kuonesha juhudi za UOKOAJI hata ka sio UOKOAJI ili kuweka matumaini kwa ndugu kuwa serikali inapambana.Hata madaktari hujua mgonjwa huyu haponi lakini hukuti juhudi za kumhudumia mgonjwa zikipunguzwa tena waziwazi mbele ya ndugu wa mgonjwa. Hizi ni BUSARA ndogo tu wala sio lazima uende chuo au wapi.

Mwisho niseme serikali iwawajibishe wote waliohusika na hili swala,hapahitaji uchunguzi hata kidogo. Kivuko kinabeba watu 101 we unabeba watu zaidi ya 300,mahindi, cement na vitu kibao. Unataka uchunguzi wa kwanini kivuko KIMEPINDUKA kweli?Huyo RC naye atumbuliwe coz swala la BUSARA na maadili kwake ni zero.
 
Naona kashaanza kuvuruga ushahidi kwa kusema aliyekuwa anaendesha ni deiwaka! Halafu anatuhimiza tusubiri uchunguzi!!!
Kuna sehem nimesoma nahodha pia nae kafariki, sasa sijui alikuwepo tu kule juu ila akawa haendeshi
 
5422A072-89EF-42D3-8034-4B875A8A95BA.jpeg
 
Kwanza tujiulize kivuko kilipinduka saa 8 mchana,je tuseme saa 10 au 12 kuna raia yyt anaweza bado akawa hai?Kwenye ferry kuna sehem yyt mtu anaweza jificha endapo kikazama na maji yasimfikie?

Mimi mafikiri ni alikosa kauli ya busara tu juu ya usitishwaji wa zoezi lkn naamini baada hata lisaa halijakatika toka izame hakuna raia aliyekuwa hai na waliopatikana hai ni wale walikuwa wanatapatapa nje ya kivuko na sio waliofunikwa.Hapa jamaa niseme tu walikosa utashi wa kisiasa jinsi ya kuwapumbaza wananchi na kwa Mimi wakiendelea tu na zoez kujifanya wanaokoa kumbe zoez ni kuopoa.
Watu wanadhania kuokoa watu kwenye maji ni sawa na kwenye migodi ambapo hata wiki kadhaa bado unaweza kukuta watu wakiwa hai!! Na kibaya zaidi hii ilipinduka bora hata ingekuwa imezama!!
 
Kuna kitu kwenye hizi updates sijakielewa. Kuna taarifa mbili kuwa, Nahodha anashikiliwa kwa kumpa deiwaka ambaye amesababisha ajali; taarifa ya pili inasema Nahodha Mkuu ni moja ya waliofariki! Hapa, sijaelewa.

kwa nilivyoelewa, Nahodha na mkuu wa kivuko ni miongoni mwa waliokufa, Nahodha aliyekufa ni deiwaka ila bado anaitwa nahodha maana ndio aliyekuwa responsible wakati chombo kinazama. Nahodha mwenyewe muajiriwa kama nahodha na anyetambulika na mamlaka kama nahodha halali wa kivuko hakuwa onboard alikuwa onshore.. Ni shida zile zile za wabongo kuwa wazembe kwenye kutimiza majukumu.
 
Back
Top Bottom