Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Wakati Mungu anamuamrisha Nabii Nuhu ajenge boti kubwa lenye uwezo wa kubeeba viumbe na baadhii ya binadamu nadhani nuhu mwenyewe alijua mawazo ya munguni huwa hayana makosa,na kweli safari ilikuwa salama salimini.

Sasa ngoja uyasikie ya SUMATRA hawa jamaa walipopewa mamlaka ya kudhibiti chombo hicho chicho ndio unasikia vilio kila teo ni kwa nini chombo kilichopendekezwa kubeba kizazi cha watu wema ambacho katika maoni yangu ndio chombo salama muliko vyote SUMATRA wazembee kiasi hicho.

Kama SUMATRA wangelipewa jukumu la SAFINA si wangemgomea NUHU kwamba "Mzee hapandi mnyama yoyote hapa tunaijaza hii boti na mapipa ya mvinyo kwanza halafu ndio hivyo vinyama vya mwitu vitakuja juu yake"
View attachment 875233
SUMATRA WANGEPEWA KAZI YA KUISIMAMIA SAFINA MAMBO YANGEKUWA HIVI.


Kwikwikwiiiiiiiii!!!!Hiiiiiiii Wajameeeni nimechekaga sana!!!!
Sasa mm naulizaga hivi....ina maana Nuhu wa sasa ni Magufuli na Safina ni MV Nyerere au?Hiihiii wajameni alakini naokopaga Yale Majitu yasiyojulikanaga kwa sasa!!!!!!
 
Kwahiyo mawasiliano na muumba yalionyesha kuwa siku zinazofuata hali ya hewa itakuwa nzuri?
 
Huyo Dr jiwe yeye kwenye mambo ya kutafuta kiki za kisiasa ili kulinda madaraka yake hata ya hovyo kiasi gani utamuona kaenda
Kwa nchi ambazo zimeendelea. kiongozi. Wa upinzani anaweza kutembelea taasi yeyote ile ya SERIKALI na pasitokee mtafaruku, Mbowe anaweza kwenda Hospital ya Muhimbili,?, kesho utasikia. Mkurugenzi mkuu amefukuzwa. Kazi
 
Kwahiyo mawasiliano na muumba yalionyesha kuwa siku zinazofuata hali ya hewa itakuwa nzuri?
 
Tulipofikia wapo Watu ambao wako radhi majanga yatokee ili waweze „kukua“ kisiasa. Ni janga la Taifa. Zamani Nilikuwa najiuliza Hawa Boko Haramu kama wanapigania madaraka why wanateka mpka mabinti why wasipambane na wanajeshi nk na wanasiasa? Nimegundua kwa wanasiasa iwe Marekani, China, Tz —- It’s the END that justifies the means. Tuwaombee marehemu wetu wampumzike kwa amani. Amen.
 
Kwa nchi ambazo zimeendelea. kiongozi. Wa upinzani anaweza kutembelea taasi yeyote ile ya SERIKALI na pasitokee mtafaruku, Mbowe anaweza kwenda Hospital ya Muhimbili,?, kesho utasikia. Mkurugenzi mkuu amefukuzwa. Kazi
Au unasikia tu katiwa ndani kwa kufanya mkusanyiko usio halali hata wa watu 5 tu
 
Amani ya bwana.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh John Mongella akihojiwa na vyombo vya habari ametolea ufafanuzi ule upotoshaji mkubwa uliofanywa na wanasiasa watafuta kiki mara baada ya kutokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kwenye ziwa victoria.

RC Mongella amesema yeye ni mkuu wa mkoa tu na wala si mtalaamu wa maswala ya uokoaji, hivyo alichokifanya na anachokifanya sasa hivi ni kupokea na kufanyia kazi maoni ya watalaamu wa uokoaji majini (divers).
Kabla ya kusitisha zoezi la uokoaji siku ya kwanza aliambiwa hali ya maji ziwani imeanza kuwa mbaya na kutokana na usiku ,hivyo angetumia kofia yake ya ukuu wa mkoa kulazimisha divers waendelee na kazi angeweza kusababisha madhara zaidi na angeweza hata kuwapoteza hao wataalamu wa uokoaji.

Maelezo ya mkuu wa mkoa ni majibu safi kabisa kwa wanasiasa wakurupukaji wanaopenda kudandia mambo bila kuwa na ushahidi wa maelezo ya kutosha.
Mara baada ya kutokea ajali hiyo wanasiasa kama Zito, Mbowe na Mbatia walikuwa na uwezo wa kufika eneo la tukio na kushirikiana na wafiwa kwa haraka mno hata kwa kutumia ndege lakini hawakufanya hivyo badala yake wakaanza kuitisha waandishi wa habari wakiwa Dar kutoa matamko na kupotosha watu ,huku wakijifanya wanaijua sana hali ya ajali kuliko watu waliopo eneo la tukio!!

Hali hiyo ya kutafuta kiki za kisiasa kupitia ajali na matatizo ya watanzania ilikemewa vikali na Rais wetu mpendwa Dr Magufuli. View attachment 875133
Alikuwa na wajibu wa kuhoji mantiki ya maoni hayo ili kupima.Siyo kukubali tu
 
hawa wanalindana ngumu kuondolewa huyu mama wa OSHA kawekwa pale na mtu mzito sana nchi hii. Sidhani kama ataondoka let alone kuondolewa
 
Hiyo familia yako dakika hii ukiwaambia kijani yako wanakushangaa tu.

Haya maneno ya kejeli yalitolewa sana na CCM kabla ya 2015 ila saivi CCM wanajitahidi kuwa wanyenyekevu. Kwa wazoefu humu watamkumbuka @MalariaSugu alikuwa na majibu na maneno ya kejeli na ya kujitoa akili kama haya. 2020 na nyie tutawapa funzo, muda wetu na sisi utafika ila mjue tu Ukerewe mmeshaipoteza.
 
Ndugu yangu, nikuombe tuyaache haya, ungejua kuwa mimi siyo mwanasiasa, ungenielewa. Yote, tumeshaambiwa, first rescue divers walikuwa ni wale wavuvi wadogowadogo! Tuishie hapo.......
Wavuvi wadogo wadogo hawawezi kuwa divers, hapo ni sawa na kuwaita mafundi mchundo Wakandarasi. Naomba tuwe na tabia ya kuheshimu taaluma za watu mkuu.

Pili, sijakulabel uanasiasa, balii nimekumbusha ya kwamba kuna masuala hayahitaji Siasa na mihemko. Ikiwemo masuala ya kitaalam kama ya Uokoaji chini ya maji. Mwaka 2014 kuna kivuko kilizama huko Korea kusini na Kuua watu takribani 304. Kuna Diver(s) walipoteza maisha katika harakati za uokoaji. Kwa hiyo wito wangu wa sisi wakina Kipozeo tusihemke na kukimbilia kutoa lawama bila kuwa na uelewa wa uendeshaji wa zoezi zima.
 
Nimejiuliza sana ili swali hasa baada ya kusoma katika gazeti la Chadema liitwalo Tanzania Daima kwamba uongozi unakaribia kumsajili maalim Seif katika chama chao. Ndiposa najiuliza mgombea urais mtarajiwa ndio kipaumbele cha Chadema kiasi cha kumtelekeza mbunge wa Ukerewe my Joseph Mkundi?!!!
Si mmeshasema mnae IJIIIIpiii wakamatwe ulitaka waje muwakamate, msiba wenu na mmeshauteka na mwenyewe mmesema kila saa alikuwa anawapigia simu kujua kinachoendelea mnatafuta wa kula nao janga, nyie mmerikologa kunyweni lenu hilo.
 
Jimbo la Ukerewa lipo chini ya CDM ila ndani ya CDM kuna ubaguzi wa kijinga sana. Na uhakika hili balaa lingetokea Arusha au Kilimanjaro CDM makao makuu wangetuma mtu wa kuwawakilisha kwenye msiba.
Wapinzani wanalaumiwa kwa kuzama kwa kivuko,hahahaaaaaa!Wakati wwngine wanazika,mkuu wa nchi anapata breakfast na TRA wa barabarani na makamera kibao huku wakiwa na nyuso za bashasha
 
Yaani..huyu mbowe si alijidai kwenda kwenye msiba wa baba mkwe wa kikwete..sasa nini kimewashinda kwenda kuwazika watu waliowasaidia kuongeza ruzuku ya chama? Umuhimu wa wakerewe ni kwenye kura tu na ruzuku
Mkuu uko sahihi Na kule kwa Kikwete ulikuwa msiba uliojaa CCM Na nguo zao na ukiwa Chini ya CCM alienda kule Ukerewe zaidi ya watu Mia mbili wapiga kura wake wamekufa hajakanyaga.Kule kwa Kikwete aliyekufa alikuwa mtu mmoja.
 
Ni rahisi Sana kumtambua kiongozi mtupe kichwani, itokee inshu inayohitaji majibu ya papo kwa papo bila kupewa maagizo kutoka juu, utaona majibu anayotoa ni aibu, ndo Kama huyu RC.
cha kushangaza Kuna mtu wamemuokoa Siku tatu baada ya tukio akiwa hai, je ni wangapi ambao tungebahitisha kuwaokoa?
 
Back
Top Bottom