Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Waziri Mkuu ambaye ameongoza mazishi hayo leo (Jumapili, Septemba 23, 2018) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, amewataka Watanzania waiache Serikali na vyombo vya dola viendelee kufanya kazi yake.

“Wito wa Serikali kwenu wote, ni kuwasihi tushikamane na wenzetu waliopoteza ndugu zao, wakiwemo wazazi, kaka, dada na watoto. Ninaomba tuiache Serikali na vyombo vya dola viendelee kufanya kazi yake. Tuendelee kuwa wavumilivu,” amesema.

Akiwasilisha salamu za rambirambi kutoka kwa Rais Magufuli mbele ya wafiwa na waombolezaji, Waziri Mkuu amesema: “Mheshimiwa Rais alipokea tukio hili kwa mshtuko mkubwa na anawapa pole sana wafiwa wote pia anawaombea majeruhi wote wapate ahueni mapema.”

Amesema jumla ya watu 224 walipoteza maisha kutokana na ajali hiyo. Kati ya hao, miili 214 kati ya 219 iliyotambuliwa, ilichukuliwa na ndugu zao. Miili minne haikuweza kutambuliwa lakini ipo miili mitano ambayo ilitambuliwa na ndugu zao na hao ndugu wakaona ni vema wazikwe hapa eneo la tukio. Kwa hiyo leo tutawazika ndugu zetu tisa katika eneo hili,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali imechukua hatua ya kuunda tume ya uchunguzi na kuahidi kwamba tume hiyo itatangazwa wakati wowote. “Tume ikikamilisha kazi yake, wote watakaobainika kuwa wamehusika watachukuliwa hatua mara moja,” amesema.

Ili kukabiliana na tatizo la usafiri lililopo, Waziri Mkuu amesema meli ya MV Nyehunge imeanza kutoa huduma ya usafiri wa muda badala ya MV Nyerere iliyokuwa ikitoa huduma kati ya bandari ndogo ya Bugolora, Ukerewe na kisiwa kidogo cha Ukara.

Amesema jitihada za kuivuta meli ya MV Nyerere iliyopinduka zinaendelea na kwamba maafisa wote wanaohusika na usafiri wa majini ambao walizembea kwenye suala hilo, wamekamatwa na wameanza kuhojiwa.

Akigusia chanzo cha ajali hiyo, Waziri Mkuu amesema inasadikiwa kivuko cha MV Nyerere kilibeba mizigo mingi kuliko uwezo wake ambao ni wa kubeba tani 25 za mizigo, magari matatu na abiria 101. “Hadi sasa inaonesha kulikuwa na watu zaidi ya 260, yaani 41 waliookolewa na 224 waliopoteza maisha,” amesema.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wote wa Ukara waliojitokeza kusaidia kazi ya uokoaji tangu ajali hiyo ilipotokea. Pia aliwashukuru wote waliotoa michango mbalimbali, watumishi wa hospitali za Bugando, Sekou Toure, Ukerewe, kituo cha afya cha Bwisya na timu nzima inayofanya kazi ya uokoaji na uopoaji wa miili kwa kazi kubwa waliyoifanya.

Wakati huohuo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenista Mhagama ametangaza namba ya tigopesa ambayo wananchi wanaweza kuitumia kutuma michango yao kwa ajili ya waliopatwa na maafa hayo.

“Tumefungua akaunti ya maafa kwenye Benki ya NMB tawi la Kenyatta lakini ili kurahisisha upokeaji wa michango kutoka kwa wananchi wa kawaida, tumesajili namba ya tigo yenye namba 0677-030-000 kwa jina la RAS Mwanza. Naomba wale wasioweza kwenda benki watumie namba hiyo,” amesema.

Kuona Matukio picha zaidi

WAZIRI MKUU AONGOZA VIONGOZI WA CCM NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI UKARA MWANZA LEO. ~ UVCCM BLOG
IMG-20180923-WA0215.jpeg
IMG-20180923-WA0216.jpeg
IMG-20180923-WA0211.jpeg
IMG-20180923-WA0256.jpeg
IMG-20180923-WA0253.jpeg
IMG-20180923-WA0255.jpeg
IMG-20180923-WA0218.jpeg
 
Sasa bado hajasema yule kubwa lao !
Bwana Mkubwa, naona umefungua kinywa mapema mno. Sidhani kama watu watachanga tena. Rambirambi huliwa na wafiwa. Laiti ungelisema zitawasomesha hata mayatima walioachwa. Ni mawazo yangu tu jamani mnisamehe kwa domo kaya hili
 
Tatizo jiwe alifikili maafa ya Kagera ndo ya mwanzo na mwisho kwanye uongozi wake, hatuwezi kuchangia kwenye account hizo walizotengeneza, tutaipeleka mchango yetu kwenye familia za wafiwa.
 
Japo mimi si CDM kwa hili naona chenga tu! wale RAIA wanaoishi ukara,ukerewe walimchagua Mbunge pia wana viongozi wao wa CDM,si lazima kuhudhuria physically kwa mantiki ya kwamba mwanasiasa fullani alikuwepo msibani, wengine wanaenda kwa ajili ya attention..niliitegemea wote watakuwa na mavazi ya msibani na kupongeza serikali na raia waliojitoa kwa ajili ya uokooaji ila baadhi walishazoea mambo ya chama chao na serikali..
 
Zile bilioni 7 alizolalamikia CAG zingeweza kununulia taa badala ya kuzipeleka Ufisadini ufipa!

Ukitaka kujua watu wamechoka na huu mwenendo angalia idadi ya waliochangia na kiasi kilichochangwa mpaka sasa. Na sasa itabidi tuwatake viongozi wa cdm watangaze kabisa hakuna mwanachama wa cdm kumzika wa ccm wala wa serekali. Na sababu ni jinsi mshikamano wetu wa kitaifa unavyoharibiwa chini ya awamu hii. Tukifika hapo lazima tutapata suluhu ya huu unyama, hapo tutaona hiyo nguvu ccm inayosema inayo mpaka kufikia kutumia mamlaka ya nchi kuwanyanyasa wapinzani. La kwanza na lililo wazi ni hiyo kushusha idadi ya wapiga kura, na sasa michango kukosa watu, na litakalofuatia ni kutangaza kutokushirikiana kwenye misiba na mambo mengine kama hayo. Na hili linawezekana kwani watu wamechoka kukalia kimya uovu.
 
Daah........Chadema inaangamia kwa kukosa maarifa!
Aibu kubwa Ile.Bora slow slow angekuwa ndo pekee amevaa na viongozi wengine kabda.Sasa wamama kibaoooo na manguo ya CCM AIBU mkuu.Nawe unaona aibu hapo Kwa hili.
 
Aibu kubwa Ile.Bora slow slow angekuwa ndo pekee amevaa na viongozi wengine kabda.Sasa wamama kibaoooo na manguo ya CCM AIBU mkuu.Nawe unaona aibu hapo Kwa hili.
ina maana ccm wanafanya siasa hadi kwenye misiba siku hizi?
 
Japo mimi si CDM kwa hili naona chenga tu! wale RAIA wanaoishi ukara,ukerewe walimchagua Mbunge pia wana viongozi wao wa CDM,si lazima kuhudhuria physically kwa mantiki ya kwamba mwanasiasa fullani alikuwepo msibani, wengine wanaenda kwa ajili ya attention..niliitegemea wote watakuwa na mavazi ya msibani na kupongeza serikali bila baadhi walishazoea Chama na serikali..
Mbunge Nassary alipofiwa na mbwa wake mjumbe wa kamati kuu na mbunge wa Arusha mh Jonathan alihudhuria mazishi.........nakukumbusha tu!
 
ina maana ccm wanafanya siasa hadi kwenye misiba siku hizi?
Msiba wote mkuu wamejaa wamama na majamaa yamevaa maccm halafu et "tuweke itikadi pembeni,msiba huu umetugusa wote"
Halafu tena"kuna watu wanataka kuutumia msiba kisiasa" Very stupid, Stupid kabisa.
 
Viongozi wa upinzani wamekasilishwa sana na tamko la mbunge wa Ukerewe (CDM) kuwa, mapungufu aliyowasilisha Bungeni, serikali iliyafanyia kazi! Viongozi wake wamechukulia kuwa amewazodoa kwa kiki waliyotarajia kuipata kupitia msiba huu.
Baada ya msiba tutamsimamisha uanachama
 
Mbunge Nassary alipofiwa na mbwa wake mjumbe wa kamati kuu na mbunge wa Arusha mh Jonathan alihudhuria mazishi.........nakukumbusha tu!
Sioni cha kujibu naona yote chenga tu, kuna wenzako wanauliza Rais kwa nini ajaenda? Kama Mkuu ajaenda na Wengine hawajaenda wana sababu zao na zinastahili heshima..
 
Mkuu sipingi usemayo, lakini haya mambo yanazidi kushika kasi, na njia zinazokubalika zinapuuzwa. Ngoja watumie mbinu ambayo haitawaacha wananchi na vilema. Je unahitaji cdm wafanyiwe unyama kiasi gani ndio mambo yabadilike? Walitangaza kujitoa, je hao ccm walijali? Uliona wale akina Butiku na kina Warioba wakifungua mdomo kama walivyofanya kabla ya uchaguzi wa 2015? Kama wapinzani wanafanyiwa unyama na hatua hazichukuliwi kwanini wasichukue njia nyingine itakayosababisha wananchi na wengine wenye ushawishi kutaka mambo yawe sawa?

Rais anazunguka anahubiri kwamba sehemu ambayo kuna mpinzani ni mtoto wa jirani unategemea nini. Hao viongozi wenye ushawishi kwanini hawakemei hili? Sasa hivi ni jambo la kawaida kabisa kuona vyombo vya dola kuwafanyia unyama wapinzani na imegeuka ni sahihi. Sasa inabidi watu wachore mstari kwa kutumia mbinu nyingine itakayogusa jamii nzima. Nadhani umeona michango ya huo msiba mpaka sasa, yote haya ni matokeo ya huu mwenendo wa awamu hii ya tano. Narudia tena viongozi wa cdm watangaze kimachomacho kwamba umoja wetu tuliotambia haupo tena, hivyo hakuna mwanacdm kumzika mwanaccm na kinyume chake. Mkuu huyo mbunge anajua hali halisi ilivyo, ni bora huu mwenendo uwe wazi sasa kuliko kufumbia macho kisha huko mbeleni nchi yetu itumbukie kwenye machafuko.
Kwa maana hiyo mngemshauri na mbunge wenu akasusia maziko basi halafu tuone 2020 kama mtakuwa na hadhi hata ya UDP. Acha kujidanganya eti CDM ndo nini sijui. CHADEMA inaweza kuwa kama NCCR, CUF UDP au PPT MAENDELEO! mda utatupa majibu na tutakutana hapahapa na vijisababu vya kwenye vijiwe vya kahawa na maisha yataendelea kuwepo.
 
Back
Top Bottom