Ukarabati 7.5B, Magogoni twende Kwa Facts! Mnaobisha Njooni Mnijibu

Ukarabati 7.5B, Magogoni twende Kwa Facts! Mnaobisha Njooni Mnijibu

commonmwananchi

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,377
Reaction score
1,956
Harufu ya "Mashaka" ni Kali, kuliko harufu ya "Ukweli!"

Hoja kwamba Bilioni 8 za miaka ile na Bilioni 7.5 za sasa, thamani ni tofauti sana, sio kweli.
Chukua exchange rate ya wakati ule na exchange rate ya sasa!

Wataalamu wakichambua zile Bil 7.5 za ukarabati wa MV. Magogoni. Walisema hivi:

1. Kile kivuko kinaendeshwa na engine 4.
2. Engine zile ni za caterpillar yaani zile machine kama za kuunda barabara.
3. Engine moja haiwezi zidi mil 350
4. Kwa kukadiria tu engine zote nne ni kati ya bil 1.2 na bil 1.5
5. Hiyo sehemu ya engine ndio project yenye, kubeba gharama kubwa zaidi kuliko sehemu nyinginezo zote.
6. Ukarabati mwingine ni Kukwangua rangi na kupaka mpya, kukarabati viti vyote vya abiria, kubadilisha Raba za milango, Rada nk.

Swali tunalohoji hapo ni:

Kama engine 4 ni kati ya bil 1.2 na 1.5, na matengenezo mengine tuchukulie basi mil 700, je hizi karibia bil 5.3 zinaenda wapi?

Nani yupo nyuma ya upigaji huu?
Nani alipanga matumizi haya akiwa na nani au kamati gani?
Waziri wa fedha anajua hili na aliwajibika kufatilia?
Kwa nini tukatengenezee Kenya wakati tuna Songoro marine ltd mnajaribu kwenda kuficha nini?

Je, TAKUKURU imeingilia kuchunguza sakata hili maana sio kitu cha kawaida na ukisikia minong'ono kibao ujue kuna uwalakini mahali.

Je, hapa si ndio malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa TAKUKURU yangeonekana?

Tafakari na chukua Hatua!
Hili suala sio la kisiasa!
Tunaongelea pesa za walipa kodi na wavuja jasho wa nchi hii.
Tunaongelea Tozo tunazotozwa kila uchao.

#Kataa wahuni

Pia soma bandiko langu la awali kuhusiana na hili sakata!
"Hili la Magogoni Wacha Tutunze Kumbukumbu."
 
Ilikuwa ni open bidding. Huyo Songoro Marine alisema angehitaji Tsh 10 Bilion, kwa hiyo akawa siyo responsive.

Technical wise ndugu commonmwananchi huwezi kuleta balanced argument hapa bila kuweka Tender Document.

Wataalamu wa Procument wanajua tender document ilikuwa inataka ukatabati wa aina gani!!
 
Hii nchi imekuwa shamba la bibi kwa mara nyingine.
Ebu pitia na hii taarifa ya whistle blower mwingine humu JF.
"
Kwa taarifa za uhakika kabisa ni kuwa waarabu wa Dubai na Saudia wanelekea kishiwa maeneo nyeti ya Taifa letu. Bandari ya Dar es Salaam tipo mbioni kukabidhiwa kampuni ya Dubai. Ndio maana jana mmeona Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE alikuwa Zanzibar kukamilisha mazungumzo, hamkuambiwa kwenye press ya Ikulu walizungumza nini.

Huu ni mwendelezo wa ziara ya yule mwana mfalme aliyekuja majuzi toka UAE akakutana na Pindi Chana Waziri wa kipindi kile wa maliasili ambaye aliondolewa siku mbili baadaye baada ya kuonekana mrasimu.

Kama haitoshi wizara ya maliasili akapelekwa waziri mkwe na Katibu Mkuu rafikiye ili wakamilishe madili na waarabu. Kama haitoshi Said Yakubu aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu pale Utamaduni akapandishwa Cheo kuwa Katibu Mkuu Utamaduni na leo hii yupo Saudi Arabia na Mwamfalme Binti eti wanaongea mambo ya utamaduni. Saidi huyu alikuwa msaidizi binafasi wa Ndugai ambaye maadili yake ni mashaka tupu, ni mbadhirifu na mdanganyifu na mpiga dili.

Kwa hili la UAE kupewa Bandari tayari kundi la kwanza la Wabunge lilipelekwa Dubai kuangalia namna hiyo Kampuni inavyoendesha bandari za huko na kundi la pili wanaenda India mwishoni mwa mwezi huu. Lengo ni kuwaziba midomo dili likikamilika kati kati ya mwaka huu.

Sikumpenda Magufuli kwa udikteta, wizi na ujambazi lakini angalau alijitahidi kulinda strategic resources za nchi kusalama kama bandari. Huyu wa sasa na hawa waarabu tunarudi enzi za Mwinyi na Loliondo. Nadhani tuutizame Muungano wetu vizuri pengine vya watanganyika vinafanywa kuwa vya bure pale mzanzibari anapokuwa rais."
 
Wizi wa huko ni zaidi 80% ndio mtu anaona kaiba
Yaani hata biashara ukicheka na mfanyakazi utaishia kuwa na 20% tu ya mauzo na mwisho unafunga biashara

Nchi inabebwa na mikopo na misaada la sivyo tungekuwa na vita
 
Tender documents pekee ndo zinaongoza uhalali wa gharama za ukarabati?

Hebu tupe za ununuzi wa kivuko kipya!!! KENGE

Kenge ni Wewe unae pinga ndie ungeleta hizo tender Documents ili tuone wao wali tender Engine moja kwa shs ngapi?

Kama bado unaamini tender Documents, sisi tunaangalia "Value of Money"

Dunia ya siku hizi mambo yako kiganjani.
Ukitaja kampuni tu....wengine wenye uelewa wanakuwa kwenye Price list ya bidhaa husika!
Bila hata kupanda ndege wala Baiskeli.
Tafakari.....
 
Ukweli ni kwamba hii nchi yq kisenge, wapigaji %kila eneo, na machawa ndio watu wanaopaswa kuchunwa ngozi hadharani. Majitu yanayoiba, wao kidete kuyatetea.
 
Tender documents pekee ndo zinaongoza uhalali wa gharama za ukarabati?

Hebu tupe za ununuzi wa kivuko kipya!!! KENGE
Kivuko kipya kwa design ile ile ni Tshs 20 Billion kwa sasa. Umeaikia wewe pimbi !!
 
Harufu ya "Mashaka" ni Kali, kuliko harufu ya "Ukweli!"

Hoja kwamba Bilioni 8 za miaka ile na Bilioni 7.5 za sasa, thamani ni tofauti sana, sio kweli.
Chukua exchange rate ya wakati ule na exchange rate ya sasa!

Wataalamu wakichambua zile Bil 7.5 za ukarabati wa MV. Magogoni. Walisema hivi:

1. Kile kivuko kinaendeshwa na engine 4.
2. Engine zile ni za caterpillar yaani zile machine kama za kuunda barabara.
3. Engine moja haiwezi zidi mil 350
4. Kwa kukadiria tu engine zote nne ni kati ya bil 1.2 na bil 1.5
5. Hiyo sehemu ya engine ndio project yenye, kubeba gharama kubwa zaidi kuliko sehemu nyinginezo zote.
6. Ukarabati mwingine ni Kukwangua rangi na kupaka mpya, kukarabati viti vyote vya abiria, kubadilisha Raba za milango, Rada nk.

Swali tunalohoji hapo ni:

Kama engine 4 ni kati ya bil 1.2 na 1.5, na matengenezo mengine tuchukulie basi mil 700, je hizi karibia bil 5.3 zinaenda wapi?

Nani yupo nyuma ya upigaji huu?
Nani alipanga matumizi haya akiwa na nani au kamati gani?
Waziri wa fedha anajua hili na aliwajibika kufatilia?
Kwa nini tukatengenezee Kenya wakati tuna Songoro marine ltd mnajaribu kwenda kuficha nini?

Je, TAKUKURU imeingilia kuchunguza sakata hili maana sio kitu cha kawaida na ukisikia minong'ono kibao ujue kuna uwalakini mahali.

Je, hapa si ndio malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa TAKUKURU yangeonekana?

Tafakari na chukua Hatua!
Hili suala sio la kisiasa!
Tunaongelea pesa za walipa kodi na wavuja jasho wa nchi hii.
Tunaongelea Tozo tunazotozwa kila uchao.

#Kataa wahuni

Pia soma bandiko langu la awali kuhusiana na hili sakata!
"Hili la Magogoni Wacha Tutunze Kumbukumbu."
••••Mwaka kesho uchaguzi Serikali za Mitaa, mwaka ufuatao uchaguzi mkuu. Haya mambo yanataka maandalizi mapema••••tumieni akili jamani
 
Engine wanayotumia hiyo hapo unaweza omba quote ya bei directly from caterpillar wenyewe. Ila sidhani kama inazidi ata $70000 brand new. Maana nimeona used nyingi bei aizidi $20000.

EAD3B3EB-7AC3-4669-BC33-A2594A0543C4.jpeg

Main parts zote za kuendesha hilo pantoni hizo hapo juu na sidhani kama zinafika ata $1 million brand new kwa pamoja.

Tells you ata hiyo billion 8 ya kununulia mpya gharama kubwa inaonekana zilikuwa kwenye steel, charged labour hours kwenye kuunda na faida ya muuzaji. Otherwise it’s a cheap ferry.

Sasa kama chuma sio chakavu hiyo gharama ya billion saba inatokana na nini wakati replacement parts azifiki ata billion mbili za kitanzania tena brand new.

Na kama chuma ni chakavu what’s point of repairing something which is worthless than it’s residual value at scrap metal price.

Anyway wacha na wengine wale hela yenyewe ni ya vitafunio vya chai tu ata kwa viwango vya Rugemalila seuse serikali yenye mihela mingi.

Hao watoto wa shule washazoea kukaa kwenye matofali na sakafuni anyway. Wasubiri raisi mwenye kujali kwa sasa ni kulamba asali tu.

Ujambazi huko kule kwenye matrillion ambayo bi tozo kaonya PPRA wasiulize kuhusu hizo tender.
 
Back
Top Bottom