Uchaguzi 2020 Ukara: Wananchi wamuua mtu aliyetaka kumteka mgombea udiwani wa kata ya Bwisya kwa tiketi ya CHADEMA

Hakuna sababu ya msingi ya kupigana kisa uchaguzi. Ni tabia mbaya na ushamba kumuumiza mwenzako kisa madaraka
 
Wewe ndiyo unaweka siasa mbele.
Kwanini tume na vyombo vya usalama vinashiriki kuharibu uchaguzi ?

Kwanini chama cha mapinduzi hawataki kushindana kwa hoja majukwaani ?
 
Hii roho mbaya ya kutekana inaonekana kushamiri. Kama waliweza kumthibiti wasingemua ili tujue ni akina nani waliowatuma.....
Hapana asee asingeshindwa kusema katumwa na chadema hao hao, ilo somo liwafikie na wengine wanaotumika kuvuruga uchaguzi..
 
Nchi hii ni yetu sote siyo Mali binafsi ya ccm na wanachama wake.

Sote tunatafuta uongozi ili tuboreshe kesho za watanzania kwanini tutumie bunduki na hila kutafuta ridhaa ya wananchi ?

Tujaribu kuwa watu na tuutambue utu wetu kama tunu yetu sote, kutenda haki siyo hisani ni sehemu ya utu wetu.

Kama unafanya propaganda za kisiasa mimi siyo sehemu ya hizo propaganda mfu.
 
Polisi wameshaenda kuchukuwa maiti, hivi ndivyo haswa inavyotakiwa kuwadhibiti watekaji hapa Tanzania, lazima codes zitumike, ili kuita msaada wa dharula wazungu wanaita SOS.
 
Ccm waachie wananchi wafanye maamuzi yao kama wao wanapitisha majina toka mifukoni mwao wananchi wana majina ya moyoni mwao
 
Hii ngoma ielekezwe kwa wasimamizi wa uchaguzi sasa. Mkiwakosa wao ondokeni na famila zao.
 
Yaani chadema walete habari kama hii bila picha?
Uongo mwingine bhana
 

Ni mjinga na mpumbavu atakayeaamini kuwa wapinzani wanasimamia polisi, TISS, PCCB, NEC, na wakurugenzi wa halmashauri.

Mimi CCM lakini nikiri kabisa kuwa tunafanya siasa za kishamba na kipumbavu kabisa.

Miaka mitatu tumeimba Hapa kazi na baadhi vitu vilivyofanywa na mwenyekiti wetu vinaonekana, sasa najiuliza hofu ya nini?
 
Hii roho mbaya ya kutekana inaonekana kushamiri. Kama waliweza kumthibiti wasingemua ili tujue ni akina nani waliowatuma.....
Naam, inasikitisha kupoteza uhai. Wanao teka ni CCM na dola ikiwasapoti, wala huitaji darubini kuona hilo. Tusingekuwq na state capture, tume wangeshafanya kitu zamani sana ku discourage hiyo tabia ya CCM. Tume ingewapa nafasi nyengine ya pekee wagombea/ chama kinacho poteza nafasi ya ushiriki kwa kufanyiwa hujuma za kihuni kama hizo. Hayo yote yanatokea tume ipo kimyaaaa!!!!!!..... na wakati mwengine maafisa wa tume hushiriki moja kwa moja na kwa uwazi kufanikisha hujuma hizo.
 


Nadhani sauti haitoshi ongeza sauti mkuu iweze kusikika vema
 

Mkuu ni kwamba unajifanya hujui kuwa ccm ndio wanaoratibu mambo haya ama? Kila mara nikikuambia toka awamu hii ya tano iingie madarakani tumeona chaguzi zilizoandanwa na ushenzi, ukatili, unyama na uhayawani wa wazi, ulikuwa unadhani natania? Na ukitaka kujua haya ni mambo ya kupanga kabisa, angalia mpaka mkurugenzi na polisi wanafanya haya haya matendo ya kihuni.

Ccm imeshachoka kushindana. Huko kwa waziri mkuu wagombea wa ACT wametekwa na kuachwa na vilema vya maisha. Huko ni kwa waziri mkuu, hao walio chini yake unategemea nini?
 
IGP aliposema waliorusha mawe wapatikane mbona wamepatikana, unganisha Dot.
 
Hii roho mbaya ya kutekana inaonekana kushamiri. Kama waliweza kumthibiti wasingemua ili tujue ni akina nani waliowatuma.....
Tatizo wananchi wamesha choka na wana hasira na chuki kubwa kutokana na matendo wanayo fanyiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…