Ndugu wanabodi;
Ajali ya MV Nyerere imeleta msiba wa kitaifa ambapo zaidi ya Watanzania wenzetu 225 wamepoteza maisha.
Idadi hiyo ni kubwa sana kwa taifa letu. Hivyo ni matarajio yangu kuwa hill si suala LA kutuma uwakilishi Bali viongozi wote wa kitaifa wa vyama vya siasa,madhehebu ya dini na taasisi binafsi wakiongozwa na Rais wa JMT walipaswa kuhudhuria.
Sasa ukipeleka uwakilishi kwenye jambo kubwa la kitaifa kama hill yaani wewe unakuwa na jambo gani la kitaifa jingine?
Namshauri Rais afike Ukara yeye mwenyewe asisimuliwe na MTU ktk hili.Nawashauri viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa wafike wenyewe Ukara wasipige lamli wakiwa DSM.
Tukishindwa kuonesha umoja wetu kama Watanzania ktk hili tutaonesha maadili na umoja wa Utanzania wetu ktk lipi?
Nasisitiza tena Rais ufike Ukara,tena ktk kipindi hiki cha majonzi vinginevyo Mimi kama RAIA mwema nitaona umelichukulia janga hili sio kwa uzito unaostahili.Nakumbuka ulivyowatembelea wagonjwa na majeruhi mbalimbali huko muhimbili .Naamini hata ktk hili utafika huko Ukara kuwafariji wafiwa ktk kipindi hiki hiki cha majonzi na si muda mwingine.
Nasisitiza tena viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa,madhehebu ya dini na taasisi mbalimbali mnapaswa kufika Ukara kufariji wafiwa ktk kipindi hikihiki cha majonzi. Hii itasaidia kudumisha maadili yetu kama Watanzania na kuonesha mshikamano wetu kama taifa ktk shida na raha.