Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Umetusaidia sana kutoa muongozo kwamba hakuna kurusha upuuzi wowote mitandaoni kuhusu ajali ya Mv Nyerere. Asante sana, kwani hali mitandaoni ilikuwa mbaya sana
UPDATES:
---------------

IDADI YA WALIOFARIKI YAFIKIA 209.

TIGO YATOA RAMBIRAMBI MILIONI 150.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe, amesema miili iliyoopolewa hadi sasa ni 209.

Waziri Kamwelwe amesema zoezi la uokoaji linaendelea na kwamba miili iliyotambuliwa hadi sasa ni 172.
 
wanabodi tafadhalini naomba msaada wa kufikiria maana mimi naona kama nafikia etc,
hivi kweli watu wachache wanaoweza kusogea kwaajili ya kuteremka wanaweza kusababisha imbalance ya chombo kikubwa kilichobeba magunia na magari yenye mzigo mzito?

kwani na magari yalisogea au ilikuaje na magunia je yalisogea ili yateremshwe?

nashimdwa kuelewa kama ni kiki au ni nini,, haingii akilini hata kidogo. magunia 100 yanaweza kuwa na kilo 10000 na kama kulikuwa na gari lenye vifaa vya ujenzi inaweza kuwa ni kama kilo 2000,..jumla ni kilo 12000,,, na kwa idadi ya watu 400 wanaweza kuwa na uzito wa kilo 20000,,,je inamaana kwamba watu wote walisogea kwenye kale kanafasi kadogo na kusababisha hiyo imbalances? maana haiwezekani... ile nafasi ya kuteremkia huwa si kubwa kiasi kwaba watu wote 400 wasogeepo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


we are in the left track indeed.
 
Sipingani na utaratibu wa kawaida wa kuchangiana na kuwafairiji wenzetu waliopatwa na huu msiba mkubwa...
Ila serikali yetu badala ya kuongeza nguvu kwenye uokoaji wa watu wanakimbilia kuchangisha rambi rambi...
Hatujasahau
1.rambirambi za luck vicent iliyouaa watoto wetu
2. Rambirambi za tetemeko la ardhi
Je na hizi zitawafikia walengwa???
Hizo wanawachangishia akina waitara,subirini kapu lijae muone watakavyo Fanya hao panya
 
Vyama vya upinzani haswa CDM iliyo na MBUNGE wa Ukerewe ilibidi wawe mstari wa mbele kusaidia wahanga wa tukio husika
Ni kweli na siyo kusaidia serikali. Baadhi ya marehemu walikuwa wapitaji tu maana nasikia mwingine kaenda kuzikwa Nansimo Bunda, huyu Nani atamkumbuka na rambirambi siku hizi ni dili?
 
UPDATES:
---------------

IDADI YA WALIOFARIKI YAFIKIA 209.

TIGO YATOA RAMBIRAMBI MILIONI 150.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe, amesema miili iliyoopolewa hadi sasa ni 209.

Waziri Kamwelwe amesema zoezi la uokoaji linaendelea na kwamba miili iliyotambuliwa hadi sasa ni 172.
Hiyo hela waliotoa tigo sijui itafika na kama ikifika, sijui itafika yote?
 
Kuzuia mafuriko kwa mkono haijawahi kufaulu popote pale duniani

Nchi inaongozwa na vichaa kwa hiyo haitupi tabu sisi na kauli zenu za vichaa
 
Back
Top Bottom